Kimsingi kama una akili ya kibinadamu na huongozwi na pepo la Ngono. Huwezi nunua hao wanawake. Katika ujana wangu kabla Mungu hajaniokoa nilitumikishwa sana na Pepo la Ngono na kununua hao watu ila kuna siku nilijisikia vibaya. Morogoro niliendaga Chimbo Moja nikakuta Mama ana katoto kachanga. Amekalaza kitandani alafu anataka anihudumie. Nikasema hata kama nina pepo la ngono ila siwezi fanya hivi. Hii ni kumbukumbu mbaya zaidi katika maisha yangu. Mungu atusaidie kwa kweli. Kwa jinsi ya kibinadamu, huwezi nunua wale watu ila ni pepo la ngono ndio huwa linatumikisha.