Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

hakika ole Sendeka hafai kuwa kiongozi. Ni mpayukaji mno, huwa hawezi kufikiri akishapata 'challenge' kutoka kwa mtu mwingine
huyu jamaa ni janga kama unakumbuka enzi za richmond alipngea maneno ya kumsafisha lowassa akitumia neno ''kaka yangu'' akaja kumalizwa na kilango malachela
 
Wanabodi,

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa hili Bunge Maalum kupitia TV kuanzia fixed, portable na mobile. Pia nashukuru kila niendapo kwenye TV hukuta wakiangalia au TBC au Star TV, hivyo sipitwi, na hadi Isidingo na Taarifa ya habari ya saa mbili usiku, ITV, nimeitoa sadaka!.

Naomba kwanza kumpongeza kwa dhati kabisa toka ndani ya moyo wangu, huyu Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hili Mhe. Pandu Ameir Kificho, kwa umahiri, ustaarabu, uvumilivu, ustahimilivu, uungwana, upole, usikivu, na weledi wa hali ya juu sana, na hadi leo kuliahirisha bunge, ameliahirisha ili kuepusha shari!. Kwa yote haya Kificho anastahili pongezi!.

Ila pia sifa hizi nzuri, umahiri, ustaarabu, uvumilivu, ustahimilivu, uungwana, upole, usikivu, na weledi wa hali ya juu zikizidi na kupitiza viwango vya kawaida zinageuka ni udhaifu.

Umahiri ukizidi sana kwa watu wajinga wajinga, watakuona hufai, mule bungeni, kuna wajinga wajinga kibao!.
Ustaarabu ukizidi sana kwa watu washenzi watakuona huna maana, mule bungeni kuna washenzi washenzi kibao!.
Uvumilivu ukizidi sana kwa watu wenye papara, watakuona dhaifu hivyo kuongeza fujo.
Ustahimilivu ukizidi sana hadi kustahilia visivyostahilika, utaishiwa kudhihakiwa!.
Uungwana ukizidi sana kwa wapenda shari, utaishia kufanyiwa fujo!.
Upole ukizidi sana kwa watu wenye mzuka, watakupanda kichwani!
Usikivu ukizidi sana kwa kila mwenye kelele, bunge linaishia kugeuka zogo
Weledi ukizidi sana kwa waliozoea kuburutwa, au kuswaga, wataishia kukusambaratisha!.

Yote hayo yamefanywa na Mhe. Pandu Ameir Kificho kwa kuzingania nia njema tuu kwa kuzingatia bunge hili maalum ni jipya, halina kanuni zozote, hivyo analiendesha kwa kuzingatia uzoefu na ndia maana amerhusu kila kitu kulikopelekea kikao cha leo kumshinda na kuliahirisha bunge kuepushsa shari!.

Jee kwa jinsi Mhe. Pandu Ameir Kificho anavyoliendesha Bunge hili Maalum, anastahili pongezi a lawama kwa kupitiliza?
Pasco.
 
Acha uvivu wa kufikiri tumia ubongo wako vzr.kjifunza kutmia kutumia mitandao ya kijamii lmekuwa tatzo mpaka tnapa mtope yenu hmu.
 
Miongoni mwa wabunge la katiba atakaye haribu utaratibu wa kupata katiba mpya ni Mh. Ole s.....ka, uchangiaji wake ni wa kibabe babe, siku ya kwanza kabisa alizungumzia uraia wa mmbunge wa chadema, sasa aliyemchagua kuingia bungeni hana akili na pale walikwenda kuchangia uraia wa mtu au ukabila, kwanza yeye ana uhakika gani kama yeye ni mtanzania au mmasai wa kenya????
 
Mimi,Petro Eusebius Mselewa,Msomi wa Sheria,mtanzania mtu mzima mkazi wa Kibaha,Pwani NATAHADHARISHA Wajumbe wote (pamoja na viongozi wao) wa Bunge Maalum la Katiba kwa kusema ifuatavyo:...
...
sawa na sina uhakika kama hawaelewi hivi lakini uende mbali zaidi na kujiuliza kuwa ni kwa nini regimes zilizotangulia ambapo baadhi ya hawa wajumbe walishiriki katika shughuli hizi hizi ni kwa nini hakukuwa na indiscipline kiasi hiki!!?? Just think beyond the next hill.
 
Zitto Z Kabwe“@Tanganyikan: Nashukuru Mungu nimeacha kufuatilia ‪#‎BungeKatiba‬hadi huu upuuzi wa kanuni uishe.” +1
Mh Zitto Kabwe Mbunge wa mahakama anaandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa FB Facebook; hii ni hatari sana sasa jiulize kusema wanaojadili hizo kanuni ni wapuuzi? ukishiriki na wenye dhambi na wewe umiongoni mwao,swala la Zitto kama kanuni ndio zinakuwa sheria za kuliongoza bunge iweje ushishiriki kuanda kanuni?
Hii sio kwa mara ya kwanza Mh Zitto kuwaita watu wa wapuuzi,Kwa kijana kama yeye alipaswa kutumia hekima zake katika kujenga hoja na sio kukimbia tatizo kukimbia tatizo hujakwepa kitu,Ukishindwa kutatuwa tatizo basi na ww ni sehemu ya tatizo;
Leo unaita mjadala wa kipuuuzi sasa likianza rasimi utawaiteje;Usilewe sifa za kijinga;
Eti ndio mzalendo na posho anapokeal;'
 
Kificho anafanya kazi kwenye mazingira magumu sana. Japokuwa wengi wanamuona ni dhaifu, kwangu nampa heshima na pongezi kutokana na sababu zifuatazo
  1. Anafanya kazi bila miongozo yoyote hivyo mara nyingi anatumia busara zake kuamua mambo
  2. anafanya kazi na watu tofauti na wenye tabia tofauti kama Pasco ulivyoainisha hapo juu
  3. anasimamia idadi kubwa ya watu tofauti na ilivyokuwa kwenye baraza la wawakilishi au hata Bunge la Jamhuri ya muungano wa tanzania
  4. Anasimamia watu waliotoka makundi tofauti, wakiwa na hisia tofauti, mitazamo tofauti, ajenda tofauti na malengo tofauti
 
Nashukuru Mungu nimeacha kufuatilia bunge la katiba hadi huu upuuzi wa kanuni uishe.source wall ya zitto

Haya ni maneno yaliyoandikwa na zitto kwenye wall yake ya FB hivi ni kweli bunge maalum linajadili upuuzi kwenye kanuni kama zitto alivyoona tutafakari maneno haya kwa kina na tujadili

Ni zaidi ya upuuzi!
 
sijui ana matatizo gani.........ndo shida ya makabila yenye mila za mtu ukiongea basi hakuna kupingwa matokeo yake ndo haya..........!
 
mim naunga hoja ni wapuuzi kitu kidogo kwanini kikwamishwe miaka 100?just kanuni tu?you spend billions of peoples tax?
 
editoon.jpg
 
Kinachoendelea Bungeni sasa ni Day Light Robbery.., hawa jamaa wanakula jasho letu (Kodi) kwa kutumia muda mwiingiiiii na hakuna cha maana kinachofanyika zaidi ya Time wasting, ningewaelewa ili ku-save pesa zetu wangefanya overtime bila malipo na sio kujipa off days kila kukicha.
 
Binafsi nilikuwa sijawahi kumuona Mh. Pandu Kificho akiongoza mkutano wowote. Kutoka moyoni,hakuna spika mwenye hekima,busara,uvumilivu na upendo niliyewahi kumuona katika umri wangu kama Kificho. Kinachotokea bungeni {utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge} ni malezi ya hovyo {sio ovyo} waliyopata wabunge wetu toka kwa walezi wao. Mnaokataa kataeni habari ndiyo hiyo. Tutegemeeni siku 150 wakiwa bungeni kwa sababu tu ya utovu na ukosefu wa hekima. Nimekuwa nasema elimu na hekima ni vitu tofauti kabisa.

Siku 90 zikiisha posho isitishwe, waendele kufanya vikao bila posho, maana utakuwa ni uzembe wao. Haiwezekani wanahirisha vikao ovyo ovyo. Juzi usiku saa 2 nilisikia wanalalamika njaa inawauma kwahiyo wahahairishe Kikao wakati Mwenyekiti alikuwa anataka waendelee.
 
Nashukuru Mungu nimeacha kufuatilia bunge la katiba hadi huu upuuzi wa kanuni uishe.source wall ya zitto

Haya ni maneno yaliyoandikwa na zitto kwenye wall yake ya FB hivi ni kweli bunge maalum linajadili upuuzi kwenye kanuni kama zitto alivyoona tutafakari maneno haya kwa kina na tujadili
Sasa wewe ndg yangu zitto.wewe si kibaraka wa ccm?tunakujua usijisumbue kufuatilia kanuni kwa sababu hata bungeni hukai.wewe ni misele tu.habari nilizonazo uko nairobi.je huoni kuwa wewe ni janga?
 
Nilishuhudia muumini wa dini fulani akitoa angalisho kuwa wakati wakuapa wale wa mama waliokatika siku zao za mwezi si ruksa!! mambo makubwa bunge la katiba!!
 
Sendeka ni kirusi cha mafua ya ndege akichangia watu wanavaa mask hata lusinde
 
Back
Top Bottom