Yaliyotokea Leo Chamazi baina ya Azam vs Coastal Union ni aibu kubwa sana kwa soka letu Tanzania

Yaliyotokea Leo Chamazi baina ya Azam vs Coastal Union ni aibu kubwa sana kwa soka letu Tanzania

yaah Angalia mechi ya Argentina na Saudi Arabia, dakika za nyongeza zilikuwa 8 na bado mwarabu akapoteza muda kwa kujiangusha hovyo. ikabidi refa aongeze dakika nyingine 8. Kiufupi mambo ya kupoteza muda ni uhuni.
FIFA ndio wanatoa miongozo ya uchezeshaji na uendeshaji wa mpira wa miguu. Toka michuano hii ya kombe la duniani ianze tumeona mechi nyingi tu zimeongezwa zaidi ya dakika 12, first half dakika nne na second half dakika nane huku kukiwa hakuna upotezaji wa muda wa kupangwa kama ilivyokuwa kwa Coastal Union jana.
 
Mimi nashangaa sana watu wako na mawazo kila kitu kuhongwa refa alikuwa sahihi kabisa na hii kusema dakika za nyongeza mfano 4 haina maana dakika 4 tu maana yake chini kabisa dakika 4 ila kwa mechi kulikuwa na muda mwingi ukapotezwa na dawa ya hii ndio refa kufidia lakini team nzuri kama umeweza kuzuia kwa dakika 90 na wewe mzuri unalia kwa dakika 4 kitu gani? kama wanalia kwa dakika 4 basi wanastahili kufungwa team nzuri yenye kutaka kushinda imeshinda.
Na lile goal wamefungwa kwa laana ya Mungu mpira umegonga beki ukawa clear assist kwa iddy Nado
 
1. Dakika za nyongeza zilikuwa 4 lakini zimepigwa dakika za nyongeza 10.

2. Baada ya kuongeza dakika hizo, azam wakafanikiwa kufunga bao la 3 na la ushindi, hivo matokeo yakawa 3-2

3. Vurugu kubwa imetokea uwanja wa chamazi kutoka kwa wachezaji wa coastal ambao waliona dhahiri shahiri haukuwa mpira tena bali ni mipango

4. Ligi imeshafikia pabaya, mazingira ya leo pale chamazi yameleta simanzi sana, sana, sana, sana

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Refa wa jana anastahili pongezi,
Kipa kajifanya kuumia toka dakika ya 86 mpaka ya 94 ndo ananyanyuka. Alieongeza dakika alipaswa aongeze hata 10 au zaidi
 
Mpira sijaangalia lakini kwa mujibu wa maelezo yako ndugu yangu, dk ziliongezwwa 4,mchezo uliendeleq dk ya 95, 95+4=99, sasa iweje game ifike 101 kama mleta mada alivyodai?
Uliangalia mechi ya Argentina na Saudia Arabia? utapata jibu
 
Muhimu umesema kwa ufahamu wako Ila kwa taratibu za soka sio hivyo. Angalia hata kombe la dunia mwaka huu muda wowote unaopoteza lazima ufidiwe wakiongeza 6 ukizipoteza watafidia mpka zifike dakika halisi za kucheza.


Game za mwanzo team zilikua zinapoteza muda Ila tangu waone utaratibu wa kufidia dakika wote wameacha ujinga.
Mkuu ila Kombe la Dunia si ni sheria mpya hizo? Una uhakika katika ligi ya sasa, sheria hizo zimeshakuwa adopted maana sheria mpya zinachukuliwa mwanzoni kwa msimu siyo katikati?
 
Umeangalia mpira ndg....
Coastal wajilaumu wenyewe refa Hana kosa
Hana kosa kivipi mkuu?
Kumbuka ziliongezwa dakika nne.
Bora wangeongeza dakika 10 za ubaoni wangeeleweka siyo ule upuuzi.

Nilimwambia jirani yangu wa kibandaumiza "huyu refa atakutana na ngumi ndoige" ilipofika dakika ya 96.
 
Kama kawaida watoto wa kambo wa taifa hamuishiwi lawama. Simba mna shida gani, mmeanza kuwaonea wivu hadi Azam?
 
Tunaweza kuwatetea Azam kweli lakini kwanini mechi zote sasa hivi zinazochezwa pale chamanzi refa lazima aharibu
 
Mpira sijaangalia lakini kwa mujibu wa maelezo yako ndugu yangu, dk ziliongezwwa 4,mchezo uliendeleq dk ya 95, 95+4=99, sasa iweje game ifike 101 kama mleta mada alivyodai?
game ilifika dk101 kwa sababu ya vurugu walizokuwa wanazifanya wachezaji wa coastal union waliokuwa bench refa alilazmika kusimamisha mpira kutuliza hali ya uwanja baada ya kuanza kutupiwa makopo
 
Mkuu ila Kombe la Dunia si ni sheria mpya hizo? Una uhakika katika ligi ya sasa, sheria hizo zimeshakuwa adopted maana sheria mpya zinachukuliwa mwanzoni kwa msimu siyo katikati?
Sheria mpya zimeanza lini? mpira una sheria 17 worldwide
 
Tunaweza kuwatetea Azam kweli lakini kwanini mechi zote sasa hivi zinazochezwa pale chamanzi refa lazima aharibu
Kipindi Azam FC ananyongwa watu walikaa kimya na sasa hivi mkae kimya
 
Hata zikiongezwa dakika 30. Timu yeyote ingeweza kushinda, kwa hiyo kuongezwa dakika hakutoi faida kwa timu yeyote.
hasa kama kila timu ilikuwa na wachezaji 11. Je Coastal wangefunga?
 
Nipo upande wa refa licha ya kuwa sishabikii soka la bongo na yote sababu ni nidhamu ya wachezaji wa kibongo na ligi nzima...

Yaani ukitaka kuchukia mpira wa bongo timu underdog ifunge goli la mapema yaani soka linakuwa limeisha...

Kujiangusha angusha kusiko isha, kujiumiza ata kama mchezaji hakuguswa....

Leo refa kawaonesha wachezaji wazembe namna watazamaji wanapenda soka na siyo maigizo maana wanatoa pesa na muda wao ili kupata burudani na siyo vinginevyo...

NOTE:

"Angalia world cup uone mpira siyo maigizo"

Asante
Huwa najiuliza sana huu upitezaji wa muda kwa wachezaji wa Tanzania una faida gani kwa soka letu? Kwa ujumla Tanzania ndio nchi ambayo wachezaji wanapoteza muda bila sababu kwa muda mrefu na hawachukuliwi hatua sitahiki. Nilianzisha Uzi wiki iliyopita nikisema kanuni za kufidia muda wote uliopotezwa zilizoanzishwa na Corina ziletwe na huku tuone kama kina Metacha Mnata watajilaza tena dakika 4.
 
Back
Top Bottom