Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Duh, Mkuu nadhani udereva na ukonda waliacha kabisa
 
Luteni Kilawe,kiongozi wa Kwata ya Kimyakimya,nitakutafuta!
 
We mtu sio!!
 
Jamani kama heading inavyosema, leo kwenye uwanja wa Uhuru kuna maonyesho yanafanyika, yanajumuisha gwaride la majeshi jwtz, polisi na magereza.

Niende kwenye kiini, Mimi leo katika maonyesho haya nimevutiwa sana na kikundi cha guard ya kimyakimya( silent guard)

Sio siri wamefanya vizuri sana hasa katika mambo yafuatayo:
1. Mageuko(turning), Mara zote wamegeuka kikakamavu sana na wanakata upepo balaaa
2. Jinsi ya kukondamachi( yaani msitari mmoja unaingia kwenye mistari mingine ili kupanga guard kuendana na urefu yaani watu wa mbele wabakie walewale na right marker abakie yuleyule, safi sanaaaa

3. Namna ya kubadilishana silaha, wamefanya kitendo hiki kwa uharaka na ukakamavu na bila kukosea(accuracy)

4.kwenye kunyoosha mistari wamefanya wonders, hongeraaaaa
5. Kiongozi wao Lt. Kilawe yule Dada mwenye kitala ameonesha ukakamavu safi sanaaaa

Hongera zao silent guard ya jwtz (infantry soldiers)
Najua kuna mengine umeyaona mwana jf karibu uyaweke hapa
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeniii
 
Nawaza kimya kimya pia....ina maana huwa wanapata mafunzo kimy kimya [emoji40]
 
Lipumba ndani ya kwata ya kimya kimya
 
Mkuu,usisahau kupita na pale Makongo,even though,afande Miraji is no more,umwage hata mvinyo pale nje kwa heshima yake!
 
Hivi mkitumia muda mwingi kuangalia huyu kaja yule hajaja itasaidia nini. Mi nilizani kama watalaam as great thinkers tungekuwa tunajadili issues na sio nani kaja nani hajaja. Mfano tukajadili maudhui ya sherehe ya mwaka huu. Tunatarajia nini kama taifa na mengineyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…