Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma leo March 08, 2014

Wakuu, kuweni na subira. Wabunge wanaendelea kuingia ukumbini. Mambo yakiwa sawa mtapata kila kitu kupitia JF
 
Mkuu, bado wabunge wqnaendelea kuingia ukumbini. Stay connected.

Watu wamejaa mazoea. Hawajali muda. Unakuta mijitu inachekacheka tu na mabegi yao mikononi. Utadhani haijui iendako.
 
Pamoja sana ndugu, binafsi nakutegemea maana kunako TV hadi sasa kimya
Hakuna matata ndugu. Nipo humu ndani na hakuna kitakachopita kisiripotiwe kama tunavyofanya siku zote
 
huenda watu wameshapiga mahesabu, waongeze cku ngapi ili wapate amount ile ile mliyowapigia kelele wasiipate.

Akili kumkichwa
 
Kunavitu vinawekwa sawa punde mambo yatakuwa sawa tu wala tusijofu sana wakuu.
 
Halafu hawa wajumbe hawa! Wakisema saa tisa wanaanza saa kumi, sijui shida nini aaaaghr!
 
Watu wamejaa mazoea. Hawajali muda. Unakuta mijitu inachekacheka tu na mabegi yao mikononi. Utadhani haijui iendako.
Sana tu mkuu. Hii hali ya mahudhurio hafiffu inaleta maudhi sana.
 
Hivyo vinavyowekwa sawa vitu gani, bunge linapaswa kuanza kwa muda uliopangwam, si kila wakati kupangua.... Nadhani ccm ndo wanasababisha haya.
 
huenda watu wameshapiga mahesabu, waongeze cku ngapi ili wapate amount ile ile mliyowapigia kelele wasiipate.

Akili kumkichwa
Siyo kweli mkuu yapo mambo ya kiutendaji tu lakini yatakuwa solved punde.
 
Halafu hawa wajumbe hawa! Wakisema saa tisa wanaanza saa kumi, sijui shida nini aaaaghr!
Mkuu, yaani suala la muda linawapita pembeni sana. Sasa hivi ni saa 10 kasoro dakika 20 na hali ya ukumbi haijawa nzuri
 
Hakuna matata ndugu. Nipo humu ndani na hakuna kitakachopita kisiripotiwe kama tunavyofanya siku zote

wewe dogo Chabruma, hakuna kitakachopita kisiripotiwe? Kama kinahusu mashetani ccm?Wewe ni buttliker wa magamba,inajulikana!!.
 
Last edited by a moderator:
Hili ni bunge la maajabu na kuna watu nadhani watakuwa wanajisikia vibaya kuwemo maana walionekana kupinga tangia mwanzo lakini hawana jinsi.
hebu fikiria, wanataka kura za wazi lakini majadiliano yao yawe ya siri! Utadhani ni binadamu kutoka kuzimu.
 
image.jpg
Wabunge wanaendelea kuingia Bungeni. Bado sijamuona Mwenyekiti na watu wengine kama akina Mbowe, Mbatia, Lipumba nk
 
Kama kawaida yao ikifika saa kumi na mbili wataanza ooo njaa zinauma, mara ooo twende tukale, mara ooooo.... yaani blah blah kibao ila kodi zangu wanaziteketeza bure kabisa yaani nikifikiria PAYE, VAT na makodi mengineyo ya ajabu ajabu nakosa raha kabisa.

Labda kwa kua miafrika ndivyo tulivyo? Nyani Ngabu hebu kuja hapa utupe maoni yako kuhusu mwenendo wa wajumbe wetu walioko bungen.
 
Last edited by a moderator:
Bunge lisilozingatia muda. Na maendeleo yetu ndio maana yakusuasua!
 
wewe dogo Chabruma, hakuna kitakachopita kisiripotiwe? Kama kinahusu mashetani ccm?Wewe ni buttliker wa magamba,inajulikana!!.
Mkuu, katika suala hili la Katiba, tofauti zetu ziwekwe kando na ndo maana JF wametuwekea Jukwaa la Katiba Mpya ili tusichanganyane kama inavyokuwaga kwenye lile jukwaa letu la siasa
 
Back
Top Bottom