Yaliyojiri: Yanga vs Mbao FC

Yaliyojiri: Yanga vs Mbao FC

Danny greeny

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
3,856
Reaction score
1,648

FULL TIME | Yanga 3 - 0 Mbao FC

49' Vicent Boussou (Yanga)
55' Mbuyu Twite (Yanga)
75' Amisi Tambwe (Yanga)

KADI Dk 88, Kipa Dida analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira kwa makusudi

Dk 87 sasa, Mbao wanaonekana kuamka na kutaka kupata bao angalau moja, lakini bado Yanga wako vizuri zaidi

Dk 84 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo huku Mbao kama wamekata tamaa ingawa mara kadhaa wanajitahidi kushambulia

Dk 80 Ndikumana anapiga mkwaju wa adhabu hapa, lakini Dida anadaka kwa ulaini kabisa

Dk 78 sasa, kwa hali ilivyo, Mbao wanaonekana kupoteana kabisa, Yanga wanapiga pasi wanavyotaka. Lazima Mbao FC waimarishe uchezaji wao kwenye kiungo, la sivyo Yanga wanaweza kushindilia bao la nne

GOOOOOOOOO Dk 75, Tambwe anaifungia Yanga bao safi kabisa akiunganisha pasi safi ya Simon Msuva

DK 74, Donald Ngoma anaruka na kupiga kichwa mpira wa kurusha wa Twite, lakini safari hii kipa yuko makini

Dk 71, Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na Donald Ngoma

KADI Dk 70 Ndikumana analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Haji Mwinyi

SUB Dk 64 Yanga wanamtoa Hassan Kessy na nafasi yake inachukulwia na Thabani Kamusoko, maana yake Mbuyu Twite anakwenda pembeni kulia

Dk 62, Tambwe anaachia kombora hapa linagonga mwamba na kutoka nje, ilikuwa ni al manusura

SUB Dk 56, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke

GOOOOOOOOOO Dk 55, mpira wa kurusha wa Twite unakwenda moja kwa moja kwa moja wavuni kipa kuupangulia ndani

SUB Dk 54 Venance Ludovic anaingia Damas Msiba kwa upande wa Mbao FC

Dk 50, Yanga wanazidi kusukuma mashambulizi, Niyonzima anaangushwa hapa, anatibiwa

GOOOOOOOOO Dk 49, Bossou anafunga bao lakini mpira unagusa mkono wake kabla ya kuingia wavuni. Ilikuwa ni baada ya kuunganisha krosi ya Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu

Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi wakishambulia zaidi na wanaonekana wanataka bao la mapema

Half Time | Yanga 0 - Mbao 0
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA

Dk 44, Tambwe anapokea pasi nzuri ya Niyonzima na kupiga vizuri lakini mpira unatoka kiduchu kabisa
SUB Dk 42, Salum Sued anakwenda nje kwa upande wa Mbao FC, nafasi yake

Dk 37, Bado hakuna hata shambulizi kubwa. Inaonekana wazi Yanga wanahitaji mtu wa kulazimisha kama Ngoma vile. Chirwa na Tambwe wanaonekana 'kutoiva' pamoja

Dk 30, bado inaonekana hakuna shambulizi kali zaid ya kona.

Dk 24, Mbao wanapata kona baada ya Bossou kulazimika kutoa nje mpira, inachongwa lakini Dida anadaka vizuri kabisa

Dk 18, Yanga inapata kona ya kwanza baada ya beki Mbao kumuwahi Msuva na kuutoa. Inachongwa lakini haina manufaa

Dk 14, hakuna shambulizi kali kwa upande wowote, inaonekana kila upande bado haujajipanga katika umaliziaji

Dk 8, Chirwa anapiga shuti kimo cha nyoka lakini linatoka sentimeta chache kabisa nje ya lango la Mbao

Dk 6, krosi safi ya Kaseke, Msuva anaunganisha vizuri kabisa lakini anashindwa kulenga lango. Yanga imetumia takribani dakika nne ikigongena vizuri kabisa

Dk 1 mpira unaanza taratibuuu kila upande unaonekana ukiwa makini kwa kutaka kufunga na kuepuka kufungwa

Kikosi cha Yanga Vs Mbao FC leo
1. Deo Munishi
2. Ramadhan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vincent
5. Vincent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Amis Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Deus Kaseke

Akiba;
Beno Kakolanya
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Thabani Kamusoko
Donald Ngoma
Matheo Anthony
Juma Mahadhi

Credit: Saleh Jembe Blog
 
Leo tunacheza mpira utafikiri tupo ligi daraja la pili.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Watanyooka tu hao Mbao FC aka Mnyama nduguye...
Mkuu kwa mpira wanaocheza hawa jamaa ni kama vile wanataka kujustify kuwa Lwandamina alikuwa ni Bora kuliko Pluijm.

Mpira hauna kasi wala umakini. Hata ile striking force inayopiga watu goli nne leo haionekani.
 
mleta uzi huu unapo weka kikosi cha timu moja tu maana yake nn??punguza unazi unapoamua kuripoti hv vitu
 
Second half itabidi tukaze sana. Kuw tofauti ya point nane au saba na Simba, ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom