Yaliyojiri Yanga Vs FC Platinum

Wadau - inshallah tukivuta kwa hao Platnum, ni timu gani inafuata?
 
Hahahaaa, ujue wiki ilopita walitawala jukwaa ila leo ni zamu yetu....
Kutesa kwa zamu ila sisi ndio zaidi.

na kweli leo ni zamu yetu watuwache maana siku ile nifah tulibaki peke yetu tu tunagugumia maumivu ya kufungwa na mikia
 
Last edited by a moderator:
na kweli leo ni zamu yetu watuwache maana siku ile nifah tulibaki peke yetu tu tunagugumia maumivu ya kufungwa na mikia
Hahahaaa, mikia noma wakibahatisha!
 
Last edited by a moderator:
Timu imefunga magoli zaidi ya ishirini huwezi kusema ina washambuliaji butu, labda useme hatuna namba tisa tegemeo kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Gabriel, Nteze John Lungu,Musa Mgosi, Felix Sunzu, Amis Tambwe, Selemani Ndikumana au Athumani Machupa.

Lakini niamini kombinesheni ya Okwi, Singano na Ibrahim mwalimu akiiamini inaweza kufanya vizuri sana. Bado hata Maguri na Danny Serunkuma nao sio wa kupuuzwa.

Halafu yale magoli ya Okwi kama ni mfutiliaji mzuri sio ya kubahatisha; Aliwafunga Yanga goli kama hilo mwaka 2012, aliwafunga Shandy , aliwafunga Entente du Setif, aliwafunga Azam, amewafunga Yanga tena, kawafunga Mtibwa ya aina hiyo. Sio bahati 100%, yanafanyiwa mazoezi kwa hiyo unapopiga siku zingine unakosa siku zingine unapata na ndo maana kafunga magoli mengi tu nje ya 18.
 
yaan kwa matokeo haya kwa upande wangu ni bora sana kuliko tungemfunga mtani.maana hapa tunapata heshima africa nzima.pia huku tutapata zaid ya ml200............
 
yaan kwa matokeo haya kwa upande wangu ni bora sana kuliko tungemfunga mtani.maana hapa tunapata heshima africa nzima.pia huku tutapata zaid ya ml200............

Ni kweli lakini suala la kuwafunga Simba nalo ni mhimu sana
 
Simba wametoa pongezi kwa watani wao wa jadi Yanga kutokana na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.



Yanga imeshinda kwa mabao hayo na kujiweka katika nafasi nzuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema kwa niaba ya Rais wa Simba, Evans Aveva wanaipongeza Yanga.


"Yanga ni wawakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa. Hakika wanastahili pongezi kutokana na kufanya vema.


"Inapofikia katika suala la nchi, si vibaya kuwapongeza. Tukirudi kwenye ligi basi upinzani unaendelea.


"Ndiyo maana leo tulikuwa uwanjani kushuhudia Yanga wakipambana na walifanya vema kwa kweli," alisema Tully.
 

Umelala na viatu leo
 

Huyo wa kumsamehe tu maana anaongea utadhani mtu asiyefuatilia mpira wa duniani, magoli kama ya Okwi yamefungwa na mastaa wengi tu wa dunia hii mf. David Beckam, C. Ronaldo, Rooney nk
 
Ningechagua hii
Bado lakini nina hamu ya kuwaona SIMBA wakibutuliwa kipigo kama cha leo

Simba huwa inapiga 5 kwa 0, muulizeni Manji kama wengine mmesahau. Kumfunga shoga yako Mdako hakumaanishi unaweza kumfunga na mumeo Simba.
 

Mkuu unachoongea ni kweli kabsa hatuna namba tisa tegemeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…