Dk 55, kosa hapa Dante anachichanganya Simba wanaingia hatariiiiiii Dante anaokoa
Dk 54, kona ya Kichuya, hatari tena, Dida anaokoa hapa
Dk 53, Kichuya anaingia vizuri hapa, hatariiii lakini Dante anamuwahi na kutoa nje, kona
Dk 53, Juma Abdul anacheza faulo hapa lakini mwamuzi anamsamehe, akimuonya kwa maneno. Kumbuka kadi ya njano
Dk 52 kona nyingine inachongwa na Kotei lakini Yanga wako makini wanaokoa
Dk 51, Simba wanafanya shambulizi kali hapa, krosi ya Kichuya Yondani anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya, Dida anaokoa tena na kuwa kona tena
Dk 49, Simba wanagongeana vizuri na Mo Ibrahim anaachia mkwaju na Dida anadaka vizuri
Dk 47 krosi nzuri ya Mwinyi lakini Mwanjale anauwahi, kona. Inachongwa na Niyonzima , wanaokoa
Dk 46, Yanga wanacheza vizuri, lakini Tambwe anashindwa kupiga krosi kutokana na kasi ya mpira