Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

La Mbowe, Mtikila, Lisu, Lusinde n.k ndiyo waliokuwa wanaongoza kufanya fujo.
Mkuu mwanzoni na mimi niliwalaumu ila nimemaliza kuongea na jamaa wawili walokuwa mjengoni (Siyo kutoka kambi ya upinzani) wamenambia kuwa ubabe wa Mzee Six ndo umeyasababisha haya. Kimsingi amekiuka kanuni kwa ubabe ndo maana yametokea haya. Kanuni za bunge hili maalum zinamtaka rais ahutubie na kufungua rasmi hili bunge maalum then ndo Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya katiba akabidhi na kutoa hotuba kwa bunge hili maalum. Sasa Mzee wa viwango kakiuka hili bila kuwashawishi wajumbe na matokeo yake ndo haya..... 189,300,000 Tshs kwa leo tu zimepukutika bila kazi ya maana!!!!

Inaumiza sana!!!
 
CCM ni baba wa demokrasia ndiye iliyoanzisha mchakato wa KATIBA, wapinzani mnataka kuharibu nia nzuri ya CCM kutuletea KATIBA nzuri
 
mkuu hoja yako nzuri lakini umeiweka si mahali pake!
Hapa ni kanuni zimebutuliwa ili warioba amtangulie huyu mzaramo ilhali uhalisia anatakiwa azindue ,na warioba awasilishe katiba mpira uanze

Hoja yake inaendana kabisa na majibu aliyotoa Sita kuhalalisha Mh. Warioba aanze kwanza. Iko mahali pake
 
Mkuu mwanzoni na mimi niliwalaumu ila nimemaliza kuongea na jamaa wawili walokuwa mjengoni (Siyo kutoka kambi ya upinzani) wamenambia kuwa ubabe wa Mzee Six ndo umeyasababisha haya. Kimsingi amekiuka kanuni kwa ubabe ndo maana yametokea haya. Kanuni za bunge hili maalum zinamtaka rais ahutubie na kufungua rasmi hili bunge maalum then ndo Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya katiba akabidhi na kutoa hotuba kwa bunge hili maalum. Sasa Mzee wa viwango kakiuka hili bila kuwashawishi wajumbe na matokeo yake ndo haya..... 189,300,000 Tshs kwa leo tu zimepukutika bila kazi ya maana!!!!

Inaumiza sana!!!

Inauma xana hivi wanaingia jf kweli hawa
 
Tukiwa shule walimu walitumia adhabu ya viboko kudhibiti kelele na fujo darasani sasa kwa kuwa wabunge wa bunge la katiba wamekosa nidhamu kabisa bila shaka adhabu ya viboko inawafaa sana kwani hawamuheshimu kiongozi wa bunge hilo.

Weee ujielewi kabisa na kujitambua....
 
CCM ni baba wa demokrasia ndiye iliyoanzisha mchakato wa KATIBA, wapinzani mnataka kuharibu nia nzuri ya CCM kutuletea KATIBA nzuri

Kumbe umesahau mpaka tunaingia katika mchakato katiba mambo yalikuwaje! Kwa ujumla ccm hawakutaka katiba akiwemo aliyekuwa waziri wa sheria na katiba na mwanasheria mkuu. ccm iliingia katika mchakato ikiwa haitaki katiba mpya na ilijua huku mbele itatumia mbinu zile zile inazotumia katika chaguzi na katiba inabaki ilele. Na hilo naona giza mbele, haitafanikiwa.
 
Kweli, hata mimi nina shaka naye. Anaogopa kutengwa na chama.

Sasa bandugu, kuna jambo ambalo hamtaki kulielewa. Sitta hamjasikia siku zote anawania naye kuteuliwa na Chama chake cha magamba kuwania urais mwakani? sasa itakuwa ajabu km kuna yeyote anayetegemea aende kinyume na matakwa ya wanaccm, kwa sababu ndio watakaompima na kuona km kweli analinda maslahi yao. Sita bado ana ambitions za kisiasa kwa hiyo kuna mabo ataogopa kuyafnya kwa kuhofia kuotekelezwa kwa ambitions zake. sema labda akipewa urais ndio atakuwa na uwezo wa kuwageuka wenzake na kufanya mabo kwa maslahi ya taifa badala ya CCM. kwa sasa hata km anaona ccm wanakosea itabidi aendane nao ili wasmuudhi. Ila huyu jamaa akipata urais anaweza kuwageuka CCM maan hatakuwa na cha kupoteza, ukizingatia umri wake.
 
CCM ni baba wa demokrasia ndiye iliyoanzisha mchakato wa KATIBA, wapinzani mnataka kuharibu nia nzuri ya CCM kutuletea KATIBA nzuri

Acha upunguani tuonyeshe kwenye ilani ya ccm wapi mlipoandika uundaji wa katiba mpya?
 
Hivi nani kauloga ule mjengo yani kila mtu mwenye akili timam akiingia mule anakuwa chizi au ndo zile ndumba za naniii alikutwa anawanga mule ndani
 
Mkuu usiumize kichwa kubishana na makapi yenye vichwa vya nazi, ni kupoteza nguvu zako bure.
Mkuu upoooo? Hawa wanasiasa wamekuja kutuharibia Bunge letu
 
Back
Top Bottom