Hahahaaa!
Uzuri ni kwamba mtaendelea kubaki kuwa mashuhuda tu wa jinsi CCM ilivyo kubwa na isiyoyumbishwa........inajisahihisha dakika hiyohiyo ikipatwa na hitilafu Huku mtiahitilafu akiwajibishwa dakika hiyo hiyo. Hilo halipo kwa chama kingine chochote. Mpaka Sasa ikiwa ni siku ya nne; vyama vyote, social media zooote, watu woooote habari ni za ujio tu wa makamu mpya wa Raisi..........huo ndo unaitwa ukubwa! Mpaka waliopo mahakamani wanasahau yao kwa muda huko mahakamani na kuzungumzia habari hii ya ccm.
Mtu aliyetisha kwa ukubwa, mtandao, uwezo na kujiamini alitoka ccm na kukabidhiwa kwa wapinzani..........ccm ikaendelea kuwa imara na jamaa akaona ukubwa wa ccm akarudi mbio mbio. Huo ndiyo ukubwa
Huko upinzani Kuna mtu analalamikiwa mwaka wa 20 Sasa🤣🤣🤣, lakini Cha kufanya mpaka Sasa hawajakipata....huo unaitwa udogo/uchanga. Kazi yao kuuubwa iliyobaki ni kuanzisha ,Amina ya nyuzi tu za kuzungumzia ccm Huku CCM ikifanya yake.
Ndiyo, upo sahihi; mtashuhudia mengi mno Hadi kufikia 2030 na mtaendelea kuipata CCM imara (iliyoboreshwa) daima dumu☺️☺️☺️. Karibuni!!🙏🙏🙏