Sawa kaka, Swali la hati za majengo anazo nani hilo swali bwana Mo alitakiwa kujiuliza mapema maana yeye si mgeni hapo simba.
Unajua watu wengi mnajipotosha mnapoamini kwamba tayari kisheria simba na Mo walishafikia kupeana hizo hisa. Kilichotokea ni kwamba kuna Azimio la Mkutano mkuu wa simba kukubali kumpa Mo hisa lakini hakuna makubaliano ya kisheria yaliyofikiwa,
Ili Mo amiliki hizo hisa 49% ni lazima kuwe na makubaliano ya kisheria ambayo yatasimamiwa na pande mbili yaani Klabu ya simba na mwekezaji Mo. Nani anaweza kutuambia ni lini na wapi Simba na Mo wametiliana saini makubaliano ya kuuziana hizo hisa?
Jee ni nani anaweza kusema hizo hisa 51% za wana Simba zinapatikanaje na ziko wapi? Kwa ivo hapa watu wanajadili kama vile suala la Mo kupewa 49% ya Klabu ya simba tayari limeshatokea lakini hata mchakato wenyewe bado kabisa kuanza.
Mchakato hauwezi kuanza kama thamani halisi ya Klabu haijulikani, na Mo alisema kuwa atawekeza bilioni 20 kwenye klabu lakini hakusema atatoa bilioni 20 kwa Klabu.
Kama Klabu ikithaminishwa na kuonekana ina thamani kubwa zaidi ya shilingi bilioni 44 basi Mo inabidi aongeze fedha anazotaka kuwekeza zifanane na thamani ya hisa za Klabu zilivyo.
Na ijulikane inawezekana baada ya tathimi ikaonekana Simba thamani yake ni shilingi bilioni 10 basi hata hizo bilioni 20 za Mo zitakuwa ni zaidi ya thamani ya Klabu.
Na kuna watu wanazungumzia mashabiki kama ni sehemu ya "mtaji" wa Klabu. Hivi shabiki ana ulazima gani wa kununua Jezi za Klabu? Nani anaweza kutuambia kwa hakika kwamba Mwaka jana Simba iliuza Jezi za shilingi ngapi kwa mashabiki wake?