UTARATIBU KWA SIKU YA LEO - UWANJA WA TAIFA:
Ni Magari maalumu tuu kuingia uwanja wa Taifa.
Magari yenye shughuli maalumu tu ndiyo yanayoruhusiwa kuingia uwanja wakati wa mechi ya leo kati ya Simba na Yanga - kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi inaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu inaruhusiwa kuingia na magari matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya viongozi.
Ukaguzi wa kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huu si wa kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama.
Vilevile watu hawaruhusiwi kuingia uwanjani na mifuko ya aina yoyote ikiwemo mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari wanaotumia mabegi hayo kwa ajili ya kubebea kamera zao.
Pia hakuna wafanyabishara watakaoruhusiwa kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka uwanja.
Kwa washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa kero kwa wenzao wakiwemo walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale wenye silaha kama bastola ambapo wakikamatwa watafikishwa polisi na baadaye kufunguliwa mashtaka kortini.
Barabara ya Uwanja wa Taifa imefungwa kuanzia saa 2 asubuhi upande wa Chang¡¯ombe.
Washabiki walitakiwa kununua tiketi zao mapema kuanzia jana (Jumamosi) ambapo ziliaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia saa 4 asubuhi.
Vituo hivyo ni:
Mgahawa wa City Sports Lounge,
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa,
Sokoni Kariakoo,
Mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora,
Oilcom Ubungo,
Kituo cha Mafuta Buguruni,
Dar Live Mbagala,
Uwanja wa Uhuru,
Mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na
BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.., nk.