Wakuu JF Amani iwe nanyi.
Bunge Maalum la katiba linaendelea kutufumbua macho as days goes on.
Leo tumekuja kujua kuwa Ndugu zetu wa Zanzibar pamoja na jeuri yao yote kumbe hawajiwezi na wamekiri kabisa kuwa wao Zanzibar kama Zanzibar hawawezi kufanya kitu bila Tanganyika.
Wamekiri kuwa hawajiwezi kabisa katika masuala mbali mbali, Umeme, Elimu, Madawa, Shule etc etc wengine mtakuja hapa kujazilizia.
Wameenda mbali zaidi na kusema kuwa wao hata wakipewa kiti UN Hawataweza kumgharimia huyo balozi wao huko ughaibuni.
Wa Zanzibar hao wanakiri kabisa kuwa ndani ya Miaka ya 50 ya Muungano wamefika hapa walipo kwa Fadhila za Tanganyika.
Haya yameelezwa na wabunge wa CCM kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar.
Waone
Barubaru Pasco,
Bobwe ,
dudus 50thebe n.k