Yaliyonikuta kwenye biashara ya daladala

Yaliyonikuta kwenye biashara ya daladala

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Haya nimetulia sasa niwaambie yaliyonikuta kwenye biashara ya daladala🤣basi baada yakuona dereva na konda wake wananizingua sikuhiyo nikaamua niingie mzigoni mwenyewe nikae mlangoni nikusanye hela nione mpaka jion gari itakufa nini au tutapata shilingi ngap ✍️

Jioni dereva kaleta gari nikamwambia kesho tunaamsha wote mwambie kondawako apumzike✍️wakati ule nilikua naishi ukonga kwahyo nikamwambia rot ya kwanza tunaanza sasa tisa nanusu uwe hapa ✍️Basi tumeagana pale kila mtu akachukua time yake tayari kwakujiandaa kwaajili ya kesho✍️.

Basi kisanga kinaanza asubuhi nawasha dcm nafikiri gear zake Rahisi kama za land cruiser 🙌Oya gear unatumia nguvu kama unataka kungoa muhogo kwenye ardhi ngumu🙌nikajikaza nikasema leo mpaka kieleweke nakomaa hivyo hivyo 🤣dereva kachelewa mimi nimetoka mwenyewe nimeanzia mzambaraoni napiga debe mwenyewe abiriq kibao wanapanda nikasema niibe root Kwasababu wa feri ndoyo wengi.

Basi gari imejaa nageuza gomsi dereva ananipigia upo wapi namwambia gomsi kumbe nayeye yupo kituo kipya nimefika pale nikamuachia gari mimi nikarudi mlangoni.Haya naanza sasa kupiga debe oya ya mnazi mmoja posta hii hapa chap tuondoke🤣duuu watu wamekaa chuma inanyanyua hesebu za haraka haraka mmeru mimi nasema kwa hii nyomi sikosi laki 🤣😆🙌. Haya tumefika banana dereva anasema anza kudai nauli. Mimi huyo napita kudai nauli gari yenyewe imejaa hata njia hakuna😆Oya nauli hapo nyuma abiria hawana baya wanafungua nauli zao wananipa siunajua ile sehemu hufiki unasema nichukulie hapo mara yule anatoa anampa abiria mwenzake mpe kond😆

Basi tumeendelea nafika tazara mtu anadai chenji anasema kanipa elfu 10 mhhh sina uhakika ila natoa chenj Nampa maana sijui nani kanipa nanani hajanipa🤣Sasa naanza kuona mbona hela kidogo na gari imejaa full au kuna ambaye sijakusnya huko??mhhh nikaona nisogee kule kwa dereva nimnong'oneze ety gari ikijaa inakua bei gni naona hela ndogo🤣ananiuliza unabei gani mpaka sasa?nikamwambia nina 28,000 akashtuka eehe 28,000!!!😳

🤣🤣🤣🤣🤣Hii biashara mtu asiwahi nishauri kwakweli nitamvunja mguu🤣🤣🙌🙌narudi tumalizie 🙌🙌🙌

Tuendelee kujuzana biashara gani ilitaka kukutia uchizi🤣🤣
@highlight
Magical power
 
Boss unakabia kwa juu ha ha...kipindi tunamaliza high school miaka hiyo, nilimaliza na mwana, Shemej yake alistafu akanunua costa, yeye alikuwa dereva, akamwambia jamaa awe konda atafute Ada ya chuo!, wakakomaa baada ya mwaka Ada ikapatikana....
 
Ile kazi sio rahisi kama wengi wanavyodhani...ni ngumu sana hasa kwa jiji kama la daslam..na ndio maana kwa tajiri asiyejua ugumu wa kazi atabadilisha Kila siku madereva na makondakta .
 
Boss unakabia kwa juu ha ha...kipindi tunamaliza high school miaka hiyo, nilimaliza na mwana, Shemej yake alistafu akanunua costa, yeye alikuwa dereva, akamwambia jamaa awe konda atafute Ada ya chuo!, wakakomaa baada ya mwaka Ada ikapatikana....
Umeona sasa angempa mtu je unafikiri angepata iyo ada kwa huo mda
 
Nimecheka 😹😹😹
Kuingiza gia km unang’oa mzizi wa muhogo 🤣🤣🤣

Abiria wamekuingiza Chaka wanadai chenchi ya elfu 10 wakati wamekupa buku, km nakuona mijicho ilivyokutoka..!!

Kalaga Baho Nongwa njoo umuone pacha wako huku 😹
Na kuna abiria makauzu sana, akikucheki tu anajua huyu sio mzoefu,lazima akutie damage.
 
Mkuu sometimes biashara usipo kua nayo kalibu kujua kinacho ingia na kutoka kwa siku nayo ni rahisi mno kufirisika
Malizia kwanza ndo uanze kureply comments puliiizzzz 🤣🤣🤣

We jamaa umefanya nimecheka sana.!! 😹
 
2003 nilipomaliza sekondari mzee wangu alininunulia Hiace dungu (Kipanya) kifanye daladala ili nianze kuwekeza pesa za chuo. Kilikuwa kinapiga route ya Tabata Mawenzi - Buguruni.

Ile gari kila siku ilikuwa haiishi matatizo, kupelekea kupigana sound katika kupewa hesabu jioni ikifika. Hesabu ilikuwa 25,000 kila siku na Jumapili ilikuwa ni ya Dereva na konda. Ila kuipata hiyo 25,000 ilikuwa mbinde.

Siku moja nikaona isiwe kesi, nikaamka na gari. Mimi nilikaa siti ya mbele nazunguka tu na gari. Cha ajabu siku nzima mpaka saa 9 hakukuwa na pancha, kukamatwa wala tatizo lolote. Ilipofika saa 10 dereva akapigiwa simu kuwa kuna tatizo kwake, ikabidi ampe jamaa yake 'deiwaka'. Kipindi hicho bado nipo siti ya mbele.

Dereva wa deiwaka kuingia tu, akamuuliza konda, vipi leo umetoa taarifa ya kukamatwa au kuharibikiwa kwa boss wako. Konda akajifanya haelewi. Dereva alikuwa hanijui, alidhani ni abiria. Na nilipokaa konda hawezi hata kumtonya.

Jamaa akawa busy anamsifia konda kuwa kwa speed wanayokwenda nayo, yeye na dereva wake watanunua hiace yao muda si mrefu maana wamepata Boss mjinga.
Hapo ndipo nilipogundua kulikuwa na hujuma za makusudi ili wao wavune mimi niumie.

Tulipopaki ile gari jioni nilipata pesa yangu kamili ya siku na ikawa ndio mwisho wa ile daladala maana nilimwambia mzee auze tu gari yenyewe.
 
Back
Top Bottom