Yanayoendelea katika uwanja wa uhuru katika kuaga mwili wa Rais Magufuli

Yanayoendelea katika uwanja wa uhuru katika kuaga mwili wa Rais Magufuli

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Wakazi wa Dar wamefurika Uwanja wa Uhuru kumuaga Hayati Rais Magufuli ambapo Saa 11, mwili utasafirishwa kuelekea Dodoma.

Kutokana na wingi wa watu Mkuu wa Mkoa wa Dar, Abubakar Kunenge amewaomba wale ambao wanataka kumuaga Rais Magufuli lakini hawataweza kufanikiwa kufika uwanja wa Uhuru, wajipange barabarani.

Sababu ni kuwa hawataweza kuingia na mwili utakuwa unaanza safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere tayari kwa kusafirishwa kwenda Dodoma
==
MWILI WA RAIS MAGUFULI WAZUNGUSHWA MARA 6, ILI WALIOSHINDA KUAGA WAPUNGE MIKONO

Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli ambalo limefanyika kwa siku mbili katika Uwanja wa Uhuru, limesitishwa kutokana na wingi wa watu

Ili kuheshimu kila aliyehudhuria mwili umezungushwa katika uwanja mara sita ili kila aliyekwenda apunge mkono, Ishara ya kumuaga Rais Magufuli

Saa kumi na moja Mwili wa Magufuli unatarajia kusafirishwa kwenda Dodoma kwa ndege. Viongozi kama Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tayari wapo Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili wa Rais
 
Tundu Antipasi Lissu amehoji kutembezwa kwa mwili wa Hayati Magufuli kuagwa kwa heshima wakati ati ugonjwa wake ulifichwa (ona kiambatanisho)!

Screenshot_20210321-160105_Twitter.jpg

Je, yuko sahihi au Hayati Magufuli anastahili heshima kubwa zaidi kama inavyoelezwa kwenye Video clip - kiambatanisho?
 
Lissu anataka kutochonganisha watanzania
Afadhali huyo Lisu ni muwazi sana na ndiye aliyetujuza kuwa Rais wetu anaumwa.

Mbona Ikulu haikusema mapema ili tumuombee. Kuaga gani huku kwa wiki nzima, mbona Nyerere na Mkapa haikuwa hivi?
 
Hapa nipo mitaa ya chako ni chako dodoma nasubiri muda si mrefu watampitisha.

Sio nilimpenda nataka japo nione akiondoka!

Nitakachomiss sana kwa mwendazake ni uongo wa waziwazi halafu mkavuu!

Eti sadam husen raisi wa kuwait!
 
Hapa ndo nimefika hapa Mikese, nakaribia mizani. Pale Uhuru nimechemka kabisa na sikuridhika ile tunazungushiwa mwili kama marathon na nilikuwa far. Hapa nakanyaga mpk Dodoma. Lazima nimuone huyu mzee as last time nilimuona pale TMA. He was my hero as individual man no matter how tulitofautiana in few matters.

Chatoooo....rest easy Mzalendo halisi.
 
Jiangalie tu na ww usije agwa after few days..

Mnyama COVID yupo around..
 
Hapa ndo nimefika hapa Mikese, nakaribia mizani. Pale Uhuru nimechemka kabisa na sikuridhika ile tunazungushiwa mwili kama marathon na nilikuwa far. Hapa nakanyaga mpk Dodoma. Lazima nimuone huyu mzee as last time nilimuona pale TMA. He was my hero as individual man no matter how tulitofautiana in few matters.

Chatoooo....rest easy Mzalendo halisi.
Mie nimeshindwa muaga pia, nimefanya juhudi hapa dar imeshindikana. Sababu ya lile nyomi, nimefika saa tatu uwanjani mpaka saa nane hamna dalili watu ni wengi foleni haziendi, hivyo MUNGU AMLAZE JEMEDARI WETU MAHALI PEMA KABISA PEPONI...
 
Back
Top Bottom