Wanabodi,
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa hili Bunge Maalum kupitia TV kuanzia fixed, portable na mobile. Pia nashukuru kila niendapo kwenye TV hukuta wakiangalia au TBC au Star TV, hivyo sipitwi, na hadi Isidingo na Taarifa ya habari ya saa mbili usiku, ITV, nimeitoa sadaka!.
Naomba kwanza kumpongeza kwa dhati kabisa toka ndani ya moyo wangu, huyu Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hili Mhe. Pandu Ameir Kificho, kwa umahiri, ustaarabu, uvumilivu, ustahimilivu, uungwana, upole, usikivu, na weledi wa hali ya juu sana, na hadi leo kuliahirisha bunge, ameliahirisha ili kuepusha shari!. Kwa yote haya Kificho anastahili pongezi!.
Ila pia sifa hizi nzuri, umahiri, ustaarabu, uvumilivu, ustahimilivu, uungwana, upole, usikivu, na weledi wa hali ya juu zikizidi na kupitiza viwango vya kawaida zinageuka ni udhaifu.
Umahiri ukizidi sana kwa watu wajinga wajinga, watakuona hufai, mule bungeni, kuna wajinga wajinga kibao!.
Ustaarabu ukizidi sana kwa watu washenzi watakuona huna maana, mule bungeni kuna washenzi washenzi kibao!.
Uvumilivu ukizidi sana kwa watu wenye papara, watakuona dhaifu hivyo kuongeza fujo.
Ustahimilivu ukizidi sana hadi kustahilia visivyostahilika, utaishiwa kudhihakiwa!.
Uungwana ukizidi sana kwa wapenda shari, utaishia kufanyiwa fujo!.
Upole ukizidi sana kwa watu wenye mzuka, watakupanda kichwani!
Usikivu ukizidi sana kwa kila mwenye kelele, bunge linaishia kugeuka zogo
Weledi ukizidi sana kwa waliozoea kuburutwa, au kuswaga, wataishia kukusambaratisha!.
Yote hayo yamefanywa na Mhe. Pandu Ameir Kificho kwa kuzingania nia njema tuu kwa kuzingatia bunge hili maalum ni jipya, halina kanuni zozote, hivyo analiendesha kwa kuzingatia uzoefu na ndia maana amerhusu kila kitu kulikopelekea kikao cha leo kumshinda na kuliahirisha bunge kuepushsa shari!.
Jee kwa jinsi Mhe. Pandu Ameir Kificho anavyoliendesha Bunge hili Maalum, anastahili pongezi a lawama kwa kupitiliza?
Pasco.