Yaliyotokea mpakani na Kenya, Zambia na Rwanda yanaonyesha haja ya umakini kwa Magufuli kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani wenye uwezo wa kidiplomasia

Naona Wakenya mnaendelea kutoka mashimoni mlipokuwa mmejificha.. Bado dawa yenu inachemka..
Nadhani wewe mtu akiongea kitu ambacho hukubaliani nacho basi atakuwa ni Chadema au Mkenya, sivyo? Jifunze kuongea kwa hoja badala ya tuhuma, huo ndio uungwana katika jamii.
 
John atakuwa aliwapigia simu martin na Anna akawaambia wachimbe mkwara.

hujamsikia balozi ameambiwa na aidani kuwa ampigie baada ya wiki kwa sasa yuko bize?
 
Wewe tuliza kitesi huko ebhoo
 

Mkuu hiyo reaction ya hao RC's ni maagizo ya jiwe direct.
 
Hio ndio dawa yao. Ilibidi wakuu wote wa mikoa mipikani wafanye kama Tanga. Ingependeza sana.
Tuoneshane makali kidogo kidogo
Unajua uungwana ni sifa, sio udhaifu. Ukikumbuka hilo maisha yako nyumbani, kazini hata na jirani zako yatakuwa mazuri sana
 
RC Shigela sio mwanajeshi,nadhani point yako ni kwamba RC's wa mikoa ya mipakani lazima wawe na uelewa na diplomasia,hata hvyo RC wa kigoma kwa mfano alishakuwa mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Tanzania Marekani
 
Hebu Wape Ushaur hawa waliokosa dipolo.masia wafanye nn cha kidipolomasia ili wadeal na kukosa "diplomasia" kwa Rais wa nchi jiran.

Naomba uwape USHAURI ambao n Substantive


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu Wape Ushaur hawa waliokosa dipolo.masia wafanye nn cha kidipolomasia ili wadeal na kukosa "diplomasia" kwa Rais wa nchi jiran.

Naomba uwape USHAURI ambao n Substantive
That is very simple. Unapo deal na mtu mwenye kukosa diplomasia onyesha diplomasia!
 
Mkuu, unajua inawezekana Rwanda waliamua kuwa na diplomasia kuliko sisi ndio mana tatizo pale likaisha, umefikiria hilo?
Inawezekana kabisa,upo sahihi...Lakini pia inawezekana majirani zetu wa kaskazini-mashariki wana diplomasia ya chini mno kuliko sisi...Rais wetu si alitangaza hatafunga mipaka kutokana na majirani zetu kutegemea bidhaa kutoka kwetu hasa chakula na wengine za bandarini? Hapo tu diplomasia alishaionyesha....Sasa walimwamsha aliyelala walitegemea nini? Hawa walijiamini sana na kuona hakuna atakayewatikisa zone hii...Let's see who is who.
 
Mimi naona Shigela amekuwa mpole ilitakiwa zaidi.Jumuiya ya Africa mashariki ilikufa sababu ya unyang'au wa hawa watu.
Uweke diplomasia na watu walioshindwa kuunganisha makabila yao.
Mkuu, hivi Tanzania tunaweza kuwasema wakenya kuhusu ukabila? Kwani kabila ni nini - kikundi cha watu wenye desturi na mila na lugha sawa. Na ukabila unakuja pale ambapo kikundi kimoja cha namna hiyo kinakuwa na bifu na kikundi kingine, sivyo?

Basi kwa jinsi hiyo hata chama cha siasa kinakuwa ni namna ya kabila.Tunaweza kuwa na kabila la CCM, na kabila la Chadema, ACT nk

Sasa niambie, wepi wana hali mbaya zaidi - Wakenya katika ukabila wao wa vikundi vya lugha au Watanzania katika ukabila wetu wa vikundi vya kivyama?

Tanzania hata siku moja hatuwezi kuwasema Wakenya katika ukabila wao wa vikundi vya kilugha, kwa kuwa ukabila wetu wa vikundi vya kivyama unaweza kuwa mbaya kuliko wa kwao!

Nilimshangaa sana Prof Kabudi bila aibu anawaambia Wakenya waache ukabila. Tanzania tuna hali mbaya ya ukabila wa kivyama kuliko Kenya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…