Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Kwa mjumbe makini asingeandika hivi maana kama naye sio miongoni mwao basi inampasa atuonyeshe sisi na wao njia. Mkuu Imma Saro, bora sasa unamuona huyu bwana rangi zake halisi.
Lakini pia huyu 'rais mtarajiwa' naye kaandika ifuatayo:
When your seat is plastered with nation's court-of-arms, and your carpet has national flag colours, you lose the right to act stupid.
Sasa ni wazi hili linageuka kuwa taifa la majuha!
 
Nimekaa kimya nikiwatazama wachangiaji na malengo yao nini hasa,kwani wanapoteza mda na kodi za wananchi.
Ifikie wakati wajitambue wapo kule kwa ajili ya nini na ni kwa nini,na kwa faida ya nani, wanaharibu hali ya hewa ya nchi pasipo wao kujua,pia wajue kuongea kwingi sio kujua sana.
Kosa lilofanyika ni serikali kutoleta muswada ambao ungekuwa na sharti la kuhakikisha wanamaliza kutengeneza katiba ndani ya siku 70...wakizidisha siku wajigharamie wenyewe....mpaka katiba ipatikane. Hii ingewasaidia kuwajibika zaidi kwa wakati....wala kusinge kuwa na upuuzi huu.
 
Zitto Z Kabwe"@Tanganyikan: Nashukuru Mungu nimeacha kufuatilia ‪#‎BungeKatiba‬hadi huu upuuzi wa kanuni uishe." +1
Mh Zitto Kabwe Mbunge wa mahakama anaandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa FB Facebook; hii ni hatari sana sasa jiulize kusema wanaojadili hizo kanuni ni wapuuzi? ukishiriki na wenye dhambi na wewe umiongoni mwao,swala la Zitto kama kanuni ndio zinakuwa sheria za kuliongoza bunge iweje ushishiriki kuanda kanuni?
Hii sio kwa mara ya kwanza Mh Zitto kuwaita watu wa wapuuzi,Kwa kijana kama yeye alipaswa kutumia hekima zake katika kujenga hoja na sio kukimbia tatizo kukimbia tatizo hujakwepa kitu,Ukishindwa kutatuwa tatizo basi na ww ni sehemu ya tatizo;
Leo unaita mjadala wa kipuuuzi sasa likianza rasimi utawaiteje;Usilewe sifa za kijinga;
Eti ndio mzalendo na posho anapokeal;'

Yeye mwenyewe Zitto ni mpuuzi
 
Last edited by a moderator:
Ni wazo zuri sana. Ningekuwa mimi ndiye Mh. kikwete, ningevunja Bunge lote la Katiba na kisha kuliunda lingine kupitia kura za wananchi. Hawa wabunge wote wa sasa wasingeruhusiwa kugombea! (Pesa/gharama katika nchi hii siyo kigezo kwani BOT zimejaa hadi watu wanazipeleka nje kuzihifadhi kwavile hakuna nafasi ya kuziweka hapa TZ!)
 
Olesendeka hanaga nidhamu, alafu huwa anajifanya mjuaji sana
 
Mh. Kificho yuko juu Mkuu; ni bahati mbaya kwamba hakubahatika kupiga sana kitabu. Ila kile kichwa, pamoja na kukosa shahada and yet kiko vizuri vile, sijui kingepata PhD ingekuwaje? Mzee yuko vizuri sana; pamoja na kuwa member wa magamba lakini hapendi kujitoa ufahamu kama majuha wengine waliojazana humo. Angekuwepo madam wa mjengoni kwetu pale nadhani ingekuwa vituko. Ha ha ha!
 
Ndugu zangu,
Watanzania leo tunavuta pumzi huku tukielekeza
macho na masikio yetu katikati kabisa ya nchi
yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Ni Dodoma.
Huko itapatikana leo hatma ya mwelekeo wa
mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya
Nchi Yetu.
Hata hivyo, kuna ishara mbaya kuwa
tuliowatuma Dodoma wako katika hatari ya
kukwamisha mchakato mzima kwa kujikita
kwenye kupigania kisicho na maslahi ya nchi hii
kwa miaka 50 au 100 ijayo.
Watapigania yaliyomo kwenye vifungu vya 36
mpaka 37 za Kanuni za kuendesha Bunge hilo
Maalum. Inahusu namna watakavyofikia
maamuzi, kuwa iwe ni kwa kura za faragha au
dhahiri. Ndio, inahusu kura za siri au kura za
wazi. Ni' vifungu vya kifo' maana ndivyo
vitakavyoamua, kwa namna moja au nyingine,
uhai wa mchakato mzima wa kuitafuta Katiba.
Tuliowatuma Dodoma wamejigawa katika
makundi ya ' Sisi' na ' Wao'. Wanatafuta
kushindana na kupata mshindi badala ya kutafuta
muafaka wa Kitaifa. Na hakika, kama alivyopata
kusema Rais wa Nchi, Jakaya Kikwete, kuwa
kwenye kushindana huko hakuna atakayeshinda.
Tutashindwa Sote. Na huo ndio UKWELI.
Hakika, huu ni mtihani mgumu ulio mbele yao
tuliowatuma Dodoma. Wakishindwa mtihani huu,
basi, ishara zinazoonekana ni za mkwamo wa
jumla wa mchakato mzima. NI AIBU.
Tuliowatuma Dodoma hawajachelewa kuitafuta
hekima na busara kutunusuru na aibu kubwa ya
taifa iliyo mbele yetu. Tuliowatuma Dodoma
wawafikirie pia watoto wa kesho na wa vizazi
vijavyo katika nchi yetu tuliyozaliwa na
tunayoipenda.
Na ushauri hapa ni heri kukubaliana
kutokubaliana, na hivyo, kusitisha kwa muda
mchakato huo, kuliko kulazimisha kwenda
mbele. Ni ushauri pia, kuwa ni heri kuyatafuta
maridhiano kwanza kabla ya kuingia kwenye
majadiliano, kuliko kuyatafuta maridhiano baada
ya kuingia kwenye mapigano na kujeruhiana. Ni
busara basi, tuliowatuma Dodoma wakaunda
Kamati Maalum ya kuyatafuta maridhiano wa
vifungu hivyo. Na ifahamike, kuwa MARIDHIANO
ndio msingi wa UHALALI wa mchakato na hata
Katiba yenyewe.
Tusipotanguliza busara, hekima na maslahi ya
taifa, yumkini yaweza ikawa kama yale aliyopata
kuyasema miaka 60 iliyopita, mwandishi yule
mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert,
aliandika; ” Wasadikika wana desturi ya kutafuta
fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha
umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya
zamani.
Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani
kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia
katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema
ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta
kifo.
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu.
Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea
faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”-
Shaaban Bin Robert.
 
Mchakato huu umekuwa " hijacked" na ma CCM na hawana hata uwezo wa kueleza jambo likafahamika. Wanatumia ubabe na wingi wao kama tishio. Katiba ni ya wananchi kwa hivo sisi ndio wenye neno la mwisho,
 
wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya mambo ya nchi hii.
Wasifanye mchezo.
Wooooote tunaweza kuwaondoa.
Watanzania wako wengi wengi mno wenye busara na uwezo wa kujadili hayo mambo.
Wasidhani kuwa wao ndio mwisho wa yote.
Hii ni tahadhari tu.
Wajiheshimu nasi wananchi tutawaheshimu.
 
Nami napenda sana kumpa pongezi za dhati mh Kificho kiukweli anajitahidi sana kuwaweka sawa hawa jamaa haswa wengi wenye maoni yanayofanana! ila jambo la muhimu hapa ni kumsubiri mzee wa viwango atakapokalia kiti mwenyewe utaona watu walio na mawazo yanayofanan watakapo nywea kama maji ya baridi ! hakiki SITA watanzania wanakusubiri kwa hamu kubwa kuona uwamuzi wako kwa hawa jamaa!
 
Kama ole sendeka akijenga hoja bunge zima linanuka unafiki mmasai zuzu sana yule
 
Nilishuhudia muumini wa dini fulani akitoa angalisho kuwa wakati wakuapa wale wa mama waliokatika siku zao za mwezi si ruksa!! mambo makubwa bunge la katiba!!


Mwendawazimu kweli huyo! Then akishajua (m)wenzake yuko kwenye siku zake ili iweje? Huu ni udhalilishaji wa waziwazi. Kama itaonekana kuna vizingiti fulani fulani vya kidini, ni afadhali ukatafutwa utaratibu mwingine wa kuapa bila kudhalilisha utu wa wengine.
 
Kosa lilofanyika ni serikali kutoleta muswada ambao ungekuwa na sharti la kuhakikisha wanamaliza kutengeneza katiba ndani ya siku 70...wakizidisha siku wajigharamie wenyewe....mpaka katiba ipatikane. Hii ingewasaidia kuwajibika zaidi kwa wakati....wala kusinge kuwa na upuuzi huu.

Kweli kabisa laiti kama serikali ingeweka sheria ya namna hiyo mambo kama yale yasingefanyika,sasa wameifanya kama the source of income kwa kuzidi kuchezea mda.
 
Ni sawa na baba anayeamua kula hotelini kwa sababu nyumbani kwake jiko limeharibika! Kwa nini asipeleke hizo 'busara' zake bungeni ili upuuzi usipate nafasi?
 
Siyo kauli nzuri kwa mwanasiasa ambaye ndo kwanza chama chake kipya cha hakina hata desk
 
Nami napenda sana kumpa pongezi za dhati mh Kificho kiukweli anajitahidi sana kuwaweka sawa hawa jamaa haswa wengi wenye maoni yanayofanana! ila jambo la muhimu hapa ni kumsubiri mzee wa viwango atakapokalia kiti mwenyewe utaona watu walio na mawazo yanayofanan watakapo nywea kama maji ya baridi ! hakiki SITA watanzania wanakusubiri kwa hamu kubwa kuona uwamuzi wako kwa hawa jamaa!

(i) Hatabiriki
(ii) Ni mnafiki
(iii) Sometimes anababaika kutoa maamuzi

Yetu macho.
 
Mwendawazimu kweli huyo! Then akishajua (m)wenzake yuko kwenye siku zake ili iweje? Huu ni udhalilishaji wa waziwazi. Kama itaonekana kuna vizingiti fulani fulani vya kidini, ni afadhali ukatafutwa utaratibu mwingine wa kuapa bila kudhalilisha utu wa wengine.

Hili bunge naona liko kama halina utaratibu hata wa kusikilizana na kila mtu anakuja na hoja hafifuhafifu na nawasiwasi na kama kuna katiba ya maana hapa. Litakapokuja suala la vipengele vya udini hapo kuna jambo lisilo la kawaida litatokea yetu macho!!
 
Kanuni moja kubwa ambayo Mwenyekiti anatakiwa kuiweka iwe ya wajumbe wajitambulishe kwa utanzania wao 90% ya kutokuelewana itapungua, jingine mtu akienda kinyume cha kanuni adhabu ya kutoka ukumbini itumike au kuomba radhi hapo hapo, Kificho ni mpole lakini anatakiwa kuwa mkali kidogo, nakumbuka 6 kuna wakati Raisi wa jamuhuri alihutubia bungeni , 6 alimwomba awe mkali kidogo, huu upole ndio unaleteleza vitu kwenda nje ya mstari.
 
Back
Top Bottom