Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Mbona unaongea vitu vya ajabu ajabu halafu wakati huo huo unajiita ni mmoja wapo wa wabunge la katiba !

Nyie mmetumia wiki tatu kutengeneza kanuni, halafu anakuja mpuuzi mmoja anavunja kanuni wazi wazi mchana kweupe, na watu ambao wapo responsible wanapomzuia asifnye hivyo, eti unadai wana agenda ya siri.....

Ndugu yangu, mbona huu ni mwanzo tu......mambo baaaaado sana ! Nakuhakikishia tutapata katiba tunayotaka wananchi wa Tz. Hatutakubali kabisa katiba ya CCM !

Naona hawa wajumbe toka vyama vya siasa hasa chadema na cuf wako na agenda yao ambayo bado hatuijui kabisa sielewi kwa nini wanataka rais aanze kuhutubia kwani warioba ni mkuu kuliko rais.
 
12493_505774686195127_955804782_n.jpg
 
CCM ni baba wa demokrasia ndiye iliyoanzisha mchakato wa KATIBA, wapinzani mnataka kuharibu nia nzuri ya CCM kutuletea KATIBA nzuri

Unajua kinachoendelea bungeni? Au umeamka tu ukajisikia ku'comment!
 
Sasa bandugu, kuna jambo ambalo hamtaki kulielewa. Sitta hamjasikia siku zote anawania naye kuteuliwa na Chama chake cha magamba kuwania urais mwakani? sasa itakuwa ajabu km kuna yeyote anayetegemea aende kinyume na matakwa ya wanaccm, kwa sababu ndio watakaompima na kuona km kweli analinda maslahi yao. Sita bado ana ambitions za kisiasa kwa hiyo kuna mabo ataogopa kuyafnya kwa kuhofia kuotekelezwa kwa ambitions zake. sema labda akipewa urais ndio atakuwa na uwezo wa kuwageuka wenzake na kufanya mabo kwa maslahi ya taifa badala ya CCM. kwa sasa hata km anaona ccm wanakosea itabidi aendane nao ili wasmuudhi. Ila huyu jamaa akipata urais anaweza kuwageuka CCM maan hatakuwa na cha kupoteza, ukizingatia umri wake.

Umesema sawa na hapo mwisho umemalizia vizuri kuwa UMRI wa Sita hauna cha kupoteza. Na ni kwasababu hiyo ya UMRI wala nisingependa tuwe na rais Mzee vile. Aijenge heshima kwa watanzania na baada ya hapo apumzike, tutampa heshima kama anazopewa Mzee Warioba.
 
Mkuu upoooo? Hawa wanasiasa wamekuja kutuharibia Bunge letu

Mkuu nipo ndiyo maana toka asubuhi nimeshindwa kushiriki kutoa update nikichelea kuchepuka na kuelemea kwenye hisia zangu.
 
Hawa wajumbe wa CUF na CHADEMA wanataka kuongeza siku ili posho iongozeke wameshasahau majukumu yao. Kama walikuwa na hoja ya msingi ilibidi waitoe leo asubuhi, wanatia aibu kwa Mbowe na Prof Lipumba wameshindwa kusikilizwa na wafuasi wao walipo mjengoni
 
Hii nchi sasa iko mikononi mwa genge fulani la watu ambalo sasa linataka kujinufaisha lenyewe, Watanzania tuamke bassiiii.
 
Kazi kupokea posho za bure tu. Nchi huliwa na wenye navyo waliovipata bure.
 
Unajua kinachoendelea bungeni? Au umeamka tu ukajisikia ku'comment!

Kilichofanywa na wafuasi wenu ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kuanzisha fujo huku wakisahau wajibu na majukumu yao katika mchakato wa kupata katiba mpya
 
Mkuu mwanzoni na mimi niliwalaumu ila nimemaliza kuongea na jamaa wawili walokuwa mjengoni (Siyo kutoka kambi ya upinzani) wamenambia kuwa ubabe wa Mzee Six ndo umeyasababisha haya. Kimsingi amekiuka kanuni kwa ubabe ndo maana yametokea haya. Kanuni za bunge hili maalum zinamtaka rais ahutubie na kufungua rasmi hili bunge maalum then ndo Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya katiba akabidhi na kutoa hotuba kwa bunge hili maalum. Sasa Mzee wa viwango kakiuka hili bila kuwashawishi wajumbe na matokeo yake ndo haya..... 189,300,000 Tshs kwa leo tu zimepukutika bila kazi ya maana!!!!

Inaumiza sana!!!

mama yangu wee sasa hizo pesa si wangepeleka kwa babu hangu kujenga visima vya maji? au kwa kujenga maabara za kisasa? duu kweli ubunge unalipa 2015 naenda kwa babu loliondo kunywa kikombe then naingia kugombea ubunge.
 
NEWS!!!
Rais JAKAYA KIKWETE kulihutubia
bunge maalum la katiba ijumaa
wiki hii.

Source: Clouds TV Facebook account
 
Hiyo mbona Sitta alitangaza tangu leo asubuhi !

Itabidi JK ajipange kuhutubia kabla ya hiyo ijumaa au kama hana muda basi Dr. Shein ahutubie kwani wabunge wanaojitambua wameshasema Warioba hatahutubia kabla ya Rais !

NEWS!!!
Rais JAKAYA KIKWETE kulihutubia
bunge maalum la katiba ijumaa
wiki hii.

Source: Clouds TV Facebook account
 
Back
Top Bottom