Mda huu nilikuwa naangalia Bunge la Katiba na limeahirishwa mpaka saa kumi kwa sababu ya vurugu. Mimi ninachoona kuna kila aina ya mipango ya kuhakikisha katiba haipatikani. Wajumbe wote wa bunge la katiba wanaonyesha utovu wa nidhamu kana kwamba wanafanana na watoto wa chekechea kwa kelele wanazopiga Bungeni. Pia inaonyesha Mwenyekiti ameshindwa kuendesha Bunge kwani anakubali kuyumbishwa na wajumbe. Mh Jk hawa watu hawana nia ya dhati kutupatia katiba mpya ila wana nia tu ya kupoteza muda. Kama inawezekana iwekwe sheria ya kuwakata posho pindi wanapolivuruga Bunge. Hilo linaweza kusaidia kupunguza usumbufu unaojitokeza. Mh Rais chukua maamuzi kuhusu hiki kinachoendelea Bungeni.