Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Mwenyekiti amelazimika kusitisha shughuli za bunge leo jioni baada ya wabunge kukataa kusikiliza hotuba ya mwenyekiti wa tume ya Katiba. hii inaonesha pia Warioba ameamua kugoma kusoma kwani wazo la Sita lilikua isomwe tu.

Inadaiwa kuwa wabunge hawa wanataka protocol izingatiwe na Rais alifungue bunge kwanza na si vinginevyo hofu bila shaka ikiwa ni umuhimu wa hotuba ya Warioba utatiwa kampuni ikianza.
Yetu macho. tunaendelea kuona sura ya ule muhafaka unaotarajiwa na una sura inapambwa na matukio kama haya!

Bunge limehairishwa kwa muda.
 
Please, updates. Inakuwaje jioni hii wabunge wamchemsha Sita na Bunge kuahirishwa mpaka itakapotangazwa?
 
Kuna tetesi nambiwa hapa eti Warioba ameshindwa kuwasilisha Rasimu baada ya Wajumbe baadhi kuzomea....na Bunge limeahirishwa !.
hEBU TUPENI HABARI ,WENGI BADO TUPO OFISINI
 
Mkuu nini kinaendelea huko, naona utabiri wako unatimia kuwa inawezekana leo kukatokea mgawanyiko mkubwa.!

Sitaki kuegemea upande wowote, namkaribisha Chabruma atupe mtiririko zaidi
 
Last edited by a moderator:
Nimefurahi sana sana kuone wabunge wamechukua hatua ila nimeona kitu Warioba anaonekana amelazimishwa kufanya hivyon. Samwel Sitta hovyo kabisa alafu ndio awe rais au waziri mkuu.
Kama mambo yako hivi ndio maana ccm wanalazimisha kura ya wazi
 
Punde nimefungua TBC Tv channel nilichokishuhudia ni wajumbe kumshangilia jaji Warioba mfululizo kwa kugonga meza bira kikomo mpaka speaker akaamua kuvuja kikao. nini kilitokea?// naomba mnijuze wana jamvi
 
Si mnajifanya mna serikali kiasi cha kuamua kupuuza wananchi waliowapa hiyo ridhaa ya kuunda serikali ! Mlifikiria mtaburuza watu, halafu mu-enjoy utulivu....Yaani mbona bado sana !.

From now to 2015 CCM mtaona rangi zote !

Vyama vya upinzani wanatuletea mambo ambayo siyo.
 
Eti sita kwa ubabe anamwambia jaji aendelee kuwasilisha ivoivo na makekele akidai itaingia kwenye ansered, Jaji akaona us...nge akajiendea kukaaa.
 
Hii ni kali sasa na cjui tunaenda wapi laki tatu zinaliwa buree tuu bora tusitishe hili la katiba maana hatukuwa tumejiandaa kisaikolojia na suala hili
 
hii nchi ngumu!
aliokwambia si akueleze kila kitu?
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati m/kiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba akianza kusoma hotuba yake,wabunge kadhaa walianza kugonga meza na kuzomea bila kikomo.hali hiyo imemfanya m/kiti wa bunge mh. Sitta kusitisha shughuli za bunge hadi itakapotangazwa tena.
 
Back
Top Bottom