Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Ni kweli bunge limeahirishwa mpaka watakapotangaziwa baada ya jaji Warioba kukaribishwa kuwasilisha rasimu ya katiba lakini wabunge walikuwa wanagonga meza zao kuashiria kutoafiki kuwasilishwa huko, pia nimewasikia wengine wakisema kanuni zifuatwe.
 
This thing will take longer than expected!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Walisema hawata kubalu wasomewe rasimu kabla ta rais kufungua bunge rasmi.
 
Duh! Kweli watu wana mipango, hivi inakuwaje kuwaje mambo yanafanyika tu holela holela tu, na bado wao wanakomaa tu huko na mihela wanalamba? Kweli sie watanzania bado sanaa!
 
Vurugu hizi nilijua zitatokea kwani UKAWA tangu mchana walijipanga kuhakikisha Warioba hawasilishi kabla ya Rais kufungua ! Nimefurahi sana leo ! At least machungu ya Kalenga yamepungua kidogo, ingawa bado yapo !

Hiyo ni dalili Njema! Hapo kutajadiliwa vitu kwa umakini mkubwa bila kuchezeana. Kiti kimeshawafahamu wabunge mapema. Hiyo naiona ni nzuri.
 
Kanuni zinataka rais autubie bunge kabla ya warioba kuwasilisha rasmu ya katiba, bt CCM walipindua ili aanze Warioba then Rais aje baadae na kuvunja Nguvu ya warioba ndo maana wamepinga.
 
Hajazomewa isipokuwa baadhi ya
wajumbe walikuwa wanataka kwanza rais azinduwe bunge then walioba awasilishe rasimu

Wamefanya vyema kwani wanasaidia in future kusiwe na uvunjifu wa kanuni lakini kwa upande mwingine ni matatizo kwani wanalitia hasara taifa.so jk kama amenogewa na k huko .sometimes busara inahitajika
 
tatizo inaonekana ni wajumbe kutoka vyama vya chadema,cuf,nccr na wale wengine wa upinzani na makundi ya kiraia hawakubaliani na mabadiliko ya kanuni yaliyofanywa na mwenyekiti yanayomtaka jaji warioba kusoma rasmu ya pili ya katiba kabla ya rais kuhutubia bunge hilo.Kwa wao wanataka kwanza rais ahutubie bunge hilo ndipo jaji warioba apewe wasaa wa kuwasilisha rasmu ya katiba bungeni.
 
Anayevuruga huo utaratibu ni hoyo mwenyekiti wenyu ati Sitta, kauli huumba.

Asiukweoe huo nzigo ni wake na yeye ndo wa kuumaliza asituharibue hali ya hewa.

Kutumika hasa ukiwa mtu mzima ni jambo baya sana.
 
Shall we make it?
wameshindwa hata kumsikiliza wakiwa na maana kwamba wamegoma/hawataki.
kama mitoto ya chekechea vile.Bola tu bunge livunjwe kila mwananchi achukue sheria yake mkononi.
WANAUDHI...
 
mkuu uliona mbali sana.

Hapana mkuu, ujue leo sita alikua akijibu hoja kibabe huku wajumbe wakiwa kimya ila wakiwa na nyuso za kutoridhika nikahisi kuna bomu linasubiri kulipuka
 
Wabunge wanataka jaji warioba apewe muda zaidi na sio saa mbili kama alivyopendekeza sitta na mkumbuke jaji warioba ndio ana maoni mengi ya wananchi kumpa masaa mawili hataweza kuwasilisha Yale yote alikutana nayo wakati wa maoni sita anadhani hili ni bunge la ccm Mzee akili hamnazo
 
Hii ni kali sasa na cjui tunaenda wapi laki tatu zinaliwa buree tuu bora tusitishe hili la katiba maana hatukuwa tumejiandaa kisaikolojia na suala hili

631x300,000= 189,300,000 zimeondoka leo!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom