Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Hebu tuambieni ni kwa nini wabunge wamekataa kumsikiliza warioba?bado tupo maaofisini wenzenu

Kanuni inasema kabla Warioba hajawasilisha rasimu ya katiba lazima Kikwete ahutubie Bunge,Ma ccm kupitia Sitta wametengua kanuni wamelazimisha aanze Warioba ndio aje Jk. Wabunge wenye akili wamepinga hili swala kwa kupiga meza mfuliluzo hivyo kukoseka usikivu bungeni na hatimae Six kuairisha bunge hadi hapo itakopo tangazwa tena.!
 
Kuna mdudu ananyemelea Tanzania na amejificha ndani ya upinzani,

Niliowaona wakigonga meza kwa Fujo ni Mtikila, Mbowe, Tundu Lisu, Lusinde....wengine sikuwakariri sura. Nahisi hasira za Kalenga wamehamishia kwenye Katiba.
 
kuna nin nyuma ya hili? Naamin chin ya uongoz wa 6 suluhu itapatikana maana si kawaida kuwaona viongoz wangu mahil wakiwa wanyonge mbele ya wapinzani...nawaomben kwenye hili utaifa mbele uchama nyuma..mungu ibari tanzania.
 
Hii ni kali sasa na cjui tunaenda wapi laki tatu zinaliwa buree tuu bora tusitishe hili la katiba maana hatukuwa tumejiandaa kisaikolojia na suala hili

ndugu,usilalamike bila kujua kilicho nyuma ya panzia,ni hivi asubuhi alisimama mtatiro na zito zuberi kabwe,kuomba muongozo wa mwenyekiti kwamba ni kwanini mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba apewe masaa2 yakuwasilisha rasimu ya katiba, kwanini asipewe walau masaa3 yakujieleza na kutoa ufafanuzi wa mambo yaliyokuwepo kwenye rasim ya katiba, wakati kunasemina zilizotengewa siku4 je rasimu ya katiba siyo jambo kubwa kwa taifa? mwenyekiti akafunika, sasa jioni ihi ameonyeshwa trela,kwamba ubabe hausaidii bali ni ujinga,busara za mzee pandu zimekosekana,
 
wadau labda naomba mnisaidie kuna jipya gani ambalo hawa UKAWA wanatarajia endapo Mh. Rais atakuja kuzinduwa hilo bunge? kwa ufupi kuna tija ipi hapo??
 
tatizo inaonekana ni wajumbe kutoka vyama vya chadema,cuf,nccr na wale wengine wa upinzani na makundi ya kiraia hawakubaliani na mabadiliko ya kanuni yaliyofanywa na mwenyekiti yanayomtaka jaji warioba kusoma rasmu ya pili ya katiba kabla ya rais kuhutubia bunge hilo.Kwa wao wanataka kwanza rais ahutubie bunge hilo ndipo jaji warioba apewe wasaa wa kuwasilisha rasmu ya katiba bungeni.

OK hiyo naaza kuelewa sasa
 
Nimefurai sana wajumbe walipinga kuburuzwa na maamuzi ya sita na mgongo wa ccm kwa kuvunja kanuni njia ya kupiga makelele ni nzuri sana na warioba alipo amriwa na sita kusoma tuuu na makelele nae aligoma mpka sita akaona aihirishe kwa muda usiojulikana.safi sana ilitakiwa ndio raisi aanze leo kuhutubia ndio warioba awasilishe rasimu ya 2.ccm hawataki rasimu ya warioba wanatumia kila mbinu.tusubiri tuone mengi
 
Vurugu hizi nilijua zitatokea kwani UKAWA tangu mchana walijipanga kuhakikisha Warioba hawasilishi kabla ya Rais kufungua ! Nimefurahi sana leo ! At least machungu ya Kalenga yamepungua kidogo, ingawa bado yapo !

Ohoooo! Kumbe hoja yao ni rais ahutubie kwanza! Mimi nilidhani asubuhi waliridhiana na Kiti baada ya maelezo aliyoyatoa kabla ya kuliahirisha Bunge. Kumbe waliburuzwa! Hapo patamu, Sita akae sawa hata kwa maswala yenye utata.
 
Nimeona Jaji Warioba ametolewa nje chini ya escort ya mgambo wa bunge lakini ameoneka amesononeka sana kwani inaonekana hotuba yake imekataliwa sijajua waliompinga ni kundi gani????

La Mbowe, Mtikila, Lisu, Lusinde n.k ndiyo waliokuwa wanaongoza kufanya fujo.
 
Wabunge wanataka jaji warioba apewe muda zaidi na sio saa mbili kama alivyopendekeza sitta na mkumbuke jaji warioba ndio ana maoni mengi ya wananchi kumpa masaa mawili hataweza kuwasilisha Yale yote alikutana nayo wakati wa maoni sita anadhani hili ni bunge la ccm Mzee akili hamnazo

Mkuu kwa heshima kabisa naomba ni kwambie kuwa umepotosha jukwaa kinacho gombewa hapo mjengoni ni kanuni walizopitisha ni kwamba aanze Kikwete kurihutubia bunge kisha warioba lakini sitta kwa manufaa ya majangili kaamua kufanya kinyume chake yaani aanze Warioba kisha kikwete na sababu iliyo tolewa kwanini asianze warioba ni kwamba atakapo panda Jk kuhutubia atajibu mapigo kwa warioba na wabunge wa ccm itabidi wafate maoni/ushauri/mapendekezo ya mwenyekiti wao(mr Dhaifu)
 
Mzee sita ameanza kupwaya, au ili dili kaliandaa mwenyewe nn ili asionekane anapingana na wenzake, maana nae mafya mzee huyu.
 
Ohoooo! Kumbe hoja yao ni rais ahutubie kwanza! Mimi nilidhani asubuhi waliridhiana na Kiti baada ya maelezo aliyoyatoa kabla ya kuliahirisha Bunge. Kumbe waliburuzwa! Hapo patamu, Sita akae sawa hata kwa maswala yenye utata.

Au kuna mtego kwenye hlooo??
 
Sita amekwamba kuliongoza bunge lililosheheni watu wenye weledi, kazi imeanza, na hapo bado hatujafikia kifungu cha 37 na 38 cha kanuni na kabla hajakaa sawa kuna sura ya 6 kwenye rasimu ya katiba, tuwemo hadi bunge liwake moto
 
Back
Top Bottom