Yaliyomkuta Abdul Jumbe yatamkuta Mwanasheria mkuu wa Zanzibar Mh Othman ?

kwani kura maana yake nini?

"Mwanasheria Mkuu ndiye atakayekuwa Mshauri Mkuu wa kisheria kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na atatekeleza shughuli nyengine zozote za kisheria zitazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais au kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria nyenginezo zozote.".....katiba ya zanzibar sehemu ya madaraka ya serikali kifungu cha 56..inaweka wazi kuwa anatakiwa kuheshimu katiba na kufuata directions za rais kama mamlaka iliyomteua la sivyo angejiuzulu
 
Sita afahamu tu kuwa zanzibar haitokuwa tanganyika milele.
 

Sasa pale kaingia kama mjumbe au mwanasheria mkuu?
 
Wafuasi wa chadema sijui kama kuna alietimia sawa sawa.
 
Sasa pale kaingia kama mjumbe au mwanasheria mkuu?
ameingia kutokana na wadhfa wake hivyo angechagua kutenda kama wadhfa wake unavyomuelekeza kwenye katiba au angejiuzulu
 
Sijawahi kusikia Zanzibar imeshawahi kuwa na raisi anaitwa Abdul Jumbe,,namkumbuka Aboud Jumbe Mwinyi,mmmmh labda walikuwa wana undugu

kwa lugha ya kihaya Abdul ni Aboud
 
Huyu mwanasheria ni mbmumbumbu sijawahi kuona, NAKUMBUKA THE ORIGINAL COMEDY walipokwenda Zanzibar walikuwakuta wakazi wengine kule ni "MNDEMBWEDO" huyu mwanasheria atakuwa mmoja wao

Eti nini? Kwa kipi unacholingana nae? hata ..............!
 
ameingia kutokana na wadhfa wake hivyo angechagua kutenda kama wadhfa wake unavyomuelekeza kwenye katiba au angejiuzulu
Kama ameingia kwa wadhifa wake basi yuko sahihi kuzikataa hizo ibara kwa sababu zinaivunja katiba ya znz ambayo yeye ndo mlinzi wake mkuu.
 
Ameshindwa kazi ya unafiki, ameamua kusimamia kile anachoamini
 
Hivo kwa nini wanasiasa wa bara wanaingangania Znz? Kwa ninj wasiwaache waamue fate yao? Kama wakitaka kuwa na devolution sawa wakitaka kuwa huru wapewe referendum waamue.
 
Kamanda doreen

Maneno makubwa haya...well articulated Mkuu.

tatizo tangu mwanzo ni jinsi wajumbe wa bunge hili walivyopatikana hata hivyo naomba mwenye majibu anipe huyu mwanasheria alikuwa anapiga kura kwa niaba ya nani serikali ya mapinduzi zanzibar au ccm zanzibar au kama mjumbe binafsi kama alivyo ona yeye katiba ni ya serikali au ya wananchi?
 
Last edited by a moderator:
Kama ameingia kwa wadhifa wake basi yuko sahihi kuzikataa hizo ibara kwa sababu zinaivunja katiba ya znz ambayo yeye ndo mlinzi wake mkuu.

katiba ya jamhuri ya muungano ndo katiba mama...na1964 zanzibar na tanganyika zili-surrender sovereignty..hivyo huwezi sema inavunja katiba ya zanzibar bali katiba ya zanzibar ndo inavunja katiba mama ya jamhuri ya muungano wa tanzania
 
katiba ya jamhuri ya muungano ndo katiba mama...na1964 zanzibar na tanganyika zili-surrender sovereignty..hivyo huwezi sema inavunja katiba ya zanzibar bali katiba ya zanzibar ndo inavunja katiba mama ya jamhuri ya muungano wa tanzania

warioba aliyaona haya ndio maana alipendekeza 3 bomba. wale,wapuuzi wakamuona mjinga ag wa zanzibar kawarudisha kujifunza heshima kwa nchi yake as a free sovereign state of zanzibar.
 
kwa lugha ya kihaya Abdul ni Aboud


Mwenye jina lake anaweza kumpeleka mahakamani huyu jamaa ni sawasawa "Chausiku" akaitwa "Chamchana" au "Fataki" akaitwa "Risasi"....... 🙂
 

Kisharia Mh Othman Masoud yeye aliapa kuilinda katiba ya Znz na alichofanya ni kuhakikisha maslah na ustawi wa Znz unapatikana katika katiba mpya. Na pale alipoona kuna kuminywa kwa haki hizo na matakwa hayo alikuwa na haki zote kupinga kwa kula hali na aliposhindwa alijiondosha katika kamati ya Uandishi kwa kutoa sababu zake..

Na hata alipopiga kura amevikataa vifungu vyote visivyo na maslahi kwa Znz. Huyu ni jasiri sana na mkweli na anasimamia haki na maslahi a katiba ya Znz. watu hawa ndio wale wa kupongezwa.

Si kama alivyokuwa mh Kessy amejitahidi kuinanga na kuitetea Tanganyika lakin katika kupiga kure AMEUFYATA na kupiga kura ya NDIO kwa katiba nzima. Watu wa aina hii tunawaita WANAFIKI


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…