Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Chabruma

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
5,660
Reaction score
1,780
Wadau,

Habari za Jumatatu, siku njema, siku tulivu hapa Dodoma. Hali ya hewa ni nzuri kabisa kwa siku ya leo. Joto kwa sasa ni nyuzi joto 20 na kwa siku ya leo inatabiriwa kuwa kutakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Baada ya kushuhudia viapo kwa wajumbe kuanzia siku ya Ijumaa na Jumamosi, zoezi hilo litaendelea tena leo asubuhi na litawahusu wale tu ambao hawakuwepo wengi wao wakiwa kule Kalenga kwa ajili ya kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana ambapo William Mgimwa wa CCM aliibuka kidedea. Nitumie fursa hii kumpongeza aliyeshinda na kuwapongeza pia washindani wake kwa kura walizopata.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kutakuwa pia na mjadala wa pamoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya. Katika mjadala huo, wataalikwa wataalam mbalimbali wa masuala ya katiba na historia ya Tanzania wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, tukio muhimu kwa siku ya leo ni kwamba, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba majira ya saa 10 jioni atawasilisha Bungeni Rasimu ya Pili ya Katiba kama sheria inavyomtaka. Aidha, inategemewa kuwa Warioba atasema machache kwa muda wa masaa mawili kabla ya tukio hilo la kukabidhi Rasimu hiyo. Hivyo siku ya leo si ya kuikosa hata kidogo.

Kama kawaida yetu, tutaendelea kuwaletea matukio yote yatakayojiri kuanzia saa tatu asubuhi hadi kukamilika kwake. Natarajia pia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wengine akina Skype, Simiyu Yetu, MaishaPesa, Pasco, Invicible, kbm, Deo Corleone, Mkuu ya Kaya na wengine wengi. Hadi wakati huo, Stay Connected

-------------------------------------

- Wadau, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta ameingia. Dua imesomwa na anatoa ufafanuzi juu ya ujio wa Rais na Mwenyekiti wa Tume. Kwamba kimsingi mtu ambaye anatakiwa aje kwa mujibu wa sheria ni mwenyekiti wa tume. Anawashangaa wanaoshinikiza Rais aanze. Kwamba ratiba ya Rais haimruhusu kuja Dodoma leo wala kesho. Anasema kuwa Watanzania watatushangaa tukae bila ya kufanya kazi hadi atakapofika Rais

- Sitta anasema kuwa wameshauriana na Warioba na wamekubaliana kama nilivyodokeza hapo juu kuwa ataongea na Bunge kwa muda usiozidi dakika 120 yaani masaa mawili. Kwamba baada ya hotuba hiyo ya Warioba, hakutakuwa na majadiliano jioni. Aidha, anasema kuwa bunge litamuita wakati wowote warioba au mjumbe mwingine wa tume kuja kutoa ufafanuzi juu ya mambo ambayo yatahitaji ufafanuzi

- Sasa kqnuni zinatengulwa ili kuruhusu Warioba kuingia Bungeni leo jioni

- Ratiba ya leo ni kama ifuatavyo

  1. Viapo
  2. Wimbo wa Taifa
  3. kusitisha bunge hadi saa 11 jioni kwa ajili ya kupokea Rasimu ya Katiba

- Kesho wabunge watapata semina ya kanuni kuanzia saa tatu hadi saa saba, watapumzika then wataendelea saa 11 hadi saa mbili usiku

- Ratiba ya jumatano ni kwamba watapokea wageni wawili toka Kenya kwa ajili ya kueleza uzoefu wao wakati walipofanya mchakato wa Katiba. Pia kutakuwa na mada kuhusu historia ya Zanzibar na Tanzania bara na historia ya Muungano. Kuna wataalam watatu toka Zanzibar na watatu toka Bara. Ratiba hiyo itaendelea hadi Alhamisi

- Rais amepangwa kuhutubia siku ya Ijumaa.

============================================================
UPDATES

BAUNGE limeahirishwa mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo. Ni kwamba ilipotimia saa 11 kasoro dakika tatu hivi, Mwenyekiti wa abunge Maalum, Sammuel Sitta aliingia ukumbini kuendelea na ratiba ya jioni. Kwa mujibu wa ratiba ni kuwa Mwenyekitk wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba alipangwa kuwasilisha Rasimu kwenye bunge Maalum. Na warioba alikuwa ameingia ukumbini tayari kwa kutimiza matakwa ya kisheria.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum alimkaribisha Warioba kulihutubia Bunge. Warioba naye akasogea kwenye kipaza sauti ili azungumze. Kabla hajafanya hivyo wabunge wa upinzani wakaomba muongozo wa Mwenyekiti. Mwenyekiti akasema kuwa hakuna muongozo kwani kazi iliyo mbele ni moja tu nayo ni kupokea Rasimu ya Katiba kutoka kwa mwenyekiti wa tume. Hata hivyo, wabunge karibu wote wa upinzani walisimama huku wakigonga meza. Kwa mbali walikuwa wanamshutumu Mwenyekiti kwa kumruhusu Jaji Warioba aongee kabla ya Rais kama kanuni invyosema. Pia walikuwa wanasikika wakilalamika kitendo cha Warioba kupewa masaa mawili tu ya kuongea badala ya manne mpaka matano. Hivi ninavyopost wqbunge wa upinzani wapo ndani ya ukumbi wa bunge huku wabunge wa ccm na baadhi ya wale 201 wakiwa nje ya bunge na wengine wamebaki ukumbini. Hiyo ndo hali halisi iliyojitokeza jioni hii. Bado hatujajua ni lini bunge litaendelea tena.

UPDATES

WABUNGE WAKIWA NJE YA BUNGE BAADA YA KIKAO KUAHIRISHWA
image.jpg
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    691.3 KB · Views: 838
Ahsante mkuu.Asubuhi hii kutakuwa na ratiba gani.Hivi mbunge mteule atahusika kwenye hili bunge la katiba au?
 
Wadau,

Habari za Jumatatu, siku njema, siku tulivu hapa Dodoma. Hali ya hewa ni nzuri kabisa kwa siku ya leo. Joto kwa sasa ni nyuzi joto 20 na kwa siku ya leo inatabiriwa kuwa kutakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Baada ya kushuhudia viapo kwa wajumbe kuanzia siku ya Ijumaa na Jumamosi, zoezi hilo litaendelea tena leo asubuhi na litawahusu wale tu ambao hawakuwepo wengi wao wakiwa kule Kalenga kwa ajili ya kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana ambapo William Mgimwa wa CCM aliibuka kidedea. Nitumie fursa hii kumpongeza aliyeshinda na kuwapongeza pia washindani wake kwa kura walizopata.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kutakuwa pia na mjadala wa pamoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya. Katika mjadala huo, wataalikwa wataalam mbalimbali wa masuala ya katiba na historia ya Tanzania wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, tukio muhimu kwa siku ya leo ni kwamba, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba majira ya saa 10 jioni atawasilisha Bungeni Rasimu ya Pili ya Katiba kama sheria inavyomtaka. Aidha, inategemewa kuwa Warioba atasema machache kwa muda wa masaa mawili kabla ya tukio hilo la kukabidhi Rasimu hiyo. Hivyo siku ya leo si ya kuikosa hata kidogo.

Kama kawaida yetu, tutaendelea kuwaletea matukio yote yatakayojiri kuanzia saa tatu asubuhi hadi kukamilika kwake. Natarajia pia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wengine akina Skype, Simiyu Yetu, MaishaPesa, Pasco, Invicible, kbm, Deo Corleone, Mkuu ya Kaya na wengine wengi. Hadi wakati huo, Stay Connected

Tuko pamoja
 
Ataapishwa na nani sasa wakati Makinda siyo spika.. Akae kwanza atulie
aalah, UNAJUA HATA MIMI NILICHUKULIA KIRAHISI TU KUWA KESHO ATARIPOTI KWENYE BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUMBE YEYE UTARATIBU WAKE NI TOFAUTI, AU KWA KUWA SPIKA YUPO BUNGENI WANAWEZA KUMUOMBA AMWAPISHE AU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU ANAWEZA KUMUAPISHA KWA AJILI YA BUNGE HILI MAALUMU TU.
 
Kwa kuwa spika yupo dodoma kuna uwezekano akaapishwa hata katika ukumbi wa msekwa.
 
aalah, UNAJUA HATA MIMI NILICHUKULIA KIRAHISI TU KUWA KESHO ATARIPOTI KWENYE BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUMBE YEYE UTARATIBU WAKE NI TOFAUTI, AU KWA KUWA SPIKA YUPO BUNGENI WANAWEZA KUMUOMBA AMWAPISHE AU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU ANAWEZA KUMUAPISHA KWA AJILI YA BUNGE HILI MAALUMU TU.
hivi kwani amekwisha fahamika?.
 
Thanks kamanda wetu,tuko na wewe wakati wote.Ameeeen.
 
- Wadau, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta ameingia. Dua imesomwa na anatoa ufafanuzi juu ya ujio wa Rais na Mwenyekiti wa Tume. Kwamba kimsingi mtu ambaye anatakiwa aje kwa mujibu wa sheria ni mwenyekiti wa tume. Anawashangaa wanaoshinikiza Rais aanze. Kwamba ratiba ya Rais haimruhusu kuja Dodoma leo wala kesho. Anasema kuwa Watanzania watatushangaa tukae bila ya kufanya kazi hadi atakapofika Rais

- Sitta anasema kuwa wameshauriana na Warioba na wamekubaliana kama nilivyodokeza hapo juu kuwa ataongea na Bunge kwa muda usiozidi dakika 120 yaani masaa mawili. Kwamba baada ya hotuba hiyo ya Warioba, hakutakuwa na majadiliano jioni. Aidha, anasema kuwa bunge litamuita wakati wowote warioba au mjumbe mwingine wa tume kuja kutoa ufafanuzi juu ya mambo ambayo yatahitaji ufafanuzi

- Sasa kqnuni zinatengulwa ili kuruhusu Warioba kuingia Bungeni leo jioni

- Ratiba ya leo ni kama ifuatavyo
  1. Viapo
  2. Wimbo wa Taifa
  3. kusitisha bunge hadi saa 11 jioni kwa ajili ya kupokea Rasimu ya Katiba

- Kesho wabunge watapata semina ya kanuni kuanzia saa tatu hadi saa saba, watapumzika then wataendelea saa 11 hadi saa mbili usiku

- Ratiba ya jumatano ni kwamba watapokea wageni wawili toka Kenya kwa ajili ya kueleza uzoefu wao wakati walipofanya mchakato wa Katiba. Pia kutakuwa na mada kuhusu historia ya Zanzibar na Tanzania bara na historia ya Muungano. Kuna wataalam watatu toka Zanzibar na watatu toka Bara. Ratiba hiyo itaendelea hadi Alhamisi

- Rais amepangwa kuhutubia siku ya Ijumaa
 
Ataapishwa na nani sasa wakati Makinda siyo spika.. Akae kwanza atulie
Tume ya Uchaguzi ikishakutangaza tayari wewe ni Mbunge. kwahy anaenda Dodoma kuhapishwa na Mzee Sitta kuwa mbunge wa Bunge la Katiba!!
 
Pamoja sana Chabruma, nipo hapa nafuatilia kwa makini
 
Last edited by a moderator:
Mambo yanavyokwenda bungeni si ya kupendeza ila nafuatilia, na kwa minajili ya kutovuruga mjadala huu nakaa kimya
 
Ratiba ya jumatano ni kwamba watapokea wageni wawili toka Kenya kwa ajili ya kueleza uzoefu wao wakati walipofanya mchakato wa Katiba. Pia kutakuwa na mada kuhusu historia ya Zanzibar na Tanzania bara na historia ya Muungano. Kuna wataalam watatu toka Zanzibar na watatu toka Bara. Ratiba hiyo itaendelea hadi Alhamisi

Wataalamu toka Tanganyika hawatokuwepo?
 
Mtatiro na Lissu wanaomba mwongozo wa Mwenyekiti kuhusu uhalali wa Warioba kupewa dakika 120 tu wakati wakenya wanapewa siku nne
 
Hapa ndipo pamenipa ugumu wa kuendelea kuchangia mjadala huu baada ya majibu ya Sitta
 
Mambo yanavyokwenda bungeni si ya kupendeza ila nafuatilia, na kwa minajili ya kutovuruga mjadala huu nakaa kimya
Mkuu, nimekupata vema sana. Tuvumilie tu hapa mkuu. Huu ni upepo tu
 
Back
Top Bottom