Elections 2015 Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Karagwe - Septemba 22, 2015

Elections 2015 Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Karagwe - Septemba 22, 2015

Mkuu! Jukwaa la kampeni dhumuni lake kuu ni kuuza Sera ya chama chako,haswaaa kutoa ufafanuzi Juu ya maswala yaliyopo katika Irani...zilianza kashfa,zikaja comedy,zikaja matusi,maigizo...sasa imegeuzwa gym...doooh

Mwisho wa siku kuokota ma..kop...o.
 
Magufuli hajitambui anaongozwa na hisia tu ndio maana anaropoka
 
Alikuwa ana piga push up ,anajidai kwamba afya yake ni bora,kama ubondia ndo kipimo cha ikulu,basi Matumla angekuwa ikulu,viva EL
 
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge jimbo la Nkenge kupitia CCM Balozi Dk. Deodorus Kamara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mkutano maarufu kama uwanja wa Chakaza ,Bunazi wilaya ya Misenye.
Baadhi ya wagombea wa udiwani wakiwa tayari kujinadi kwenye mkutano wa kampenii za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa maarufu kama Chakaza,Bunazi wilaya ya Misenye.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akimtambulisha mgombea wa ubunge jimbo la Nkenge
Balozi Dk. Deodorus Kamara kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa maarufu kama Chakaza.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bunazi wilaya ya Misenye ambapo aliwaahidi kuondoa kodi zote zisizokuwa na maana kwa mkulima wa kahawa.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihtubia wakazi wa Misenye na kuwaahidi kuwa ataondoa vikwazo kwa wafanya biashara ili waweze kufanya biashara vizuri.
Wakazi wa Bunazi wakiwa wengi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo pia ulihutubiwa na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Sheikh wa Wilaya ya Misenye Alhaj Abdul Chagulani akimuombea dua njema Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipokea dua ya sheikh mkuu wa wilaya ya Misenye Alhaj Abdul Chagulani.
Wakazi wa Karagwe wakimsubiri Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kuwahutubia kwenye viwanja vya Changarawe Kayanga wilayani Karagwe.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Karagwe ambapo aliwaahidi kutekeleza anayo ahidi ikiwemo ukamilishwaji wa ujenzi wa barabra kwa kiwango cha Lami.

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga push up mbele ya maelfu ya wakazi wa Karagwe kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Changarawe,Kayanga.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Kyerwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Rumanyika kata ya Nkwenda wilaya ya Kyerwa.

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kyerwa kwenye mkutano wa kuomba kura kwa wananchi.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Kyerwa Ndugu Innocent Balikwate kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Rumanyika.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Wakazi wa Benako wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati akielekea kwenye mkutano wa kampeni Ngara.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Alhaj Abdallah Majura Bulembo akihutubia wakazi wa Ngara kwenye uwanja wa posta ya zamani.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ngara mjini
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubiawakazi wa Ngara ambapo aliwaahidi wakazi hao kuwa atashughulikia kupunguza kodi zinazo mkandamiza mkulima.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimndadi mgombea wa ubunge jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashaza .



Mbunge Mteule anayewakilizsha Wazazi Oliva Semguruka akihutubia kwenye mkutano wa Kampeni za CCM kulia ni Halima Bulembo Mbunge mteule kupitia vijana
Mbunge Mteule anayewakilizsha Wazazi Oliva Semguruka akihutubia wakazi wa Ngara ambapo aliwaambia wakina mama kushikana na kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo na kuitunza amani iliyopo.
Mbunge mteule atakayewakilisha vijana Ndugu Halima Bulembo akihutubia wakazi wa Ngara kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea ubunge wa jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashazaakihutubia wakazi wa Ngara mjini wakati wa mkutano za CCM za kumnadi Dk.John Pombe Magufuli
 
Hivi Magufuli kupiga push up nne jukwaani kuna tija kwa wapiga kura?
 
Kapige push ups ukweni kama hujanyimwa mke.. watajiuliza zimetimia kweli?
 
Afya kwanza Urais baadae,hata Lowasa nilimuona akionyesha makeke yake kwa kukimbilia helkopta iliyopo kwa ajili yake
 
Afya ni muhimu sana katika uongozi, ameonyesha jinsi alivomkakamavu.
 

Attachments

  • FB_IMG_1442994096615.jpg
    FB_IMG_1442994096615.jpg
    55.4 KB · Views: 230
Kapige push ups ukweni kama hujanyimwa mke.. watajiuliza zimetimia kweli?

Bila shaka hata sisi wapiga kura tunatakiwa kuwa na shaka ya utimilifu wa akili ya mgombea huyu! Rais wa nchi ndio afanye hayo hadharani???!!!
 
CCM hawana product ya kuwauzia wananchi... Hata Magufuli akipewa nafasi anadanganya mchana kweupe eti ataigeuza Tanzania iwe ya Viwanda wakati sera na Ilani ya CCM ni ubinafsishaji wa viwanda na mashirika ya umma ..
 
Back
Top Bottom