Yaliyojiri Yanga Vs FC Platinum

Yaliyojiri Yanga Vs FC Platinum

Mzee wa sababu kazini.....
Kipindi kile nilikueleza sababu za kusuasua ni kwamba tulikuwa tunauguza na siku na stendi ndo ulikuwa msiba lakini baada ya kuanua matanga sahivi kila tunayekutana naye ni vipigo tu. Shahidi wewe mwenyewe.

Na kuhusu Minziro hilo linafahamika, kuna msimu mmoja alikuwa anafundisha timu ya Prisons aliwapa maelekezo kabisa mabeki wake kwamba baadhi ya wachezaji wa Yanga wasiwakabe kwa nguvu sana na matokeo yake timu ilipoteza na Minziro msimu uliofuata akapata ajira Yanga, kwa hiyo sioni ni kwa nini sasa ashindwe kuisaidia timu yake anayoipenda kupata ushindi ukizingatia mbio za kugombania ubingwa zilivyopamba moto.
 
Wamekula ban wapi?
kimewapa ambacho hawakukitegemea leo.
Hahahaaa, ujue wiki ilopita walitawala jukwaa ila leo ni zamu yetu....
Kutesa kwa zamu ila sisi ndio zaidi.
 
Mkuu mimi mpaka niliumwa ile jumapili na wiki yote hii nimeitia hasara serikali kwa kufanya kazi chini ya kiwango.
 
Kipindi kile nilikueleza sababu za kusuasua ni kwamba tulikuwa tunauguza na siku na stendi ndo ulikuwa msiba lakini baada ya kuanua matanga sahivi kila tunayekutana naye ni vipigo tu. Shahidi wewe mwenyewe.

Na kuhusu Minziro hilo linafahamika, kuna msimu mmoja alikuwa anafundisha timu ya Prisons aliwapa maelekezo kabisa mabeki wake kwamba baadhi ya wachezaji wa Yanga wasiwakabe kwa nguvu sana na matokeo yake timu ilipoteza na Minziro msimu uliofuata akapata ajira Yanga, kwa hiyo sioni ni kwa nini sasa ashindwe kuisaidia timu yake anayoipenda kupata ushindi ukizingatia mbio za kugombania ubingwa zilivyopamba moto.
Sababu ya kwanza ulibahatisha tu.
Ila ya pili ni maneno ya vijiweni tu siwezi kuyaamini.
Ila unaonekana mzee wa tantalila sana wewe...lol
 
Mkuu mimi mpaka niliumwa ile jumapili na wiki yote hii nimeitia hasara serikali kwa kufanya kazi chini ya kiwango.
Dah, pole sana mkuu.Jobless kama mimi tuna raha sana sometimes. ...
Ujue uchungu wa kufungwa ni pale unapokatiza mitaa na maofisini huko kama kuna wapinzani utaiona dunia chungu, ila sisi.....aaaah tunaugulia maumivu ndani kwa ndani tu.
Ila JF niliiona chungu sana!
 
Dah, mkuu nawe ulipotea sana.
Huyo jamaa bora usimtaje tu maana.....

Ni kweli Mkuu nilikuwa safarini huko Katavi na Rukwa katika maeneo ambayo yana shida ya umeme. Kwa sasa tuko pamoja sana Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Sababu ya kwanza ulibahatisha tu.
Ila ya pili ni maneno ya vijiweni tu siwezi kuyaamini.
Ila unaonekana mzee wa tantalila sana wewe...lol
Tantalila ndo nini?

Kama unaona hiyo ya Minziro ni maneno ya vijiweni ngoja nikupe na hii:

Kuna msimu mmoja sikumbuki ni msimu upi, Simba na Yanga zilikuwa na pointi sawa na zilikuwa zimebakiza mechi moja kwa kila timu, Yanga ilimaliza na Toto na Simba ilimaliza nadhani ni maji maji, kuna beki wa Toto baada ya kuona Yanga hawafungi badala ya kuzuia akawa anapisha mpira au ana uruka kama ni mpira wa chini, na kipindi kile golikipa Wiliam Mweta baada ya kuwazuia Yanga kipindi cha Kwanza kocha akamtoa na kipindi cha pili akamwingiza kipa mwingine ambaye ndani ya dakika 45 alifungwa mabao ya kutosha na hatimaye Yanga kuwa mabingwa kwa wingi wa tofauti ya magoli.
 
Hiyo mechi naikumbuka sana, bila shaka ulikua msimu wa 2010-2011.Hii mechi ilikua ya mwisho na nilifurahi sana.Ila kuna mchezaji wenu mmoja alipaisha penalty (simkumbuki ni nani) na kama angeipata nyie ndio mngekua mabingwa.Bado siyaafiki maneno yako.
 
Tantalila ndo nini?

Kama unaona hiyo ya Minziro ni maneno ya vijiweni ngoja nikupe na hii:

Kuna msimu mmoja sikumbuki ni msimu upi, Simba na Yanga zilikuwa na pointi sawa na zilikuwa zimebakiza mechi moja kwa kila timu, Yanga ilimaliza na Toto na Simba ilimaliza nadhani ni maji maji, kuna beki wa Toto baada ya kuona Yanga hawafungi badala ya kuzuia akawa anapisha mpira au ana uruka kama ni mpira wa chini, na kipindi kile golikipa Wiliam Mweta baada ya kuwazuia Yanga kipindi cha Kwanza kocha akamtoa na kipindi cha pili akamwingiza kipa mwingine ambaye ndani ya dakika 45 alifungwa mabao ya kutosha na hatimaye Yanga kuwa mabingwa kwa wingi wa tofauti ya magoli.

Simba ilicheza na Ruvu JKT Dar, kipa wa Ruvu alipigwa red card, Pius Kisambare alivaa gloves na kudaka michomo yote ya Simba, refa angewasaidia vipi zaidi ya hapo? Yanga ilirudi kipindi cha pili ikiwa na nguvu mpya, Toto hawakuweza kuhimili huko jijini Mwanza.

Kwa msimu huu, kiufundi Simba bado haijatulia, ushindi dhidi ya Yanga na hata Mtibwa ni kama vile ni God given, magoli yamefungwa na mtu mmoja tena mita kibao toka langoni. Ni dalili kuwa safu ya ushambuliaji ni butu, si ajabu mtarudi kwenye draw zenu mlizozizoea katika mechi zijazo.
 
Back
Top Bottom