Yanayoendelea Enduleni Ngorongoro si haki. Sauti zipazwe

Mambo ya ajabu sana, kiongozi unasamini wawekezaji kuliko raia unaowaongoza? Na cha kushangaza huo uwekezaji haujawahi kuwa na tija yeyote kwa nchi. Mambo ya kijinga sana.
 
Kenya walikuwa na matatizo kama haya na walipata solution.

Lakini hawa wetu wanatutawala kama Wakoloni.
Utakuwa unawasingizia! Unafikiri kama Wakoloni wangekawia kuipa Tanganyika uhuru, tuseme wangeuchelewesha hadi 2005, hali ya Tanganyika ingekuwaje kwa sasa? Hayo maswaibu yangekuwepo?
 
Samia anatumia nguvu nyingi sana kuficha uvundo wa Ngorongoro.

Hivi nani anamshauri afanye haya mambo? au kajizungushia Machawa matupu?

Samia jua kuwa Wahenga walishasema kuwa "lakuvunda halina ubani"
 
Au hizi tetesi za Ngorongoro crater kuuzwa kwa Mwanamfalme wa Sharjah zina ukweli?

Mbona Mapolisi kama wote wamehamishiwa huko? Kwanini wanamzuia Lissu kufanya mkutano wa hadhara Karatu.

Au Wamang'ati Wairaqwi na Wamassai wako chini ya Martial law.?

Maswali ni mengi mengi kweli kweli hadi kichwa kinauma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…