"
Kalamu1, post: 34606549, member: 494040"]
Nimesoma sehemu zote za bandiko, sikupata pendekezo mbadala, kati ya vyama vya upinzani "kushiriki au kutoshiriki" uchaguzi 2020.
Pendekezo lipo wazi.
Hakuna ushindi wa aina yoyote nilieleza kwanini. CCM wana NEC yaani tume ya uchaguzi.
Hakuna shaka ipo upande wao. Kikwete alibadili tume wiki moja kabla ya uchaguzi. Hilo tu linaeleza.
Polisi wapo upande wa CCM hakuhitajiki ramli.
Bushiru na Pole pole wanaweza kufanya mikutano ya wazi. Zitto na Lema wanaishia mahakamani.
Vyombo vingine kama msajili wa vyama haviwezi kusema lolote kwa UVCCM hatutegemei miujiza.
Kwa kushirikiana na Lipumba na uzembe wa viongozi wa iliyokuwa CUF, matokeo yanajulikana, Maalim shahidi
Kwa hiyo ikanibidi nirudi kwenye mistari hiyo hapo miwili na kuisoma kwa makini kuangalia busara zake. Sikuziona!
Ni kweli kuna nyakati busara hazionekani bali zinafikirisha tu.
Mtu akisema Wapinzani hawawezi kushinda hata kwa dawa na hata Bungeni hawatazidi 10 kuna busara hapo.
Yaani, CCM itakuwa imepata ushindi bila kujali kama vyama vingine vitashiriki au havitashiriki kwenye uchaguzi huo, mfano ukiwa ule wa serikali za mitaa.
Ndipo busara inapoingia, kwamba unaweza kurudi hatua 5 nyuma ili uweze kuruka kiunzi.
Unachaguo la kuchechemea na kukwama katika kiunzi.
Kususia uchaguzi si ushindi kwa CCM ni dhahma.Kususia uchaguzi wa mitaa kumezaa matokeo mazuri. Kwanza, kunawafanya wananchi waelewe wapi kuna tatizo.
Pili, kumesaidia sana kuwalazimisha viongozi kuongelea uchaguzi mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Hii maana yake ni kuwa jumuiya ya kimataifa imeona na inatafakari ndiyo maana siku hizi utasikia ''uchaguzi utakuwa wa haki na huru''. Hayo yanasemwa sasa na Wapinzani wanaitwa mezani.
Hii maana yake ni moja, tayari umma na jumuiya ya kimataifa zimeona tatizo. Hivyo wapinzani hakupoteza.
Hizi jitihada za kuongea na akina Mbatia na Lipumba ni katika kuhakikisha uchaguzi haususiwi.
Kama itatokea basi iwe chama kimoja na hilo haliwezi kuwa tatizo.
Katika kuhakikisha hayo kuna ''msaada'' wa aina fulani utatolewa.
Ushindi kwa CCM unaweza kukosekana kwa njia moja pekee kama vyama vya upizani (soma CHADEMA) wataweza kuwashawishi wananchi uchaguzi huo usiwepo.
Nashangaa kwanini hukuona busara hii ambayo kimamtiki nimeieleza vizuri.
Suluhu hapa ni kutoshiriki uchaguzi hadi uwanja wa siasa uwe sawa
Hata CCM wakishinda watakuwa wana ushindi legal usiokuwa na political legitimacy.
Tawala za duniani zilizoanguka katika sanduku la kura au kwa njia nyingine ni kwa kukosa political legitimacy.
CCM wanajua hilo ndio maana chaguzi za mitaa walitaka watu wajiandikishe ili kuwe na political legitimacy.
Hawawezi kutangaza asilimia 100 bila uwepo wa wapiga kura.
Hata wakiwepo idadi ina justify kama kuna political legitimacy.
Nchi ya watu milioni 45 wakipiga kura watu milioni moja hakuna political legitimacy
Baada ya kuona ipo shaka ya political legitimacy, CCM wamejitafakari kwamba uchaguzi mkuu ukikosa political legimacy huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho. Ndiyo haya ya kina Mbatia yanafanyika.
Hofu ya CCM si kushindwa, wana uhakika 100% kwa kutumia vyombo vya dola kama alivyobainisha KM wa CCM Bushiru.
Hofu ya CCM ni kukosa political legitimacy na ndiyo weakness yao ambayo ni strength ya Wapinzani.
JokaKuu Pascal Mayalla