Yaliyokuwa yakiogopwa na watangulizi wake CCM kuwafia mikononi yanaenda kutimia kwake?

Yaliyokuwa yakiogopwa na watangulizi wake CCM kuwafia mikononi yanaenda kutimia kwake?

Tujaribu na chama pinzani, hasa ndiyo nia ya raia hivi sasa.

Wakitawala wataendesha vizuri sababu kama faulo nyingi wasizopenda raia wa Tz, wanazijua, na wao ndo'wanaozipigia kelele kwamba zitanzuliwe.

Baada ya miaka mitano ya kikatiba na wao wakileta ushenzi tunaridhia na kukiweka chama kingine hadi tutakapopata utulivu tunaoutaka waTz.

Kwanini tusijifunze Kenya ama Zambia, kwani demokrasia yao imewaletea madhara, kuwaondoa vyama kongwe vilivyokuwa vimejimilikisha utawala kama ilivyo Ccm?

Hakuna chama chenye hakimiliki ya kutawala milele.

Chama chochote chaweza kushika Dola mradi kipate ridhaa ya raia, siyo ridhaa kwa njia ya wizi wa kura kama wanavyofanya Ccm no.

Ccm wangelikuwa wanajali na kusikiliza kero za raia ambao ndiyo waajili wa Serikali hii, hakuna raia ambaye angeipinga Serikali ama Ccm kama inavyotokea hivi sasa.

Je kwa mfano Magufuli alivyotawala na kwenda na kero za wanyonge, ulionaje alivyokubalika na kukonga nyoyo za watu ?

Mpaka ukapatikana msemo wa: ... "chagua mtu usichague Chama".

Kwanini msingeenda na kasi yake?

Haya wewe msisiem tuambie, hauoni faulo zote zifanywazo na watawala wa Serikali yako pendwa katika awamu hii, ambazo ni rahisi sana kuzitanzua ili kuweza kutembea na imani na mioyo ya wananchi?

Usiniulize faulo gani, we'mwenyewe unazijua.

Kwanini watawala wameziba pamba masikioni?

Sababu ipo na dalili za dhahiri zimeshaonekana!

Wahenga walisema: "sikio la kufa halisikiagi dawa"

Magufuli alikuwa Kiongozi wa hovyo kuliko wote katika nchi hii.

Narudia wa hovyo sanaa.
 
Yaliyokuwa yakiogopwa na watangulizi wake ya CCM KUWAFIA MIKONONI yanaenda kutimia kwake?

Tumeona ongezeko la urudishaji wa kadi maeneo mbalimbali Mtwara, Tanga na kule kwa Maasai Ngorongoro.

Awamu hii itakuwa ni anguko kwa CCM? Ataendelea kuongoza?
JamiiForums-2082348249.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ilishindikana 2015,hii ngoma bado sana.
Nini lengo la wapinzani?
Unaadhani wataondoa huu unasikini wa watanzania?
Hizo nchi zilizobadili uongozi je zimeedelea kuliko TANZANIA?
Nijuavyo mimi, serikali za upinzani barani Afrika hazijaonesha tofauti yoyote ya kiutawala na kiuchumi barani Afrika mifano ni mingi
Nigeria
Kenya
Zambia
Malawi
Hizi nchi mpaka sasa ni nchi zinazotegemea misaada, na hazina tofauti yoyote ya maana na nchi zenye serikali ya chama kongwe. Watu wana hamu tu upinzani ila wapinzani hawana mbinu zozote za maana za kubadili uchumi.
Naamini maendrlto ya Aftoka yataletwa na waafrika wala si kunfi la watu wanaoongoza bali watu wote.
Mimi si mwanachama wa chama chochote .
 
Umeongea vizuri, ila ndugu yangu kwa chadema hii ya mbowe na lissu nakuapia haifai kuiweka madarakani hata kwa mwezi mmoja......wabinafsi, wajuaji na watemi mno kuweza kumjali na kumsikiliza yeyote yule. Siku zao kumi za kwanza madarakani zirakuwa za kubadili kila kitu ili waweze kuwepo zaidi madarakani......ref. katiba ya chama chao na mwenendo wa lissu. Kuelewa hili hauhitaji hata jicho la tatu, la kwanza tu linakuonesha kila kitu.
Hiyo chadema iliwai kuongoza nchi gani ili uje na hitimisho lako kua haifai?.Hakuna kinachofaa hadi kifanywe kifae.
 
Baba yake raisi wakenta aliestafu hivi karibuni alikuwa chama gani na mtoto wake anestaafu Kwa chama gani?
Baba yake alikuwa KANU na mtoto wake kastaafu kwa chama kingine(nimesahau jina la chama).
Katika maelezo yangu ilikuwa ni kuonesha kwamba si lazima "kuburuzwa" katika maamuzi kwenye uchaguzi.
Watu mwaweza kuchagua chama chochote na mambo yakaenda.
 
Hiyo chadema iliwai kuongoza nchi gani ili uje na hitimisho lako kua haifai?.Hakuna kinachofaa hadi kifanywe kifae.
Dalili ya mvua ni mawingu jombaa, nimesema hapo kuwa rejea tu ufuataji wa katiba yao na mwenendo mzima wa huyo muheshimiwa mwenye kujua sheria
 
Back
Top Bottom