Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Mda huu nilikuwa naangalia Bunge la Katiba na limeahirishwa mpaka saa kumi kwa sababu ya vurugu. Mimi ninachoona kuna kila aina ya mipango ya kuhakikisha katiba haipatikani. Wajumbe wote wa bunge la katiba wanaonyesha utovu wa nidhamu kana kwamba wanafanana na watoto wa chekechea kwa kelele wanazopiga Bungeni. Pia inaonyesha Mwenyekiti ameshindwa kuendesha Bunge kwani anakubali kuyumbishwa na wajumbe. Mh Jk hawa watu hawana nia ya dhati kutupatia katiba mpya ila wana nia tu ya kupoteza muda. Kama inawezekana iwekwe sheria ya kuwakata posho pindi wanapolivuruga Bunge. Hilo linaweza kusaidia kupunguza usumbufu unaojitokeza. Mh Rais chukua maamuzi kuhusu hiki kinachoendelea Bungeni.
 
Yaani hao kwa kuchambana ndio wenyewe, mie jana namsikia watu wanazungumza na vipaza sauti vyao viko wazi vinaingiliana hadi sisi kwenye tv tunasikia mwingine alikuwa anahadithiana habari za jana yake, wengine watoto wao uko nyumbani waivyokuwa wasumbufu, mwingine ndio anaongea kwa sauti tumekuchoka anamwambia mbunge mwenzie anayepayuka kuchangia yaani kama kilabu cha pombe hawana hata aibu. utafikili vyuzi zao zimekatika naona mitambo ile inawatoa akili ovyo kabisa kichefuchefu tena mie naona hata aibu kulingalia.

Ni bunge la aibu kabisa hili watu wanakua kama totoz. Hiyo katiba sijui itakuaje Mungu saidia.
 
Natamani hili bunge livujwe tu ili tujipange upya kama huu u.puuzi utaendelea hivi. Manake kwenye kanuni tu tayari ishakuwa muziki, kwenye mjadala wa muundo ya serikali ya muungano si ndo itakuwa balaa?
 
Mliokuwa mnasema kuwa Rwanda, Kenya na Uganda wametutenga kwenye EAC sasa mnaweza kuona kilichowachosha. Yaani mwezi mzima wanaume na wanawake wa Kitanzania karibia 700 hawajaweza hata kumchagua mwenyekiti wa kuendesha vikao huku muda wa kazi nzima ukiwa chini ya miezi mitatu!!!!
 
Binafsi nilikuwa sijawahi kumuona Mh. Pandu Kificho akiongoza mkutano wowote. Kutoka moyoni,hakuna spika mwenye hekima niliyewahi kumuona katika umri wangu kama Kificho isipokuwa ni malezi ya hovyo sio ovyo waliyopata wabunge wetu toka kwa walezi wao. Mnaokataa kataeni habari ndiyo hiyo.

huyu mzee anaongoza kwa hekima sana
 
Binafsi nilikuwa sijawahi kumuona Mh. Pandu Kificho akiongoza mkutano wowote. Kutoka moyoni,hakuna spika mwenye hekima niliyewahi kumuona katika umri wangu kama Kificho isipokuwa ni malezi ya hovyo sio ovyo waliyopata wabunge wetu toka kwa walezi wao. Mnaokataa kataeni habari ndiyo hiyo.

Uko sahihi kabisa.Mazoea ya Sendeka kubebwa na spika na wenyeviti kwenye bunge la jamhuri yanamfanya ajisahau.Hii ni mara ya pili kaaibika kwa ajili ya kukurupuka.Juzi aliropoka kwa kelele nyingi kupinga article of union isiwekwe hadharani akaelezwa ile tayari ni public document.By design hakupaswa kuwa pale maana hakuwahi kuunga mkono katiba mpya ndio maana alimbana mwenyekiti wake kuhusu kukubali katiba mpya!Aibu iendelee kumwandama kwa kuwa lengo lake ni kuvuruga.
 
Maana wanapiga kelele bungeni na kuzomea ovyo kama watoto wa Kindagaten! Yaani hawana hekima wala busara! Mpaka wanakera! Wao wanadhani ukiishakuwa mpinzani basi ni kupinga tu hata kama huna hoja! Kibaya zaidi wanazomea kama wehu! Hawafai, wanakula hela za walipa kodi bure!

Unaleta mada kama vile uliyeangalia Bunge ni wewe pekee. Chuki zako kwa Chadema hata Sendeka akiongea hovyo au kutukana wewe unamwona ni wa Chadema. Kama kuna mwana Chadema alikugegedea vyako chuki yako iwe kwake sio kwa chama kiujumla.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Hakika kama Wananchi tutakaa kimya hawa wawakilishi sasa watafanya wafanyavo..............
 
Yote haya ni kwa sababu ya wingi wa wanasiasa...

Wengi wa wanasiasa huongea vitu kwa kutegemea maslahi ya vyama vyao..
 
Kuliko kupitisha kanuni zitakazo zaa katiba ya ccm bora liendelee kuvurugika tu!
 
Mliokuwa mnasema kuwa Rwanda, Kenya na Uganda wametutenga kwenye EAC sasa mnaweza kuona kilichowachosha. Yaani mwezi mzima wanaume na wanawake wa Kitanzania karibia 700 hawajaweza hata kumchagua mwenyekiti wa kuendesha vikao huku muda wa kazi nzima ukiwa chini ya miezi mitatu!!!!

Hii Nchi ni ya ajabu sana
 
MWENYEKITI NI DHAIFU...ANAEPINGA APINGE... Kuongoza baraza la wawakilishi kwa miaka 18 siyo hoja... Amwambie makinda na ndugai yanayowakuta!! Kikao cha Baraza la wawakilishi ndo uwezo wake..
 
ni aibu sana kwa watu wazima na wengi wao ni viongozi katika jamii hawana cha maana wanachodiscuss hapo.ukweli bunge la katiba lina maudhi sana ni mabishano yasokuwa na msingi na hata hamna kinachoendelea..haya mabilioni ya watanzania ambayo mnatafuna hapo Dodoma kweli itagarimu Taifa letu na hatutapata muhafaka wa hiyo katiba tunayoitaka kwa style hi!!!
 
Nakubaliana na mdau uliyemwita ole sendeka mbwa kwani ni bogus dog asiyestahili kuwa mbunge ata wa mbwa mwitu,anapenda kupinga kila kitu amabacho kinakinzana na CCM ata kama kina maslahi ya kitaifa.Na mshangaa sana mwenyekiti wa bunge hili kumpa nafasi mara Kwa Mara mtu asiyejua ata kujenga hoja hususani za kisheria,jamaa kutoka zenji kampa makavu live kwamba asione kila mtu anakili kama za watu wa kwao simanjiro huko.
 
Shida iko kwa maccm yule mmasai Ole sendeka kiti chake makalio yanawaka moto muda wote anataka kusimama kuongea pumba zake.

ndio shida ya mtu aliyezoa kuvaa shuka bila kuvaa chupi basi akijuwa kuvaa suti ni tatizo. ila huu ndio muhura wake wa mwisho 2015 ataisoma namba.
 
Huu tu ni mwanzo na ni wakati wa mijadala ya kanuni, je watu hawa wataweza likija suala la hoja za msingi zilizopo kwenye rasimu?
 
Back
Top Bottom