Achana na wale wa kutumia silaha lakini Komando walioonyesha sarakasi wamedhalilisha kabisa tasnia hiyo. Kilichoonyeshwa kama mbinu za kupigana au karate za makomando ni mambo ya mitaani na mtu yeyote anaweza kufanya huku mitaani wako wengi tu wanafanya hayo. Niko disappointed kwa sababu tulitegemea watu walioko kambini kulinda nchi wanashindwa ku exceed mbinu za waonyesha sarakasi wa mitaani na walioko kwenye madojo. Nashauri makomandoo wawatafute wachina au wajapani wawape training ambayo ina viwango na siyo kufanya uhuni mbele ya dunia. Rais asiruhusu hawa jamaa kuonyesha ujinga kama hawajajipanga kwani ina expose udhaifu wa jeshi letu kwa maadui. Kilichoonyeshwa mbele ya dunia kinaonyesha hatuko serious. Kenya wana maonyesho kama haya lakini ukiangalia una hold your beath kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kwa mtazamo wangu kama hiki ndicho walichojiandaa nacho kuonyesha watanzania basi hii group inatakiwa iwe overhauled ili kurejesha heshima ya makomando na kuwapa watanzania matumaini kwa jeshi lao