Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Bunge limekuwa la ovyo sana, mwenyekiti Wa muda bw. Kificho anatoa matangazo bila kufikiri mantiki ya tangazo lenyewe. Hakika kificho kaonyesha sura halisi ya wazanzibar. Ni mzigo kuongozwa na watu hao, sipo tayari tena kurudia makosa.

acha gubu mkuu.tena kwa taarifa yako Sita hawezi fika hata nusu ya Kificho,jamaa ni mwana sana
 
Mimi ninawasiwasi na wajumbe, najua bunge limeja jaa wasomi wengi na waelewa ambao tuna wakubali, lakini kwahili la kualibika kura saba bado sijalipatia ufafanuzi tena linatia haibu sana. Ongera mh sitta kwa ushindi.

Sio kualibika wewee! Wa wapi wewee?
 
Big up, timiza ahadi yako ya viwango, kasi uzalendo kuweka masilahi ya watanzania mbele.
 
Sita anasema asiyependa mafanikio yake anaweza akatokea Dirishani kama akipenda (Nadhani anamsema ATM ya makanisa na misikiti)

Kilicho nikera ni hao viti maalum hasa wa ccm kuligeuza bunge kitchen part.Wanashangilia kwa mayowe na vigelegele utadhan wapo sokoni?
 
Kilicho nikera ni hao viti maalum hasa wa ccm kuligeuza bunge kitchen part.Wanashangilia kwa mayowe na vigelegele utadhan wapo sokoni?
Mkuu, hakuna ushindi usio na furaha. Walishindwa kujizuia
 
Mkuu, hakuna ushindi usio na furaha. Walishindwa kujizuia

Chabruma nakubaliana na wewe 100%, lakini tufurahi na tutambue kuwa pale ni bungeni.sehemu pekee ya kupitisha sheria za kuliongoza taifa letu.
 
Sitta, ninakupa ushauri wa bure! You talk too much! Kificho ameweka standard mpya ya Spika (Mwenyekiti), so be careful, kazi yako ya nyuma inaweza kuingia mchanga. Biblia inasema katika MITHALI 10:19,"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili." Kificho yuko makini, hasemi maneno mengi, na ni mwangalifu sana katika kuchagua maneno ya kuzungumza. Mind you, kwa kila jambo sasa utapimwa katika mizani na kulinganishwa na Mwenyekiti wa muda, Kificho, na wala siyo Makinda! Mwenyekiti wa kudumu anatarajiwa na wengi, awe na uwezo na hekima zaidi, kuliko Mwenyekiti wa muda! Kumbuka kwamba kuanzia sasa, kila neno lako moja, lina tafsiri elfu moja, kwa maadui zako, na marafiki zako wa zamani! Neema ya Mungu ikufunike!

Ndugu yangu hakika umenena, ni maneno yenye ushauri mzito sana. Mungu amsaidie na kumuwezesha katika kila jambo
 
hakika nimefurahia ushindi wa mzee wa viwango samwel sitta.jioni yangu imekuwa njema sana.
 
Mkuu, hakuna ushindi usio na furaha. Walishindwa kujizuia

Mkuu, kwa maoni yangu ni kua bungeni ni sehemu yenye mkusanyiko rasmi wa wajumbe mbalimbali. Kwa hiyo (kwa maoni yangu) nadhani si sahihi kushangilia ushindi kwa kelele za kimtaani na kuchomekea nyimbo japo ni sahihi kufurahia ushindi. Mwisho.
 
Sitta huu ni mtihani kwako. Unapimwa kama juha au kama una sifa za kuwa Rais wa JMT.
 
Back
Top Bottom