Yamenikuta leo Mama G

hahahahahahahhaa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli kabisaa!wazungu na wahindi wanazk sana kwenye nyumba zao
 
Hahaha, nilishakuelewa sana ,umenikumbusha 007
 
Sawaa
 
Kali yake
 
Unatumia Nguvu nyingiii alafu Akili kiduchuu!!

Tatizo hilo
Ni kweli inahitaji akili tulivu zaidi ya mashaka. Nayaona yale ya ndugu yalikuwa mashaka hofu na wasiwasi. Nilikuwa hotelini ghorofa ya juu. Nikaenda bafuni kuoga. Milango ni ile ya kuteleza. Bafu ina pangaboi la kuingiza hewa. Ukiwasha taa nalo linawaka. Sikuwasha nilipoongia maana taa za "corridor" kuelekea mlangoni zilikuwa inawaka na kutupa mwanga bafuni. Bafu upande wa mlango ni vioo tupu "aluminium" (isiyopenyeza macho kuona upande wa pili). Ukifunga mlango wa bafu hupati hewa ikiwa pangaboi halitembei. Wakati naoga sikuufunga mlango wa bafu (ule wa aluminium wa kuteleza). Mlango ulikuwa umefunguka kwa nusu. Hivyo sikuona shida ya kupumua. Nilipomaliza nikataka kuufungua wazi wote yaani kuufikisha mwisho wa reli yake. Hapo ndipo shida ilipoanza. Nilipokuwa namalizia kuufunga ili utembee katika reli yake vizuri, mlango ukajifunga. Ukajibana. Ukagoma kufunguka. Hewa sasa haipiti. Pangaboi haliwaki. Mwanga umepungua. Nika-"panic!". Nikapiga ukuta wa chumba kwa upande wa bafu labda mfanyakazi akipita hapo atasikia. Kuvunja vioo vile vigumu sitaki. Nilijua sitaweza bila kujijeruhi na kudaiwa baadaye na hoteli.Kisha nikasema moyoni: "tuliza akili Mgileadi." Nikajua nina dakika chache za kupumua na hewa iliyomo itakwisha. Nikainama kwenye zile reli nikaunyoosha ule mlango uliojikita mahali nikaufungua. Nikapumua kweli kama dakika 5 hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…