Yanayoendelea Dodoma bunge la katiba

Yanayoendelea Dodoma bunge la katiba

Sasa Simiyu Yetu umefikaje kwenye vikao vya Bunge la Katiba? Kweli kazi tunayo? Kuna sababu zozote zimetolewa juu ya ucheleweshwaji wa rasimu ya kanuni ambazo mlipaswa kuanza kuzijadili leo? Or it doesn't matter as long as members are paid their allowances in full?

Na kwa jinsi nchi yetu ilivyo na bahati mbaya, unaweza kukuta Simiyu Yetu ni Waziri. Ee mola epushia mbali.
 
Hawatengenezi katiba. Hilo naliita kusanyiko linalopika viashilia vya machafuko ktk jamii. They better evacuate from there if their intension was to grab the whole sum amount budgeted as "a just in case"
We expect nothing meaningful aftr the said 90 days.

Naam, na ndivyo itakavyokuwa hilo kusanyiko litatuletea machafuko Tanzania badala ya katiba mpya km hawatakuwa makini. Nasikia wametunga kanuni za kuendesha bunge lenyewe kwa siri bila kuwa live. Lengo ni nini?
 
Ni siku ya jumatatu siku ambayo tulitarajia kuanza rasmi kujadili kanuni za bunge maalumu lakini zoezi hilo halitafanyika badala yake tunaendelea kujisomea kanuni kwa siku ya leo hata kesho.

yawezekana kuanzia jumatano ndiyo siku ambayo tunaweza kuanza kujadili kanuni husika ili kuweza kuzipitisha tayari kwa kuanza kutuongoza kwenye hili bunge maalumu la kuandaa katiba ya watanzania.
Mnajadili nini na wakati ccm imeshatoa maamuzi yake?hapo hakuna katiba mpya tena mmeamua kumpuuza kikwete na ndoto yake ya katiba mpya
 
Unapobeba mZigo unakuwa na Malengo yako ya kwamba unaubeba mZigo kuu peleka wapi na unaenda kufanya ila nini baada ya kufika sehemu husika! Na huo mZigo ni waaina gani.
Watanzania tulitangaziwa Mizigo yetu ambayo ni wananchi Wenzetu waliopata Bahati ya Kuwa viongozi katika jamii yetu, Mizigo hii ni kati ya Wenzetu ambao kwa mjibu wa Sheriayetu inayosimamia mchakato wa kutunga katiba mpya tumewapa waamue na kupitisha katiba hiyo na kuna fununu Kuwa rais aliamua kuongeza Mizigo mingine ikasaidiane kupitisha katiba hiyo. Lililo wazi ni Kuwa Mizigo hiyo tumebebeshwa na raisi na inaenda kutoa katiba mZigo zaidi.

matokeo ya mtihani wa kidatu cha nne yameakisi Mizigo hii.
ni lini tutaondokana na Mizigo hii?
 
Ndugu wana JF,
ninaomba kama kuna mwenye taarifa ya kinachojiri kwenye bunge la katiba atujuze kwani tuko mbali na radio pamoja na tv,
Asanteni kwa msaada wenu

Nani kakwambia kuwa Bunge la Katiba linarushwa hewani na Radio au TV???
 
Back
Top Bottom