Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Wadau,

Habari za Jumatatu, siku njema, siku tulivu hapa Dodoma. Hali ya hewa ni nzuri kabisa kwa siku ya leo. Joto kwa sasa ni nyuzi joto 20 na kwa siku ya leo inatabiriwa kuwa kutakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Baada ya kushuhudia viapo kwa wajumbe kuanzia siku ya Ijumaa na Jumamosi, zoezi hilo litaendelea tena leo asubuhi na litawahusu wale tu ambao hawakuwepo wengi wao wakiwa kule Kalenga kwa ajili ya kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana ambapo William Mgimwa wa CCM aliibuka kidedea. Nitumie fursa hii kumpongeza aliyeshinda na kuwapongeza pia washindani wake kwa kura walizopata.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kutakuwa pia na mjadala wa pamoja kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya. Katika mjadala huo, wataalikwa wataalam mbalimbali wa masuala ya katiba na historia ya Tanzania wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, tukio muhimu kwa siku ya leo ni kwamba, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba majira ya saa 10 jioni atawasilisha Bungeni Rasimu ya Pili ya Katiba kama sheria inavyomtaka. Aidha, inategemewa kuwa Warioba atasema machache kwa muda wa masaa mawili kabla ya tukio hilo la kukabidhi Rasimu hiyo. Hivyo siku ya leo si ya kuikosa hata kidogo.

Kama kawaida yetu, tutaendelea kuwaletea matukio yote yatakayojiri kuanzia saa tatu asubuhi hadi kukamilika kwake. Natarajia pia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wengine akina Skype, Simiyu Yetu, MaishaPesa, Pasco, Invicible, kbm, Deo Corleone, Mkuu ya Kaya na wengine wengi. Hadi wakati huo, Stay Connected

-------------------------------------

- Wadau, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta ameingia. Dua imesomwa na anatoa ufafanuzi juu ya ujio wa Rais na Mwenyekiti wa Tume. Kwamba kimsingi mtu ambaye anatakiwa aje kwa mujibu wa sheria ni mwenyekiti wa tume. Anawashangaa wanaoshinikiza Rais aanze. Kwamba ratiba ya Rais haimruhusu kuja Dodoma leo wala kesho. Anasema kuwa Watanzania watatushangaa tukae bila ya kufanya kazi hadi atakapofika Rais

- Sitta anasema kuwa wameshauriana na Warioba na wamekubaliana kama nilivyodokeza hapo juu kuwa ataongea na Bunge kwa muda usiozidi dakika 120 yaani masaa mawili. Kwamba baada ya hotuba hiyo ya Warioba, hakutakuwa na majadiliano jioni. Aidha, anasema kuwa bunge litamuita wakati wowote warioba au mjumbe mwingine wa tume kuja kutoa ufafanuzi juu ya mambo ambayo yatahitaji ufafanuzi

- Sasa kqnuni zinatengulwa ili kuruhusu Warioba kuingia Bungeni leo jioni

- Ratiba ya leo ni kama ifuatavyo

  1. Viapo
  2. Wimbo wa Taifa
  3. kusitisha bunge hadi saa 11 jioni kwa ajili ya kupokea Rasimu ya Katiba

- Kesho wabunge watapata semina ya kanuni kuanzia saa tatu hadi saa saba, watapumzika then wataendelea saa 11 hadi saa mbili usiku

- Ratiba ya jumatano ni kwamba watapokea wageni wawili toka Kenya kwa ajili ya kueleza uzoefu wao wakati walipofanya mchakato wa Katiba. Pia kutakuwa na mada kuhusu historia ya Zanzibar na Tanzania bara na historia ya Muungano. Kuna wataalam watatu toka Zanzibar na watatu toka Bara. Ratiba hiyo itaendelea hadi Alhamisi

- Rais amepangwa kuhutubia siku ya Ijumaa.

Katika hao wataalam wa katiba na HISTORIA ya Tanzania , ingekuwa busara kama angealikwa mzee Mohammed Said, Mzee Moyo na Mzee Abdu Jumbe.
 
Viapo vimemalizika. Matangazo yanatolewa kuwa wabunge watumie geti kubwa kwa ajili ya usalama zaidi badala ya lile geti dogo mkabala na barabara ya Dodoma- Dar es Salaam
 
Katika hao wataalam wa katiba na HISTORIA ya Tanzania , ingekuwa busara kama angealikwa mzee Mohammed Said, Mzee Moyo na Mzee Abdu Jumbe.
Mkuu, hayo ni mapendekezo yako. Huenda katika hao walioalikwa, wamo pia hao uliowapendekeza.
 
Tangazo linatolewa kuwa wanachama wa UKAWA (Umoja wa Kambi ya Wapinzani) wakutane kwenye ukumbi wa Pius Msekwa mara baada ya kikao hiki
 
Viapo vimemalizika. Matangazo yanatolewa kuwa wabunge watumie geti kubwa kwa ajili ya usalama zaidi badala ya lile geti dogo mkabala na barabara ya Dodoma- Dar es Salaam

Pamoja sana mkuu
 
Bunge limesitishwa hadi saa 11 jioni. Nami pia niwage wadau na niwqombe tukutane hapo saa 11 jioni
 
Naomba kuweka hisia zangu wazi kuwa mchakato wa kupata katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi umevurugika hasa baada ya mambo ya uvyama kutawala mchakato mzima mpaka sasa.
 
Hivi hili jina Tanzania bara ni kitu gani? ni nchi au ni muunganiko wa Tanganyika bara na Zanzibar bara?
 
Hivi hili jina Tanzania bara ni kitu gani? ni nchi au ni muunganiko wa Tanganyika bara na Zanzibar bara?

Mkuu, utaumwa kichwa bure, inavyoonekana wanasiasa wameamua kutetea uanasiasa wao badala ya masilahi ya wananchi
 
nashukuru kwa taarifa nzur sana hii kwani nimeibiwa TV
na sijaona taarifa kwa wiki sasa nashukuru sana hapa jf
 
mimi naomba kujua ni wabunge wangapi bado kuapishwa hadi sasa (kama inawezekana)
 
Hapa Sitta kakosea kabisa. Hadi sasa wajumbe wa bunge la katiba wako kwenye maandalizi yaani uandaji wa kanuni, uchaguzi wa viongozi wa bunge hilo pamoja na viapo. Baada ya haya kufanyika ndipo bunge linaanza kazi ramsi ya kujadili katiba mpya na kazi hii inazinduliwa na rais.

Busara ndogo tu ilimtushota Sitta kitambua kuwa mwenyekiti wa tume ya kukisanya maoni/kuandaa rasimu ya katiba hawezi kuwasilisha rasmi rasimu kwa bunge ambalo bado halijazinduliwa rasmi na rais. Hii ni sawa na kukabidhiana rasimu vichochoroni. Kosa.
 
Mkuu, ulichokinena umeniwakilisha vyema kwa asilimia zaidi ya mia
 
Ngoma ikivuma sana mwisho upasuka sita kalewa sifa

Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
mimi naomba kujua ni wabunge wangapi bado kuapishwa hadi sasa (kama inawezekana)

List ipo kwa uongozi wa bunge, ni vigumu kwa mtu wa kawaida kufahamu unless uombe upewe majina ya walio bado kuapishwa...........lakini sio wengi sana; sana sana wale walioenda jana uchaguzini kalenga wale ambao hawajaapishwa tu!

Usiumize kichwa ndg yangu!
 
Back
Top Bottom