Yanayoendelea wilayani Songwe kwenye ujenzi wa madarasa kutokana na pesa za Covid. Ni hatari tupu pesa zimeliwa

Yanayoendelea wilayani Songwe kwenye ujenzi wa madarasa kutokana na pesa za Covid. Ni hatari tupu pesa zimeliwa

Songwe Yetu

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
84
Reaction score
99
Kwa heshima na taadhima ujumbe huu mhe: Rais ukufikikie popote uliopo.Mhe Raisi umekuwa mstari mbele kuhakikisha Nchi yetu inakuwa salama na tunapata maendeleo katika nyanja mbalimbali. Na umefanya jitihada za dhati kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele.Lakini watendaji wako wanakuangusha nilikkuwa kwenye msafara wa ukaguzi wa majengo ya pesa ya Covid yaani vituko zaidi ya vituko.Kwanza nilichogundua watumishi wa kitanzania wengi sio wazalendo. Nasema hayo kwa sababu zifuatazo.

1.kwanza walisema ujenzi umekamilika wakabumba taarifa wakapeleka tamisemi tamisemi wakakubali kweli ujenzi umekamilika bila kujiridhisha wakati ujenzi bado unaendelea.

2.majengo yaliojengwa karibia wilaya nzima tulipopita yako chini ya kiwango ina maaana sasa serikali inatakiwa kutuma pesa za ukarabati ili majengo yakarabatiwe. Hata kabla hsyajaanza kutumika nina picha nitaziweka hapa.
3Majengo mengi yamejengwa bila msingi imara na hivyo kusababisha mengi kukatika kuna moja nimeona lenta nzima ya jengo imekatika na imetoa nyufa lakini ujenzi wakauendeleza hivyo.

4.Upigaji mkubwa umefanyika kwenye madirisha. Wameyaegesha nayamelegea yako taaabani kabla hayajaanza kutumika. Na uenda hali ikawa mbaya sana yatakapoanza kutumika.

5.Madawati yalioletwa ni balaaa ni mabovu hayajapigwa msasa na misumali iko nje. Pia inaweza kuwadhuru watoto. Wakuu wa shule walichojali kutafuta mafundi ambao watahitaji hela kidogo hili wenyewe wapata za kutosha mlo.
6.Rangi na matilio yaliotumika hayafai yako chini ya kiwango.

Chenji iliobaki kwenye ujenzi wameambiwa waitafutie matimizi.

7.Mwisho kabisa baada ya kufanya madudu haya wale wasimamizi wakuu wakaomba kuhama kwenye vituovyao na kuhamia katika vituovipya ili kuwaachia msala hawa wapya waliokuja.

Serikali iwashughulikie wote walioofanya madudu katika miradi hiii either kwa kuwashusha vyeo na kuwawajibisha katika nafasi zao.

Haiwezekani majengo yana nyufa na mengine lenta imekatika lakini wakajifanya hawaoni na wakaendelea kujenga. Serikali ianze na injinia wa wilaya kwanza vinginevyo mchezo huu utaendelea. Nitoe Rai tu kwa watu walioaminiwa katika serika yetu kuipenda nchi yetu na kuwa waadilifu.

Rais wetu anahangaika huku na kule kuhakikisha Nchi inapata maendeleo tusimwangushe.Inno Bashe na prof Mkenda shugulikeni nawatu hawa ambao wanaomuhujumu Rais.Tanzania ni yetu Sote.

Pia maafisa utumishi wa wa wilaya hii ni wanapenda rushwa kila kitu mpaka uwape rushwa. Hawafanyi kazi yako mpaka uwape kitu kidogo.
Kuna sekondari moja madawati mabovu jengo limekatika madirisha ya alluminium mabovu ipo maeneo ya muheza hatukulipokea ubabishaji kwenye maeneo ya ratio ya sement pia ni wakubabatiza.
Kuna sehemu moja maweni kafanya ila kwenye finishing ya madirisha na madawati kavuvurunda.
Sume hali ni mbaya zaidi hapaeleweki.
Manda ujenzi unaendelea lakini wameandika taarifa kwamba wamemaliza na wameshakabidhi.
Magamba sooon madarasa mapya yataaanguka. MORE UPDATES TO COME
 
Kama unaweza wasiliana na Innocent Bashungwa itapendeza zaidi,ndio mwenye Jukumu hilo.

Pili Naibu Waziri Silinde huo ndio Mkoa wake na yeye ndio Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu.
 
Ujumbe huu uwafikie kamati ya siasa ya CCM ya Wilaya ya Songwe. Dc wa wilaya ya Songwe upo?
 
Kwa urefu wa kamba zao yaani, pesa kibindoni
 
Alafu traffic kukusanya buku 2 watu mnapiga kelele

Ova
 

Ujumbe huu uwafikie kamati ya siasa ya CCM ya Wilaya ya Songwe. Dc wa wilaya ya Songwe upo?​

Wakwanza kubeba lawama ni TAMISEMI chini ya UMMY MWALIMU kwa sababu

1. Kwanza wamelazimisha ujenzi kuisha ndani ya mwezi mmoja kitu ambacho kina hatarisha usalama na ubora wa majengo

2.kuhusu viti halmashauri nyingi zililazimisha viti 50 na meza 50 kwa darasa wakati budget ya serikali ilikuwa ni viti 40 kwa kila darasa hii ilisababisha viti vingi kutengenezwa chini ya kiwango ili kukidhi idadi hiyo

3.mafundi walilazimishwa kufanya kazi hadi usiku wa manane huku wakitishiwa na wengine kuwekwa ndani bila sabababu

4. Kuna baadhi ya halmashauri zilichukua tenda ya kununua vifaa vya ujenz kama cement , mabati, nondo , misumari nk hali iliyo iliyo pelekea kulazimisha vifaa walivyo pelekwa vitoshe hata kama havitoshi

Yapo mengi sana yatakayo sababisha majengo hayo ya kisiasa kuwa chini ya kiwango na sio majengo tu bali hata hivyo viti na meza vingi vipo chini kabisa ya kiwango kwa sababu wanasiasa ndio wamekuwa ma engineer wakati hawqjui hata kanununi na taratibu na hatua za ujenzi.
 
Ila kwa miaka mingi Mbozi huwa inaongoza kwa hati chafu, yaani ni ka utamaduni flani hivi, Utasikia mabwawa ya maji hewa, nguzo za umeme hewa, madaraja hewa, hapo Kati walimwogopa kidogo Hayati, Sasa wamerudi kulekule
 
Ila kwa miaka mingi Mbozi huwa inaongoza kwa hati chafu, yaani ni ka utamaduni flani hivi, Utasikia mabwawa ya maji hewa, nguzo za umeme hewa, madaraja hewa, hapo Kati walimwogopa kidogo Hayati, Sasa wamerudi kulekule
Kuna kiongozi mmoja kakimbia
 
Back
Top Bottom