Yamenikuta leo Mama G

Yamenikuta leo Mama G

Hahahahahahaha pole sana nacheka kama mazuri,,nilichukua ile mop ya kudekia nikaangalia hapo juu kwenye dari nikajisemea naweza kutana na nyoka hukp au nikaumwa na nge bure ,,umenichekesha kumbe we mwenzangu ulikaa sana
Acha mama ile siku ndio nilijua mi ni mwanaume kweli embu fikiria mizoga ya panya imenizingira,joto Kali niko na boksa tu ile harufu ya chakula cha kitimoto, sins simu niko alone ila wazo lilinijia paap
 
Bora umetoka salama maana sipati picha mlango umejifunga hivyo afu humo bafuni akatokea mjusi,mende au panya nadhani leo usingeweza kuandika hapa
Hivyo siogopii angetokea nyoka ningezimia
 
Acha mama ile siku ndio nilijua mi ni mwanaume kweli embu fikiria mizoga ya panya imenizingira,joto Kali niko na boksa tu ile harufu ya chakula cha kitimoto, sins simu niko alone ila wazo lilinijia paap
Pole sana aisee,mi kidogo nilie
 
Usiombe itokee siku either lift ime fail,umepotea msituni,au umejilock alone halafu hakuna msaada
Hapo ndio utajua nobody cares about yourself unless you!
 
Sina hamu na kila kitu hapa ,,ni hivi nilikuwa nafanya usafi chumbani kwangu na kupanga kila kitu ila kuondoa vumbi nimemaliza nikawa nafanya usafi nyumba yote sasa hapo nawaza nikaangalie movie (mission impossible fallout)

nikamaliza kila kitu kikawa mahala pale,kuja kuangalia muda nikawa nimechelewa hiyo movie nikaona kuna muda mwingine ambayo ni saa 1 jioni hii nikasema fresh haina shida ntaenda muda huo ,G wangu akapiga simu tukaanza kuongea weeee tukajipa break maana yupo kazini, si nikasema niende kuoga nimeingia hivi nikaubamiza mlango nikaendelea kuoga ...

Kasheshe likaanza nataka nifungue mlango mamamaweee mlango haufunguki ,vuta vuta wapiiii nikaanza kuuvuta kwa chini hakuna ,,nikashika kitasa nikavuta wapii, nikaona nitoe taulo nitupe pembeni nikaona linanibana ,nimehangaika nyie niko peke yangu nyumba nzima mlango wa sebuleni nimeufunga kwa ndani,,nikawaza sasa hapa hata nikichungulia kwenye dirisha la bafuni nikaita mtu atapitaje wakati sebuleni kule nimefunga mlango ,nikakaa kwenye sinki nimekaa machozi kama yanataka kunitoka maana nimefanya vyote havijanisaidia ,,nikawaza jamani nani sasa atanisaidia simu zipo chumbani tena nimeacha zinalia muziki wa baila ,jamani nikainuka tena nikaanza kuvuta kitasa (nikaanza kupatia picha kama kwenye movie mtu akibomoa mlango)nikapiga teke wapii kumbuka hapo nipo uchi huku narusha mateke kuupiga mlango lakin holaaa.,
Nikajisemea alieniambia nije kuoga nanii jamani au uchawi huu,,kumbuka hapo nishaubamiza mlango kwa mateke na kuusukuma kwa nguvu ,kuvuta kitasa kikang'oka nikasema leo ni leo !!!!!!!![emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22] hiii nikaweka taulo chini nikalikalia kabisa nikaanza kuwafikiria watu ninaowajua wangekuwa karibu wangenisaidia ,nimepata tabu leo ,

Nikasema sasa hapa nimeng'oa kitasa nafanyaje sasa nikanyanyuka tena piga teke ,sukuma ,bamiza mpaka mwili ukatoa jasho baadae nikaona nichukue kile kitasa pale pa kushikia nikapageuza ili nianze kung'oa kiubao kilikuwa kimeshikiwa pale kwenye eneo la kitasa bahati nzuri nikaweza kuving'oa baadhi nikaanza kuchokonoa mlango ukafunguka nikapumuua kwa nguvuu nikajimwagia maji halaf nikatoka ,sina hamu nako kabisa nimejilaza hapa nasubiria ifike saa 12 na nusu niondoke zangu nikazurure mall ...
Hapa mwili unanitetemeka ,vidole vimekosa nguvu ,miguu imechoka yaan nimefanya zoezi kwa lazima..

Basi bana ndio tabu ilonikuta muda si mrefu jamani hebu patia picha usingefunguka ingekuwaje G yupo mbali ningefanyaje majirani wasingenisikia kabisa labda wapita njia ambao siwafahamu

Jioni njema
Naomba kuuliza choo ni cha public yaani cha ndani lkn ni public Fulani hivi , au ,ulikua master bedroom? Km master bedroom mlango wa nn si unaweka plastic nyepesi ( cjui nimeeleweka)
 
Mawazo yangu yameenda mbali sana ningali nasoma hii kadhia. Nilianza kufikiri na kutafakari siku roho ya binadamu i napoanza kutoka kuwa unakuwa huwezi pata msaada hata kwa mtu yyte ni kila mtu na mola wake.
 
Back
Top Bottom