Ilikuwa ni tarehe 12 mwezi wa 7 mwaka 2018 njiani kuelekea Tabora mjini tukiwa kwenye usafiri wa jumuiya HBS Express tukitokea Dar Es Salaam. Tulifika Tabora mjini saa tano usiku kutokana na changamoto ilijitokeza katikati ya safari Bus lilipasuka Tyre hivyo tulisubiri Tyre itoke tabora mjini iletwe porini ambapo bus hili lilipata hitlafu, baada ya masaa mawili hivi tyre ililetwa wakafunga ngoma ikasepa. Mida ya saa tano usiku tabora ilikuwa imezizima kiasi labda pale stend tu ndokuna madogo wanakesha kulinda mizigo na mabus na kuuza vichipsi yai.
Nikaona niende lodge nikamtafuta bodaboda akanipeleka lodge moja inaitwa ZIMBABWE LODGE chumba 20000 ni kachukua chumba ila usingizi ukagoma nikamuuliza mdada wa reception bar ya karibu nikapate kinywaji akasema niende Oxygen gas huwa wanakesha. Nilipoenda nikalewa nikachukuwa Malaya mmoja anaitwa Regina japo huwa wanataja majina ya uongo. Huyu Malaya nililala nae Ile kuamka saa mbili asubuhi nikakuta kaloweka nguo zangu zote, Kaiba simu yangu tecno photom six, Kaiba wallet jinsi ilivyo Ina pesa zote na vitambulisho.
Akaacha ujumbe wa maandishi mezani KOMA KUCHUKUWA MALAYA USIOWAJUA KWAO NI WAPI. Nilitaka kulia ila kwa kuwa mm ni mwanaume nilijikaza kisabuni wahudumu walicheka sana wakisema mkaka umetoka safarini badala ulale unafanya uzinifu wa kipumbavu, walinitukana japo hawanijuwi heshima yangu ikawa zero. Nilichukuwa zile nguo nikaanika zilipokauka nikasepa bila kuaga
View attachment 2330016