Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yaelekea kiti cha Mwenyekiti kinaanza kumuelemea
 
Sendeka -------- wewe..nimesikia mjumbe akimtukana sendeka..wito kwa wajumbe nidhamu ni muhimu wajumbe

Hata mimi cjafurahishwa na hayo matusi lakini vipi mbona hujakikemea alichokiongea Sendeka kwa mjumbe mwenzie?
 
Yaani hao kwa kuchambana ndio wenyewe, mie jana namsikia watu wanazungumza na vipaza sauti vyao viko wazi vinaingiliana hadi sisi kwenye tv tunasikia mwingine alikuwa anahadithiana habari za jana yake, wengine watoto wao uko nyumbani waivyokuwa wasumbufu, mwingine ndio anaongea kwa sauti tumekuchoka anamwambia mbunge mwenzie anayepayuka kuchangia yaani kama kilabu cha pombe hawana hata aibu. utafikili vyuzi zao zimekatika naona mitambo ile inawatoa akili ovyo kabisa kichefuchefu tena mie naona hata aibu kulingalia.
 
Binafsi nilikuwa sijawahi kumuona Mh. Pandu Kificho akiongoza mkutano wowote. Kutoka moyoni,hakuna spika mwenye hekima,busara,uvumilivu na upendo niliyewahi kumuona katika umri wangu kama Kificho. Kinachotokea bungeni {utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge} ni malezi ya hovyo {sio ovyo} waliyopata wabunge wetu toka kwa walezi wao. Mnaokataa kataeni habari ndiyo hiyo. Tutegemeeni siku 150 wakiwa bungeni kwa sababu tu ya utovu na ukosefu wa hekima. Nimekuwa nasema elimu na hekima ni vitu tofauti kabisa.
 
Mjumbe akataa kuombwa radhi, asema yeye anajuwa kanuni zaidi ya miaka 30 na afikirii mtu atoke Simanjiro miaka kumi iliyopita halafu ajifanye eti anajua kuliko watu wengine. Kikao kimeghailishwa mpaka saa kumi jioni huku sintofahamu ikiendelea....
 
Sina hakika kama kuna lolote la maana tutakalolipata hapa kama hali itaendelea kuwa hivi!!!!!!!!
 
Amezidi upole sana... Hasa wabunge wa ccm hawana nidhamu...wanasababisha bunge linaahirishwa.. Na mchafuzi mkuu ni OLESENDEKA, NDIYE AMESABABISHA UPUUZI HUO. Kwa kujifanya analeta uchama.
 
Pandu kificho, ndo huyu wa Bunge la katiba? Namkubali. Kuongoza watu wote wale tena wengine hata hawaijui siasa sana na Elimu zao ni tofauti..
 
Hawa wabunge wa katiba hawajiheshimu hata kidogo. Utakuta Spika anaongea nao wanaongea.
 
BUNGE LA KATIBA MPYA LINASIKITISHA NA KUFEDHEHESHA SANA
1)Nidhamu za wahuska ni zero
2)Malumbano yasiyo na mantiki wakati mwingine
3)Kanuni na taratibu walizojiwekea hazifuatwi
4)Kelele kama watoto wa chekechea

vitukovituko tuu!
 
Katiba itapatikana kweli kwa mtindo huu wa wabunge kutetea maslahi ya chama, hasa ccm?
 
Leta mada ya maana kwenye jf na siyo ubabaishaji,usipende kubeza upinzaji wewe mtoto wa mkulima. Unajua waliong'ang'ania kudai katiba Mpya ni cdm. Nenda kacheze ngoma kwenu au kasome magazeti ya udaku. Usiposti tena mda humu jf ambazo za uchochezi
 
Kwani huyu mwanasheria mkuu wa Zanzibar siyo mnazi wa ccm? Mbona Ole Sendeka amemnanga hivo?
 
Ni wazi kuwa Wabunge wa Bunge la katiba kwasasa wameshindwa kujitambua nini kilichowapeleka Bungeni na hata kusahau yale yaliyowapeleka. Leo hii Bunge limehahirishwa Mpaka Saa Kumi Jioni ikiuliza sababu za kuahirisha ni fujo zilizotokea na baadhi ya Wajumbe wa Bunge hili kukataa kuzima Vipaza Sauti ili kuruhusu wajumbe wengine kuongea. Ni wazi kuwa wapo waheshimiwa wanaropoka ovyo........Mimi sioni kama kuna haja ya kuendelea kuwa na Bunge hili kwani hata katiba watakayokuja nayo itaendana na jinsi walivyo.........Wito Wabunge wa Bunge hili wajitambue na wajue wanaotuwakilisha tunauchungu kuliko wao wanafanya michezo Bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…