Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Unasema umefika ilemba Kisha mmkanza kutembea kwa miguu kuelekea ziwani mbna ziwa na ilemba hakuko mbali na Kijiji Cha nankanga Ni karibu tu kwa pikipiki natembe kwa dakk kumi had Kumi na tano kufikaa ziwani sas sijui jama alikupitisha wapi napata wasiws mkuu
 
Nimekaa sana NANKANGA, ilemba, Kuna mradi wa maji tulifanya maeneo hayo
Ziwa Tanganyika, ziwa Rukwa, hayo maziwa yote huwezi nipoteza huko, Chocho zote najua, Hadi ukivuka Tanganyika huwezi nipoteza pande zote!
Hata mm niliwai kuwa pande hzo bonde Hilo la sumbawanga nimekuepo nikipeleka mirad ya umem sas Kuna sehemu kanichamganya kidg kusema ilemba Ni mbali na ziwa sijajuwa walienda kuingilia kambi ipi kwan ilemba na nankanga Ni jirani tu ila huyu Ni mpwayangu at his best
 
Kuna Kasumba Mbaya sana JF..na inawakimbiza sana watu...mtu akileta story yake watu wanajaribu kwa nguvu zote kuifanya iwe ya uwongo na ikose posts za kutosha....shida ni nn?
Roho mbaya tu
 
Wakanifikisha nchi kavu mpaka hapo macho sioni Tena yamevimba hakuna Mfano .siwezi kutembea hata kukaa nashindwa raia karibia Kambi Zima wakaja kunishangaa pale .jamani mbona mmefanyia hivi huyu mtoto ? Jamaa wale wengine walikuwa makauzu sana nikasikia yeye anshukuru amefika Huku salama basi hayo mengine mtamuuliza mwenyewe . Nak umbuka mama alikuwa na mgahawa wakati huo pale kambini alikuwa maarufu Kwa jina la mama wiston, akapata uchungu sana wakanibeba mpaka mgahawani kwake na kuanza kunipa huduma ya kwanza ,hapo mdomoni siwezi kutafuna chochote Kwa jinsi nilivyopigwa, ni vidonda vitupu na mabonge ya damu .yule mama alinisaidia sana kunikanda na Kuninunulia dawa za maumivu, ilipita siku tatu ndio nikaanza kurudi angalau kwenye uafadhari yule kanishauri niondoke nirudi nyumbani nauli angenipa ! Nikiwa kwenye haali ya majeraha Kuna jamaa alikuwa anaitwa mangi ..kaniuliza dogo wewe malenngo Yako nn? Nikamsimulia kwamba Mimi shida yangu ada ya chuo yule jamaa akanitia sana .dogo sikiliza mm mwenyewe nimekuja Huku miaka kumi iliyopita nilishalowea Huku kikubwa usikate tamaa mi nakushauru usirudi nyumbani ukipona nitakufundisha kazi ambayo ndani ya miezi miwili tu utakuwa umepata hiyo pesa huo ndio uaname ..yule jamaa nikamwelewa lakini nikawa natamani niende nikatoe taarifa Kwa wazazi wa Fred kwamba jamaa kaliwa na mamba nauli ya kurudi Tena nitakosa baada ya wiki Moja nikaanza kujifunza kuvua samaki ,ikawa tunaenda ziwani na wazoefu tukirudi napewa mgao wangu .ilikuwa Kwa siku unaweza kuondoka hata na 50000 yule mangi akaniambia dogo Mimi Hela nitakuwa sikupi tutakuwa tunaandika tu ikifika million Moja nenda shule .nilifanya Huku nikiwa na makovu na hata nguo yule jamaa alikuwa ananipa navaa za kwake ,baada ya miezi mitatu tukapiga hesabu ikaonekana namdai milioni Moja na laki tatu nikajua hatanipa .yule mangi ni mtu wa mungu siku aliniita akanishauri dogo Huku hakufai nenda shule akanikabidhi million Moja na laki Tano !!nakumbuka yule mama pia alinichangia 70000, ila tayari nilikuwa na makovu ambayo mpaka Leo imekuwa kama kilema mwilini mwangu! Nilikuwa na hasira Sana na Mzee wangu nilipanga nikifika nyumbani nitamwonyesha makovu niliyopata nitabeba begi kuelekea chuo nakumbuka nilifika tunduma Saa Tano usiku ,Moja Kwa Moja nikaelekea nyumbani nikiwa na furaha na huzuni ,nikiwa natamani kumkuta Mzee akiwa hajalewa nilikuwa na hasira nae Sana !! Ile nafika nyumbani nakuta geti liko wazi na sio kawaida nimeingia mpaka ndani naona Hali isiyo yakawaida naangalia mlangoni nikaona kufuli ,chumba Cha wadogo zangu pia Kuna kufuli nikamgongea mpangaji Mmoja wa pale nyumbani ambae alikuwa ni mama mtu mzima! Ile kuniona nikamuona kama anahamaki ,,we mtoto ulikuwa wapi tumekutafuta sana ..nikamuuliza Kwani Kuna nn ? Yule mama kanimaliza kabisa ...baba Yako amefariki hii ni wiki ya tatu walisafirisha msiba kwenda kijijini kwenu bado hawajarudi duuu!!!majanga yakazaa majanga kiufupi niligeuka Tena kuwa mlezi wa wa wadogo zangu mpaka Sasa mungu alinijaalia wote wameolewa wanajitegemea na Sina majuto Wala laumu Kwa yeyote nashukuru tu mungu kuniokoa na mauti ..mwisho
Daah pole sana ndugu.
 
Ukiwa mgeni na una uchovu wa safari tena usiku,lazima uone mbali,tena walikua wanatembea kwa miguu,lazima aone mbali.
 
Back
Top Bottom