Yanayoendelea kwenye migodi yetu ni ya kusikitisha kwa wachimbaji wadogo

Yanayoendelea kwenye migodi yetu ni ya kusikitisha kwa wachimbaji wadogo

mmsmo

Member
Joined
Oct 11, 2021
Posts
5
Reaction score
11
"Haya madini hayaozi yaacheni siku watu wetu wakiamka na kutambua jinsi ya kuyachimba watayachimba". Hiyo ni kauli ya hayati Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kiongozi aliyetanguliza maslahi ya taifa lake na kizazi cha Taifa.

Leo yanayoendelea kwenye migodi yetu ni ya kusikitisha. Mchimbaji mdogo siku zote ndiyo huwa mgunduzi wa madini yapo wapi yakishapatikana anakuja bepari kwa jina la mwekezaji anahodhi maeneo ya huyo mchimbaji mdogo.

Huyu mchimbaji anageuka mkimbizi na mtazamaji wa rasilimali ya nchi yake. Mchina amehodhi maeneo ya wachimbaji wadogo na yeye akichimba kama mchimbaji mdogo. Kile kinachoendelea kariakoo ndicho kinachoendelea porini mchina kachukua kila kitu kwa mgongo wa mwenyeji mwenye leseni ya utafiti au mmiliki wa eneo.

Ajira hatoi, kazi ambazo mwenyeji anaweza kuzifanya zote wanafanya wenyewe(wachina). Ukifuatilia baada ya serikali kuweka mineral center(masoko ya madini) ya kununua na kuuza madini katika takwimu za kodi wachimbaji wadogo wanaingizia mapato makubwa sana kwa upande wa kodi ukilinganisha na huyo anaeitwa mwekezaji.

Wenye mamlaka mtazameni kwa ukaribu sana huyu mzawa ambae ni mchimbaji mdogo. Mwezesheni kwa sababu kila atakachozalisha kitatumika humu humu ndani na kitawafikia wengi. Haya mambo ya kutegemea gawiwo baada ya mwekezaji kutoa gharama zake ambazo mara nyingi huongezwa sifuri nyingi kama Taifa tunapoteza sana.

Au mwekezaji kujenga shule, hospital au barabara ni ulaghai hivi mtu kavuna madini ya mabilioni anakujengea jengo moja la hospital au shule au barabara ya kiwango cha changarawe ambavyo vyote vinaweza kugharimu bilioni 3 au hata 5 wakati huo mwenzako(mwekezaji) amevuna bilioni 200 au mpaka trilioni 1 kwa hapo nani anaepoteza?

Nguvu Ile ile inayotumika kumlinda na kumwezesha mwekezaji afanikishe kazi yake pia nguvu hiyohiyo inatakiwa kutumika kumwezesha mchimbaji mdogo kwa sababu huyu ni mtoto wa nyumbani vyote vinavyopatikana atagawana na wa nyumbani.
 
Back
Top Bottom