Yaliyojiri Uwanja wa Taifa: Taifa Stars 2 - 1 Equatorial Guinea

Kaseja amemuaibisha kocha wake Ndairagije! Yaani mtu anafunga kutoka katikati ya uwanja! Kwa hali hii mashabiki wa Simba wana haki ya kumlilia golikipa wao Aishi Manula, ingawa na yeye amekua akitunguliwa magoli ya aina ile ile.
 
Tatizo wabongo wengi ushabiki maandazi mtu anataka kipa wake wa yanga au simba ndio achaguliwe timu ya taifa
 
Hii mechi tatizo siyo kipa,,,Angalia timu inachezaje,,,wachezaji washapanic wasipotulia na hao jamaa wanavyocheza total football yatakuwa mengine hapa
Kwa takwimu mpaka sasa katika Ligi Kuu, Manula anastahili kuwepo kwenye kikosi cha Taifa.
 
Hii mechi tatizo siyo kipa,,,Angalia timu inachezaje,,,wachezaji washapanic wasipotulia na hao jamaa wanavyocheza total football yatakuwa mengine hapa
Sina maana kuwa kipa ni Tatizo. Nilinukuu kauli ya mmoja wetu hapo juu.

Kikubwa ni wachezaji wetu kutokujua kipi kinahitajika na kwa wakati gani.

Mara nyingi wanashindwa kuimaliza mechi mapema. Japokuwa kwa hapa wakijitahidi tunaweza kutoka na kitu.
 
Natamani sana kumuona na yule golikipa wa Gor Mahia, David Kisu Mapigano. Kuwa golikipa namba moja kwa timu kama Gor Mahia siyo kazi rahisi! Huku akimuweka nje mzawa!

Kiukweli Kaseja umri nao unamtesa, ingawa inapofikia hatua ya penati, hakika mara zote hugeuka kuwa shujaa. Hili ni goli la pili pamoja ma lile dhidi ya mechi na Sudan anaonesha udhaifu kwenye udakaji.

All in all, kila la heri Taifa Stars. Ushindi ni muhimu. Tukishindwa kabisa, tupate tu hata sare. Ila siyo kufungwa. Maana tutapoteana.
 
Aishi Manula, ingawa na yeye amekua akitunguliwa magoli ya aina ile ile.
Ya aina ile ile maana yake ni nini? Watu kadhaa nimekuwa nikiwasikia wakilizungumza hili, lakini nikiwauliza maana huwa hawajibu. Inaonekana kuna kukaririshana sentensi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…