Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
CHADEMA kama viongozi, makada na wafuasi wake makini ni kikundi kidogo sana ambacho hakiwezi kabisa kuzuia dola yenye nyenzo zote za taifa hili kuiba uchaguzi.Kama CHADEMA mmeamua kushiriki chaguzi zijazo, 2024/25, mjue for sure yale yale yaliyotokea 2020 yatatokea tena maana jana yametokea Ujiji Kigoma kwa ACT Wazalendo (ingawa ACT ni tawi la CCM ie (CCM vs ccm) kwa kukamata kura za wizi na polisi kuwakingia kifua CCM kwa kuwakamata viongozi wa ACT kuwafunga walipoingilia kati kuzuia wizi huo wa kura wa CCM.
BY HOOKS AND CROOKS LAZIMA CCM IFANYA YALE YALE YA 2020 MAANA WAMEANZA KIGOMA JANA.
MMEJIANDAAJE NA HUJUMA HIZO? MNA UWEZO WA KUKABILIANA NA POLISI? IF SO HOW?
Hata hiyo katiba na tume huru, CHADEMA kama hicho kikundi hawakuwa na ubavu wa kulazimisha dola ikubali viwepo. Labda kwa mtu asiye na picha ya dola hapa nchini ni nini hasa.
TUANGALIE PICHA KUBWA. NI nani hasa anayeibiwa uchaguzi? Ni kweli kuwa wagombea wa CHADEMA na chama chao kuna manufaa ya kiuchumi na hadhi wanayopata kwa kushinda majimbo ya uchaguzi. LAKINI hao na familia zao ni watu wachache sana ambao uwepo wao hapa duniani ni mfupi sana. Umuhimu wao uko kwenye kazi wanayotarajiwa kuifanya Wakichaguliwa na wananchi.
Wanufaika wakuu wa uchaguzi ni wananchi milioni 60+. Wao ndio wanajua ni wagombea gani wa chama kipi watawapa uongozi na uwakilishi bora. Sasa kama dola inapora ushindi wa wagombea waliochaguliwa na wananchi halafu watu wanawazodoa wagombea na chama chao (kikundi) kwa kutopambana na vyombo vya dola kuzuia kuporwa kwa kura za wananchi basi tuna nchi ya ajabu sana hii. Sijui wangapi wanafurahia bunge la sasa na halmashauri zilivyo.
Kuna wakati nilitamani CHADEMA waachane kabisa na chaguzi hata siasa ili tubaki na chama kimoja na vyama vibaraka kama enzi za Mobutu na Zaire yake. Labda watu watapata somo. Lakini nikakumbuka kuwa ni jeuri ya CHADEMA kuendelea kuwepo ndiyo inayodhihirisha jinsi mfumo wa uongozi wa nchi na siasa ulivyooza na jinsi sisi raia tulivyo gutless mbele ya genge la mafisadi.
Pia sioni tatizo makada wa CHADEMA wakipata manufaa yao madogo ya kiuchumi kutoka keki ya taifa kwa kazi yao muhimu wanayotufanyia wakati sisi tunaendekeza ujinga mbele ya watawala badala ya kujiunga na kuongeza nguvu ya mapambano. Uwepo wao angalau unatupa mwanga wa matumaini kwamba bado wapo watu wenye guts nchini. One day things might change.