Wale jamaa walinishangaza Sana
Japo ss tunataka Amani itawale sasa Ccm ikidondoka Chama gani kilichojiandaa kuchukua nchi
Kazi yangu kusoma comments na mijadala nikiwa hapa msola ni mm mtoto wa kitanzania !
Tujaribu na chama pinzani, hasa ndiyo nia ya raia hivi sasa.
Wakitawala wataendesha vizuri sababu kama faulo nyingi wasizopenda raia wa Tz, wanazijua, na wao ndo'wanaozipigia kelele kwamba zitanzuliwe.
Baada ya miaka mitano ya kikatiba na wao wakileta ushenzi tunaridhia na kukiweka chama kingine hadi tutakapopata utulivu tunaoutaka waTz.
Kwanini tusijifunze Kenya ama Zambia, kwani demokrasia yao imewaletea madhara, kuwaondoa vyama kongwe vilivyokuwa vimejimilikisha utawala kama ilivyo Ccm?
Hakuna chama chenye hakimiliki ya kutawala milele.
Chama chochote chaweza kushika Dola mradi kipate ridhaa ya raia, siyo ridhaa kwa njia ya wizi wa kura kama wanavyofanya Ccm no.
Ccm wangelikuwa wanajali na kusikiliza kero za raia ambao ndiyo waajili wa Serikali hii, hakuna raia ambaye angeipinga Serikali ama Ccm kama inavyotokea hivi sasa.
Je kwa mfano Magufuli alivyotawala na kwenda na kero za wanyonge, ulionaje alivyokubalika na kukonga nyoyo za watu ?
Mpaka ukapatikana msemo wa: ... "chagua mtu usichague Chama".
Kwanini msingeenda na kasi yake?
Haya wewe msisiem tuambie, hauoni faulo zote zifanywazo na watawala wa Serikali yako pendwa katika awamu hii, ambazo ni rahisi sana kuzitanzua ili kuweza kutembea na imani na mioyo ya wananchi?
Usiniulize faulo gani, we'mwenyewe unazijua.
Kwanini watawala wameziba pamba masikioni?
Sababu ipo na dalili za dhahiri zimeshaonekana!
Wahenga walisema: "sikio la kufa halisikiagi dawa"