Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Tumeambiwa kanuni inamtaka Rais kuhutubia kwanza ndio maana nauliza kwanini ilazimishwe Warioba kuhutubia kwanza kinyume na kanuni?
Ni kweli Mkuu kanuni zinasema hivyo. Ila imetumika kanuni ya 85 kutengua kanuni husika
 
Nusu saa kabla ya muda uliopangwa, wabunge wameanza kuingia ukumbini
 
wakuu mbona tanesco wanakata daikika chache kabla warioba kulihutubia bunge au kamchezo?
 
Macho na masikio kwa Muadilifu Jaji Joseph Sinde Warioba......
 
Sasa natangaza rasmi kuweka hisia zangu kando ili nifuatilie updates from you mkuu.
Ahsante Mkuu. Tupo pamoja katika hili. Namuona Mtanganyika Original, Mchungaji Mtkila amekaa tuli kwenye kiti chake cha kila siku
 
Namuona Freeman Mbowe naye yupo ukumbini muda huu. Nadhani ameingia mchana huu akitokea Kalenga maana asubuhi sijamuona
 
Zito leo naona kapiga nguo nyeupe kabisa juu mpaka chini,
wajumbe kwa ujumla wanaendelea kuingia kwa kasi ngoja tusikie toka kwa warioba leo.
 
Mzee wa mvi, Edward Lowasa, Lipumba, Mbatia na wengine wamo ndani ya ukumbi wa bunge
 
Back
Top Bottom