Inasadikika ipo Bariadi. Mh. Chenge anaweza akatuwekea kumbukumbu vizuri.Ndiyo wapi Mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inasadikika ipo Bariadi. Mh. Chenge anaweza akatuwekea kumbukumbu vizuri.Ndiyo wapi Mkuu?
Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.
Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa
Rais wa Zanzibar,Dr. Ally Mohamed Shein,ndiye anayewasili uwanjani.
Jecha S. Jecha naye yupo uwanjani
Sasa anawasili Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan
Kumekucha sasa,Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,anawasili sasa uwanjani tayari kuanza kwa maadhimisho haya.
Rais Magufuli yuko kwenye gari maalum kuzunguka uwanjani na kuwasalimu wananchi. Katika gari hilo,yupo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais sasa amepanda jukwaa maalum kupokea salamu toka kwa jeshi. Gwaride liko chini ya Kamanda Luteni Kanali Makanya Eras. Wimbo wa Taifa na mizinga 21 vinarindima.
Rais sasa anakagua gwaride
Ukaguzi umemalizika. Rais anarejea jukwaa kuu. Vikundi vya jeshi vitapita mbele yake kwa heshima,kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka
Sasa vikosi vinapita mbele ya Rais kwa kutoa heshima
Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.
Sasa Makomando wanaonyesha uzoefu wao
Komando wanakunja nondo kwa mikono
Komando wanapigana kwa fito hadi kuvunjika
Sasa ni zoezi la kuvuja tofali kifuani na kichwani mwa komando
Komando analalia misumari mgongo wazi
Komando wanasukuma gari lililoharibika hadi kutembea
Kwata ya kimyakimya
Sasa vinafuta vikundi vitatu vya ngoma za asili
Sasa rais Magufuli anahutubia umati uliofika katika viwanja vya uhuru.
Rais anaanza kwa kutoa salamu huku itifaki ikiwa imezingatiwa.
Rais Magufuli: Niliamua kusitisha sherehe za mwaka jana kwa sababu kuu mbili; kwanza Sherehe za mwaka jana zingefanyika kabla sijaapishwa, pili sherehe zingegharimu shiling bilioni 4. Nilielekeza hizo bilioni 4 zitumike kujenga barabara.
Rais Magufuli: Sherehe za miaka 55 ya uhuru nimeamua zifanyike hapa kwani zitakuwa ndo sherehe za mwisho kufanyika Dar es salaam, Sherehe nyingine zote zitafanyika Makao makuu Dodoma.
Rais anawapongeza wapigania uhuru na marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wote wastaafu.
Rais Magufuli: Ndugu zangu watanzania katika bajeti ya mwaka 2016/17 tumetenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tumeanza miradi mbalimbali ikiwemo kinyerezi I,II na III.
Mpaka sasa tumeshanunua ndege sita kwa ajili ya kujenga uchumi na utalii wa nchi yetu.
Bajeti ya afya imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi bilioni 131.
Makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 850 mpaka wastani wa trilioni 1.2
Rais Magufuli: Tutaendelea kuchukua hatua kali ktk masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa. Tumepanga kuondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge
Ombi langu kwenu, tuendelee kudumisha amani yetu. Tudumishe pia umoja na mshikamano wetu tusisahau kuulinda muungano wetu. watanznia pia tuendelee kufanya kazi tuzingatia kauli ya hapa kazi Tuu.
Rais Magufuli: Tutajihidi kutatua kero zenu kwa uwezo wetu wote bila kubagua mtu kwa dini yake, kabila lake au chama chake.
Asanteni sana na Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru

Angekwenda pale jamaa angeumbuka oohJamani mbona kipenzi chetu JK hayupo?
Mwenye sifa ana sifa tu hata umuingizie ufahamu akilini mwake hatoacha Tabia yake ! Huyu bwana wetu sipata picha livyokua shule ya msingi na kihele hele hiki sijui alikuaje LohNi kosa kubwa sana kwani anaingilia Kazi / Majukumu ya Watu. Kwanini huyu Mtu hapewi mafunzo ya kumbadili kutoka kuwa Mtu wa kawaida kama alivyokuwa, Mkuu wa Wilaya na Ukuu wa Mkoa alionao sasa hasa wa Kiitifaki? Anaboa bhana!
Mkwere bado anapiga ruti angani, hayupo!JK vipi au hasira za bibie bado zinawaka! Simuoni hapa.
Tuwaachie wana usalama mkuuNadhani kulinda watu waliokaa sehemu moja tu wametulia sio sawa na wanao safiri kwenye chombo kimoja
Hiyo ni zuri sana inapunguza gharama na kuimarisha mahusiano.Ni kwa usalama tu. Hata viongozi wa mihimili mingine ya Dola kila mmoja wao huwa na gari lake na ulinzi. Leo kwa mara ya kwanza Mawaziri na Manaibu wao pamoja na Makatibu wakuu wamepanda mabus madogo maalumu kwa pamoja
Mkuu kuna mzee mmoja alikuwa anachangia kwenye kipindi cha malumbano ya hoja-ITV, alisema hivi, "watz ni watu wa ajabu sana, umeme ukikatika wanashangilia, ukiwaka wanashangilia, sasa sijui tunataka giza au mwanga maana vyote tunavishangilia".., wale wale wananchi ambao mwaka jana (2015) mwezi kama huu (desemba) walishangilia kweli sherehe za uhuru zilopohairishwa kwa kisingizio cha 'kubana matumizi' na fedha zile kuelekezwa kwenye matumizi mengine., tukielezwa tufanye usafi nchi nzima..,
..., mwaka huu (2016) ndiyo wananchi hao-hao leo wanasherekea na kushangilia tena wakati maadhimisho yale ambayo mwaka jana yalikataliwa kwa kisingizio cha kubana matumizi, leo wakati yanafanyika.., tena wananchi wale-wale wakishangilia kwa vifijo na nderemo wakisema Hapa Kazi Tu..,
[emoji1485] wananchi hawa siyo watu wa mchezo-Mchezo, wanakwenda na namna unavyovuma.
[emoji1485] wananchi hawa wanacheza kila wimbo, hata wimbo reggae wao wanakata Viuno.
[emoji1485] wananchi hawa, ni rasmi wamekuwa wepesi kusahau, sasa wameruhusu watawala waone udhaifu wao, na bado!
[emoji1485] ni rahisi sana Kuwaongoza watu wa aina hii.., leo wakisikia hivi OYEE, kesho wakisikia hivi OYEE!
[emoji1485]Wale wananchi ambao mwaka jana walisema ahsante kwa kuondoa sherehe za maadhimisho haya.., leo ndiyo wameingia katika uwanja wa uhuru (shamba la Bibi) tangu alfajiri.., ajabu sana!
[emoji1485] hata mwaka mmoja haujapita, tumesahau kabisa tuliambiwa nini 2015 (Desemba) , na sasa 2016 (Desemba) tunashangilia kile ambacho tulisema kwa pamoja ni gharama na hasara kuadhimisha sherehe hizi.., WADANGANYIKA!
T U S A M E H E,
Hata mm hili swala nilikua najiuliza mda mrefyHivi najiuliza Rais, Makumu wake na PM hawawezi kupanda gari moja kwenda uwanjani? Tuna bana matumizi pamoja na kupunguza foleni.
Pamoja sanaHata mm hili swala nilikua najiuliza mda mrefy
Hawa ndio wamebadilisha sura ya mchezo maana duuuuh...View attachment 444271
Gwaride la kimya kimya [HASHTAG]#AfandeKiwi[/HASHTAG]
Naona mtaita majina yote, huko zanzibar mulikuwa munaita Tanzania visiwani, mara ikawa Tanzania zanzibarBaada ya Muungano,Tanganyika ikawa Tanzania Bara.
Nakupenda sana ndugu yangu ndio maana sitaki umpoteze huyo shemeji eti kwa mkwara wa tofali soft kuvunjiwa kifuani au kutishiwa misumari ambayo huna uhakika kama siyo ya bati na imegeuzwa.Mkuu bado hujanishawishi na naona kama vile unataka nikafe mubashara. Haya sawa yale matofali ni ya magumashi je na ile misumari 200 nayo ni feki? Mkuu hivi unanipenda na kunitakia mema kweli kwa aina yako hii ya ushawishi kwangu?