Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Yaliyonikuta Ziwa Rukwa sitokaa niyasahau

Dah,wewe umenifungua macho, Kuna wadada wawili nawafahamu wote wamekimbilia Rukwa kwenye mabwawa ya samaki baada ya kuzidiwa na madeni ya vikoba ,na Benji japo kila mmoja kaenda kimpango wake...kumbe uchaka wa wanyang'anyi
Hao madada wakoje? Wana chura? Ntumie picha zao pm nikijiridhisha ntawasaidia kulipa
 
Ni kwa vile hii nchi ina uongozi wa hovyo, lakini mtu kama huyu alitakiwa asaidiwe na kodi zetu, bahati mbaya tukishalipa akina Mwigulu wanakwapua na kujinunulia posh cars moja shilingi 500m. Hii 500m ingesomesha wangapi. Rubbish.
Story yako imenigusa sanaaa. Pole
 
Ilikuwa mwanzoni kabisa mwa mwaka 2000 nikiwa nyumbani pamoja na wazazi wangu katika mji mdogo wa tunduma karibu kabisa na shule ya msingi maporomoko.

Sitasahau wakati huo nilikuwa nikiishi na mama wa kambo baada ya kumpoteza mama yangu mzazi .maisha nyumbani yalibadilika ghafla na baba akawa ni mtu wa kulewa na kurudi usiku wa manane.

Ilikuwa akifika tu basi wote mtaamshwa kupigiwa makelele usiku kucha ,Mimi na wadogo zangu ambao wengine walikuwa wadogo kabisa, ilifika mahari tunalala njaa.

Yule mama wa kambo alibadilisha kabisa maisha na tabia za baba akawa ni mtu wa hovyo sana. Wanakula kilabuni wanarudi usiku Mimi nabaki napambana na wadogo wazangu na nilikuwa nataka kwenda chuo lakini Mzee kasema hawezi kupoteza pesa yake kunisomesha natakiwa nipambane mwenyewe.

Niliamua kujiongeza kufanya vibarua mchana jioni nikipata kitu napelekea wadogo zangu ndio hapo nilikutana na jamaa Mmoja anaitwa Alfred akanipa mchongo wa kwenda kuvua samaki ziwa rukwa.

Nilijichangachanga nikapata nauli nikawaaga wadogo zangu Kwa uchungu sana ilikuwa hakuna namna lazima nikapambane na Kwa vile jamaa alinipa matumaini ya kupata pesa nyingi Kwa muda mfupi nikaamini kabisa naenda kutoboa, tuliondoka Tunduma Kwa usafiri wa fuso kuelekea bonde la ziwa rukwa kupitia laela, Kalambanzite na usiku karibia Saa nne tukafanikiwa kufika Kijiji Cha Ilemba ambapo ndio mwisho wa gari.

Tukalala asubuhi mapema tukaanza kutembea Kwa mguu nakumbuka tuliamka Saa 12 mapema.

Kuendelea bonyeza kiungo hapo chini

Sehemu ya pili
Sehemu ya tatu
Aina ya usimuliaji ni ile ile. Kwa nini unapenda sana kubadili ID? Unajitihidi ila bado kiwango chako cha uandishi hakiwezi kuteka mtu kama mimi. Kuna mambo mengi sana hayana uhasilia kwenye simulizi zako.
 
😃😄😃kwani yeye ndio amesababisha Fred afe? Wakulaumiwa ni Fred kwa sababu yeye ndiye alitaka kusababisha kifo cha mleta thread
Lakini wakati anakufa alishindwa kumsaidia. Hivyo damu yake atailipia tu.
 
Ni stoli tu. Huyu ndiyo aliyetunga stori ya msitu wa Shengena
 
Vp kwani unataka kumtunuku tunda kimasihara?😀
ah
Mmmmmgh Ile million ilishaisha kama ndio unaipigia hesabu
khah!Hzo milion wala hazinipi wenge..ye mwenyew ndo kasema zilivutwa akahisi atapoteza uanaume,sasa kupoteza ni hasara kubwaa kuliko hata makovu aliyo nayo,nd mana nimetaka kujua kama hicho kikombe kilimuepuka.
 
Aina ya usimuliaji ni ile ile. Kwa nini unapenda sana kubadili ID? Unajitihidi ila bado kiwango chako cha uandishi hakiwezi kuteka mtu kama mimi. Kuna mambo mengi sana hayana uhasilia kwenye simulizi zako.
Kutoa maoni au hoja hakutokani na ujuzi wa kuandika Bali Nia ya kukifikisha kile unachokusudiwa .huenda wew unajua kuandika Kwa mpangilio sio lazima na mm nijue na hii sijaiandika kumlazimisha mtu aisome ni hiari
 
Back
Top Bottom