Yanayoendelea Dodoma bunge la katiba

Sasa Simiyu Yetu umefikaje kwenye vikao vya Bunge la Katiba? Kweli kazi tunayo? Kuna sababu zozote zimetolewa juu ya ucheleweshwaji wa rasimu ya kanuni ambazo mlipaswa kuanza kuzijadili leo? Or it doesn't matter as long as members are paid their allowances in full?

Na kwa jinsi nchi yetu ilivyo na bahati mbaya, unaweza kukuta Simiyu Yetu ni Waziri. Ee mola epushia mbali.
 

Naam, na ndivyo itakavyokuwa hilo kusanyiko litatuletea machafuko Tanzania badala ya katiba mpya km hawatakuwa makini. Nasikia wametunga kanuni za kuendesha bunge lenyewe kwa siri bila kuwa live. Lengo ni nini?
 
Mnajadili nini na wakati ccm imeshatoa maamuzi yake?hapo hakuna katiba mpya tena mmeamua kumpuuza kikwete na ndoto yake ya katiba mpya
 
Unapobeba mZigo unakuwa na Malengo yako ya kwamba unaubeba mZigo kuu peleka wapi na unaenda kufanya ila nini baada ya kufika sehemu husika! Na huo mZigo ni waaina gani.
Watanzania tulitangaziwa Mizigo yetu ambayo ni wananchi Wenzetu waliopata Bahati ya Kuwa viongozi katika jamii yetu, Mizigo hii ni kati ya Wenzetu ambao kwa mjibu wa Sheriayetu inayosimamia mchakato wa kutunga katiba mpya tumewapa waamue na kupitisha katiba hiyo na kuna fununu Kuwa rais aliamua kuongeza Mizigo mingine ikasaidiane kupitisha katiba hiyo. Lililo wazi ni Kuwa Mizigo hiyo tumebebeshwa na raisi na inaenda kutoa katiba mZigo zaidi.

matokeo ya mtihani wa kidatu cha nne yameakisi Mizigo hii.
ni lini tutaondokana na Mizigo hii?
 
Ndugu wana JF,
ninaomba kama kuna mwenye taarifa ya kinachojiri kwenye bunge la katiba atujuze kwani tuko mbali na radio pamoja na tv,
Asanteni kwa msaada wenu

Nani kakwambia kuwa Bunge la Katiba linarushwa hewani na Radio au TV???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…