Yameanza kwa TRA yatafata kwengine, TRA kusimamia wenyewe ajira badala ya utumishi tunarudi kule kule kwenye ajira za ukoo na kujuana

Kama hujui kitu uliza usitake kujifanya mwerevu kumbe ni mweupe ibada ya mchana uliisikia wapi sabato inaanza ijumaa jioni mpk jmosi jioni hakuna kufanya kazi yoyote wewe hiyo ibada ya mchana umeitoa wapi usifananishe imani ya wasabato na wengine
 
Mimi nilichojifunza maisha ya Tanzania ni kwamba, kuna maamuzi yanafanywa na watu kwa lengo la manufaa yao, yaani na wenyewe wanufaike. Taasis zipo nyingi siyo TRA. Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake!
 
Ungewashauri tume ya ajira iache urasimu haya yasingetokea.
Taasisi inaomba kuajiri wanaruhusiwa baada ya mwaka sasa itakidhi vipi mahitaji ktk hicho kipindi cha mwaka wamekaa bila wafanyakazi
 
Kwani utumishi inasimamiwa na mashine?
Kama ni binadamu kwani heads wa utumishi na mashirika hawajuani.?
Kusema utumishi wanakuwa unbiased syo kweli
 
Hii ni awamu haramu ya uongozi na utawala. Maskini hamna chenu, zaidi ya njaa, kukosa na kaburi.

CCM ni chama dhalimu
 
Hoja ya MTOTO wa MASKINI sijawahi ielewa kabisa.

Mtoto wa TAJIRI hana HAKI ya AJIRA isipokuwa Mtoto wa MASKINI?

Yawezekana huyo MTOTO wa Maskini akawa ndio tatizo zaidi maaana tyr ni MASKINI, akipata kazi atawaza KUIBA tu ili ajikomboe na UMASKINI.. ee unaon Mentality ilivyo?

Turudi ktk MADA,

Watanzania Sisi ni WANAFKI sana, ukiona mtu analalamikia jambo basi ujue HANA FAIDA nalo.. Akifaidika nalo hutomskia akibwabwaja tena.

Ndio maana Wanasiasa wanawapa rushwa ya kofia na Vitenge vya Chama. Mnajisahau mnawapigia KURA tena.
 
Acha ujinga
 
Kama hujui kitu uliza usitake kujifanya mwerevu kumbe ni mweupe ibada ya mchana uliisikia wapi sabato inaanza ijumaa jioni mpk jmosi jioni hakuna kufanya kazi yoyote wewe hiyo ibada ya mchana umeitoa wapi usifananishe imani ya wasabato na wengine

Aisee, watu huwa wanafanya mtihani hadi ijumaa na ni siku ya Waislam kuswali unataka nao waje kulalamika hapa ?.. Yan mtu kaleta hoja ya msingi kabisa we unataka kuleta maswala ya dini hapa mkuu ??
 
haya mashirika ni yale yanayojiendesha kwa rasilimali zake yenyewe, ni kwamba lazima ifike sehemu yawe na mentality ya private sector, yaweze kuajiri kulingana na vigezo vyake yenyewe bila kufuata vigezo vya Serikali kuu
 
Utumishi walikua wanaajiri watu, wakifika kwenye mashirika mashirika yanawarudisha sababu hawakidhi viwango. Sasa sielewi inamaana process nzima ya kuajiri haikua inamhusisha aliyeomba kuletewa watu au.
 
Mbona kuna safari walipanga usaili jumapili, hapo ni sawa si ndio? Nyie na hilo dhehebu lenu mna mambo mengi sana amueni moja
 
Kwa waliotoboa kupitia utumishi wanajua umuhimu wa Utumishi kwenye suala la ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…